Mwakyembe na uchakachuaji wa ripoti ya bandari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe na uchakachuaji wa ripoti ya bandari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiranja, Oct 21, 2012.

 1. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Waziri wa Uchukuzi, Dr. Mwakyembe, amethibitisha kuwa anachakachua ripoti ya Tume aliyoiunda kuchunguzz tuhma za bandari baada ya kuwaambia waandishi wa habari kwamba leo ndio amepokea baada ya kuirudisha kwa tume aliyoipokea awali ma pia amesema atahoji watu waliokataa kushirikiana na tume aliyoiunda na kuipa wiki mbili lakini ikatumia miezi miwili kwa gharama za Bandai. Sina hakika kama ana mamlaka kuunda Tume. Tundu Lissu alisema Waziri hana mamlaka kisheria kuunda tume, pale Nchimbi alipounda ya kuchunguza mauaji ya Mwangosi:) mmoja wa waliokuwapo kwenye Press Conf ya Mwakyembe anasema;

  "Hiyo ya kupokea report mbili kwa siku tofauti ni uthibitisho tosha kuwa kumekuwa na uchakachuaji mkubwa kwenye report hiyo. Hii kuwaita watu wengine ambao hawakuhojiwa na kamati offisini kwake ili awahoji mwenyewe *si utawala bora kabisa na tafsiri yake ni witch hunting yaani kuwindana wakati biashara ikiendelea kudorora."

  Tanzania Daima la jana liliandika:

  Mwakyembe kuanika kiini cha hasara Bandari
  na Mwandishi wetu
  WAKATI Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, anakutana na watendaji
  wake na waandishi wa habari, imethibitika kwamba Mamlaka ya Bandari Tanzania
  (TPA) imepata hasara kubwa.
  Taarifa za uhakika ndani ya TPA zimeeleza kwamba kwa kipindi cha mwezi
  Septemba, 2012 mapato ya Bandari yameshuka kwa asilimia 13.3, sawa na shilingi
  bilioni nane.
  Mapato hayo kwa mujibu wa maofisa wa TPA yameshuka kutokana na kuzorota kwa
  ufanisi bandarini uliotokana na uwezo duni wa uongozi mpya uliosimikwa na
  Mwakyembe katika mazingira tata.
  ”Ufanisi umepungua sana na sasa mwezi Septemba tumepoteza biashara kwa kiasi
  kikubwa kutokana na huduma kudorora. Oktoba hasara inaweza kuwa mara mbili
  kama tutaendelea kufanya siasa katika sekta nyeti ya bandari,” anasema ofisa
  mmoja mwandamizi bandarini.
  Ofisa huyo pamoja na kumsifia Mkurugenzi mpya wa TPA, Madeni Kipande,
  amesema kutokana na kutokuwa na uzoefu katika sekta ya bandari, upo uwezekano
  mkubwa wa kuharibiwa sifa yake ya uadilifu na uchapa kazi.
  ”Namfahamu Kipande si mtu mbaya na ana uwezo, lakini kwa dude kubwa kama
  bandari hatoweza na hasa ikizingatiwa ameingizwa kisiasa na anapokea amri za
  kisiasa badala ya kitaalamu. Hatari nyingine ni mahusiano yake ya kidugu na
  uongozi wa juu wa nchi yanaweza pia kuipaka matope serikali,” anasema.
  Kipande ambaye alitokea serikalini, ametajwa kuwa anatokea mkoani Pwani,
  pamoja na yeye mwenyewe kusema mahusiano yake na uongozi wa juu serikalini
  yamemponza kukosa nafasi nyingi serikalini badala ya kuwa msaada kwake na
  kwamba TPA amekwenda kibahati.
  Katika kikao hicho, Dk. Mwakyembe anatarajiwa kutoa taarifa ya tume aliyoiunda
  kuchunguza tuhuma mbalimbali zinazowakabili viongozi wa TPA, tume aliyoiunda na
  kuipa wiki mbili kumaliza kazi, lakini ilifanya kazi kwa zaidi ya miezi miwili kwa
  gharama za TPA.
  Waziri Mwakyembe anaelezwa kupokea ripoti hiyo na kuichambua, kabla ya
  kumshirikisha Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa safarini nchini Oman, alikorejea juzi
  Ijumaa.
  Rais Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya uteuzi ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPA,
  Ephraem Mgawe, aliyesimamishwa.
  Taarifa za ndani ya serikali zimeeleza kwamba kumekuwa na shinikizo kutoka
  serikalini kutaka uongozi uliosimamishwa urudishwe kazini kwa masilahi ya taifa
  kutokana na kuonekana pengo kubwa katika mfumo wa bandari.
  Tayari kumekuwapo taarifa za kuwapo hofu ya kuchakachuliwa kwa ripoti hiyo na
  tayari baadhi ya viongozi waliosimamishwa wanatarajiwa kuhamishiwa maeneo
  mengine.
  Imeelezwa kwamba tayari Dk. Mwakyembe amekwisha kuandaa nafasi SUMATRA
  ambako anapanga kuwahamishia viongozi hao.
  Imeripotiwa katika baadhi ya magazeti kwamba huduma nyingi zimeanza kuzorota
  katika Bandari ya Dar es Salaam, na kusababisha usumbufu kwa wateja huku baadhi
  ya makampuni ya meli yakihamia bandari nyingine na wanaobaki Dar es Salaam
  wanahamia TICTS.
  Mwakyembe aliunda tume hiyo Agosti 24, 2012 na kuipa wiki mbili lakini ilichukua
  karibu miezi miwili ikiendesha shughuli zake katika hoteli moja kubwa Dar es Slaam
  lakini imegubikwa na utata mkubwa kutokana na inavyoendesha shughuli zake.
  Taarifa za ndani ya TPA zimeeleza kwamba uongozi mpya wa bandari kwa sasa
  umeshindwa kufanya kazi kutokana na kuendelea kuwapo makundi ndani ya
  mamlaka hiyo, huku baadhi ya waliochukua nafasi wakiwa hawana uwezo wala
  uzoefu katika sekta husika.
  Kabla ya kuunda tume hiyo, Dk. Mwakyembe aliwasimamisha kazi viongozi wote wa
  TPA, akiwamo Mkurugenzi Mkuu, Ephraim Mgawe akiwatuhumu kuhujumu uchumi
  na kukaidi maagizo ya Ikulu, tuhuma ambazo tume inahaha kuzichimba kila kona,
  ikiwa ni pamoja na kurubuni baadhi ya watu.
  Pamoja na Mgawe, wengine waliosimamishwa kazi ni naibu wakurugenzi wakuu
  wawili wa TPA waliotajwa kwa jina moja moja la Mfuko na Koshuma. Pia yumo
  Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassian Ng’amilo, Meneja wa Kurasini Oil Jet,
  Meneja wa KOJ na Terminal Oil Engineer, ambao hawakutajwa majina.
  Mwakyembe alimteua Madeni Kipande ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Barabara
  katika Wizara ya Ujenzi kukaimu nafasi ya Mgawe.

