Mwakyembe: Mwanasheria anayebaka sheria kusudi

tina pole sana. maana naona nyie mmeamua kula sahan moja na mwakyembe ..ha ha ha ...sasa huku jamiiforums ndo pccb? peleka ushahid huko.siyo kuja kila siku hapa kumsema mwakyembe kisa amewabana au mmeshndana.peleken hizo data kunakohusika then mpendekeze nan anafaa ..
 
kuwa na id unknown si hoja Tina utaishia pabaya na genge lenu lote la wala rushwa hapo bandarini kwa sababu mmoja ukitiwa ndani utaeleza na washirika wako(all conspirators)
 

Na wewe pole sana. Kama jina lako linavyojielekeza huwezi kuwa chizi ukawa na maarifa!!!! Soma kwa makini uelewe hoja!
 

Mkuu angalao umetoa changamoto kwa mada husika sio wanaokwepa hoja kwa majibu mepesi na kejeli za kitoto. Tuzame kwenye hoja.


Hapa hoja yangu sio kutaja majina ya watu bali kuibua uvunjaji wa sheria unaofanywa na- Mwakyembe ili umma wa Watanzania wafahamu huyu jembe lao la zamani limekuwa butu.- Hivyo vyombo husika kama vile CAG, Usalama wa Taifa na TAKUKURU ni wajibu wao sasa kuchunguza ukweli na kuchukua hatua muafaka. Majina yote ya wahusika yanajulikana, lakini hoja hapa sio hao wahusika kuwepo au kutokuwepo bali huu ufisadi unaofanywa na Mwakyembe na Kipande bila kuzuiliwa na wenye mamlaka ya juu.- Sakata la ardhi ya Kisarawe linamhusisha Mh. Turky ambaye ni mbunge kutoka Zanzibar. Shinikizo la kununua ardhi hiyo alilitoa Mwakyembe kwa bodi ya TPA huko Mtwara mwezi wa Desemba. Suala kama hili kama kweli kuna- dhati ya utawala bora kwa vyombo husika, ni dhahiri kuwa uchunguzi utabaini hali halisi. Mimi dodosa hizi ninazipata kutokana na nia yangu ya kulinda rasilimali za nchi hii, na kuwaibua mafisadi kama Mwakyembe ambao wamevaa ngozi ya kondoo lakini kumbe ni mbwa mwitu.

Wajumbe wa bodi na sifa zao ni suala tu la kuzitafuta na zinapatikana bila taabu.- Hapa hoja ni kuwa uteuzi wa Mwakyembe umezingatia urafiki na uswahiba na sio sifa na uzoefu wao.- Uchambuzi wa kina kuhusu wajumbe hawa nilishaufanya kwenye angalizo langu la awali.- Kioja kikubwa ni kwamba Mwakyembe kavunja sheria mama ya TPA kwa kumteua mfanyakazi wa TPA ambaye ni kiongozi wa wafanyakazi bandarini kuwa mjumbe wa bodi hiyo, ili kumfunga mdomo, na pia kulinda maslahi ya Mwakyembe na Kipande.- Sheria mama ya TPA inakataza mtu mwenye maslahi yanayokinzana (conflict of interest) kuwa mjumbe wa bodi ya TPA. Hii sio siri wala majungu bali ni sheria ambayo Mwkyembe alipashwa kuizingatia. Ukiachilia mbali kuvunja sheria kwa ajili ya conflict of interest, mjumbe huyu wa bodi Edmund Njowoka kazi yake ni mfagizi, na alipokuwa Dar port alifanya kazi kama mfagizi wa maeneo ya nje na wakati mwingine kwenye vyoo. Sasa kweli mtu wa aina hii ambaye hakwenda shule kabisa, atatoa mchango gani katika masuala mazito ya TPA ili kuisaidia iende mbele? Hili nalo likifanyiwa uchunguzi wa kina, kila kitu kitajulikana, na wala sio majungu.

