Prince Tumbo
JF-Expert Member
- Apr 5, 2013
- 910
- 247
Dr H. Makyembe miaka michache tu iliyopita alikuwa ana haiba, heshima,ushujaa na uzalendo ndani na nje ya bunge ambao watanzania nadhani bado tunakumbuka.
Tume yake iliyompukutisha Edward Lowasa na Governer wa BOT kipindi hicho bwana Balali,aliye-assume amefariki dunia ( yupo hai) ni baadhi ya matunda ya uzalendo wake. Hakika kipindi hicho alikuwa NURU ndani CCM, hakuwa shabiki wa chama lakini alisimamia ukweli alioamini japo hakupendwa na wabunge karibu wote ndani ya CCM kwa kazi yake.
Mwakyembe yule...Sio huyu tulienae, AMELOGWA NA NANI?. Tuamini kwamba alikuwa hivo kwa maslahi ya taifa na sasa yuko kwa maslahi ya chama chake CCM?..
Tuamini kwamba wabunge wa CCM hawatetei tena maslahi ya taifa bali CCM? Ni kwa nini hatowi cheche zake dhidi ya fedha zetu zilizoko Uswiss? Hajasikia kwamba Tembo wanakwisha kwenye hifadhi kwa ujangili wa kinana?
Haoni kazi wanayofanya Filikunjombe na Kangi Lugola?
Aseme aliyemloga (alitishwa? Kule kupewa uwaziri? Alipata alichokuwa anahitaji?).
Kweli amelogwa.