  www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=41757
   
 2. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2012
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Bandari inazidi kusuasua kutokana na maamuzi mabovu yenye muelekeo wa kisiasa badala ya kibiashara. Kinachooneka kwenye swala la Tpa ni watu kujipanga kupata ulaji kwenye miradi mikubwa iliyoko kwenye Port Master Plan kabla ya 2015!!! Ni mkakati wa kuweka watu kwenye nafasi za juu Tpa kwa makusudi hayo.
   
 3. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45

  Kama Mwakyembe atachakachua kweli hii ripoti (jambo linaloonekana dhahiri kuwa kweli) basi tutawapa nguvu mafisadi wa Richmond, ambao watasema ndio kawaida yake na hivyo kuwapa nguvu mpya katika kuichukua nchi kifisadi. Isijekuwa mtandao unamchezea Mwakyembe kummaliza, ni bora akakubaliana na Tume aliyoiunda mwenyewe badala ya kuchakachua
   
 4. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu huyu jamaa hajui mafisadi wana mtandao mpana.
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Zaidi ya blah blah sijaona namna alivyochakachua iyo report.
  Ivi ninyi mnaomtetea uyo aliyetolewa mlishawai kupitisha ata toothpick bandarini ili uone kero za hii bandari yetu!
  Personally nimeibiwa vitu vingi pale na nimefuatilia ni network inayojulikana na wakubwa wanakula percent zao!
  Acha mapato ta TPA yashuke as long as we are in the course of trying to be on the right track
  Usikute ni sabotage ya wafanyakazi waliopo of which is quite easy dealing with them due to the unemployment rate that Tz is in right now!
  Chezea mshahara usichezee kazi
   
 6. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,743
  Likes Received: 1,804
  Trophy Points: 280
  Mtu mchapakazi ccm huwa hawamtaki.NCHI yao wenyewe wanaichakachua. wengine wamerudi jana kutoka uarabuni lakini jumatatu utawasikia wakitangaza safari nyingine ya marekani au Japani yaani ni full kuihujumu Nchi yao.uwepo wa Mweakyembe huko kuna wakera wengi!!
   
 7. Nipisheni

  Nipisheni Member

  #7
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Njowepo acheni masiala na hili dude Bandari,Mwakyembe aturudishie majembe yetu,kinyume na hapo bandari inatafutiwa mbinu ichukuliwe na watu wachache.Taarifa tunazo kwamba huyo Kipande ni shemeji yake KJ,anatokea pale karibu na Mbwewe ukipita Wami.Tukikubaliana na maamuzi haya ya Mwakyembo basi tunaruhusu utawala wa watu wa Bagamoyo na kitakachofuata ni utawala wa kisultani.
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  chezea bandari nyie...pale hawezi kitu atakwaa kisiki
   
Loading...