Kuhusu unyanyasaji wa kinjisia unaofanywa na Kipande kwa wanawake wa TPA, huo umejikita sio tu kwenye ngono bali pia anawanyanyapaa wanawake wote kutoka ngazi ya chini hadi juu ndani ya- TPA.- Hata wakifanya nae ngono, mwishowe anakuwaanika na kuwaumbua maungo yao yalivyo kwa washikaji wake akiwa kwenye mabaa. Ripoti ya Bodi ya TPA- iliyotolewa na John Ulanga kabla kuvunjwa mwezi Septemba 2013,- kwa kuwa walitaka kumdhibiti Kipande- ambayo pia nilishaitoa ili Watanzania mjionee jinsi Mwakyembe alivyowasaliti, hasa kuona ni jinsi gani- Mwakyembe kaigeuza TPA kuwa shamba la bibi kwa kumtumia KIpande ambaye mtaji wake mkubwa ni matusi ya nguoni kwa kila mtu, yaani wateja, wadau, wafanyakazi, wanawake, wakubwa zake, n.k. ilishatoa list ya wanawake waliodhulumiwa haki yao na Kipande.- Pia taarifa za magazeti mbali mbali zimeonyesha jinsi gani Kipande anawahamisha mabinti ambao wanakataa kuridhia haja zake za ngono kwa kuwapeleka bandari za maziwa ambako ajira zao (posts) wala hazipo kwenye ikama.- Hili suala la unyanyasaji wa wanawake TPA ni zito na tunatoa wito kwa Bi Sofia Simba, Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto kufanya uchunguzi wa kina ili ikithibitika basi hatua dhidi ya Kipande zichukuliwe haraka.- Karne hii ya 21 sio ya kutumia mfumo dume kuwakandamiza kina mama, dada na mabinti zetu, bali ni haki sawa kwa wote.

Hitimisho langu sio jepesi kama unavyodhani, bali hii ni njia ya kufuata sheria ili haki itendeke.- Kwa bahati mbaya, sina uwezo wa kuhakiki uozo unaofanywa na Mwakyembe kwa kumtumia Kipande na bodi ya Wakurugenzi TPA kwa asilimia mia moja, lakini Mwanasheria Mkuu na Jaji kiongozi kwa kutumia vyomba kama vile TAKUKURU, CAG, na Usalama wa Taifa, Tume ya Haki za Binadamu, n.k wanao uwezo wa kupata ukweli kuhusu kashfa lukuki zilizoibuliwa dhidi ya Mwakyembe na KIpande ili wachukue hatua zitakazoinusuru taasisi hii muhimu sana kwa TZ na majirani zetu.
 
Last edited by a moderator:
Hii ndio Tanzania, ukifanya kazi kwa bidii/ uadilifu katika ofisi za umma watu watakutafutia zengwe tu, nahisi jamaa amewabana sana mpaka mmemuwekea mitego na bahatimbaya labda yeye amenasa.
Tuhuma ni tuhuma, pelekeni malalamiko kwenye vyombo husika.
 
Watanzania wana tabia moja ambayo mie huwa inanikera sana na wengi wao wenye tabia hii tuko humu JF. Kitu kikisemwa na somebody ambaye hajulikaniki kama hiki basi tutapinga kwa namna tunazozijua sisi ila kwa kitu hiki hiki kije kisemwe Bungeni na Mbunge let's say mtu kama Mnyika au Kange Lugola basi watu hapa JF tutakuwa kama vile bendera fuata upepo na kuwa support wabunge na kumkalia kooni mwakyembe

Inshu kama Operation Tokomeza, Epa, Richmond iwapo ile ripoti ningeiandika mie C.T.U na kuja kuiripoti hapa watu wangenisakama kama mnavyomsakama Tina hapa lakini iwapo ingefichuliwa bungeni basi ingekuwa ni kama Bomu lililolipuka

Watu wengi hawaelewi kinachoendelea TPA now

Mwakyembe kajitahidi sana kucheza na media na akili za watanzania huku yeye kaficha maovu nyingi nyuma yake

Ila watu wataelewa tu kinachoendelea
 

Mkuu umeongea kama GT. Keep it up!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…