Tina,
Hii si mara yako ya kwanza kushusha tuhuma mzito mzito dhidi ya Mwakyembe na Mapande! Nakumbuka kwenye tuhuma zako za awali zili-include tabia mbaya ya Mapande kuwadhalilisha wanawake pale TPA, pamoja na mambo mengine ikiwa na kuwashika makalio bila ridhaa yao! Leo, umekuja na tuhuma zingine lakini kwa bahati mbaya zako zinakuwa juu juu wakati kati ya yale uliyotaja yangekuwa na uzito endapo yangekuwa yamewekewa nyama. Mathalani, ikiwa una uhakika kwamba Mwakyembe alishinikiza ajira kwa mtoto wa dadake basi bila shaka jina la huyo mtoto utakuwa unalifahamu unless kama na wewe umesikia tu kwa mtu kwamba yule ni mpwa wa Mwakyembe! Tuwekee hilo jina ili wasioona taabu kufuatilia wafanye hivo kwavile hili ni rahisi sana kulipatia ukweli!!!
Halikadhalika, hapa naona unajikanganya ama hueleweki. Unasema: "-
Kuvunja sheria mama ya TPA (Port Act of 2004) kwa kumteua mfanyakazi wa ngazi ya chini bandari ya Mtwara kuwa mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa TPA. Sheria mama hii inatamka wazi kuwa mtu yeyote mwenye maslahi yanayokinzana katika Mamlaka ya TPA asiwe mjumbe wa bodi.- Uteuzi huu umefanyika kwa makusudi, ili mjumbe huyo alinde maslahi ya Mwakyembe kwa nguvu zote, ili na yeye ajihakikishie maslahi yake binafsi kutokana na marupurupu na posho nono za bodi hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa mteule huyo alikimbia umande na hajawahi kukanyaga darasani." Hebu tueleze hoja yako hapo ipo wapi hasa? NI kwamba aliyeteuliwa ni Junior Staff au aliyeteuliwa ana maslahi kinzani na TPA? Which is which?
Aidha unasema: "------ Uteuzi wa wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi TPA kwa urafiki badala ya utaalamu, weledi na uzoefu katika nyanja mbalimbali, hususan sekta ya bandari ili kusimamia kwa umadhubuti taasisi hii muhimu ambayo kwayo nchi hii inaweza kuvuka kutoka kwenye dimbwi la umaskini." Hii nayo ni easily provable subject ikiwa ungitoa ikiwa imejitosheleza! Ni akina nani hao? Kwanini usiweke majina na sifa/qualification zao hapa ili tujiridhishe kwamba kweli wamechomekwa kishikaji? Mathalani, ikiwa mmoja wapo ni NasDaz mwenye Certificate ya Agriculture kutoka Naliendele, hapo kweli watu itabidi wajiulize! Ikiwa umeamua, kwanini unakuja na habari nusu nusu? Kwa staili yako ya uletaji habari haitashangaza hata kidogo watu waki-conclude kwamba ni majungu.
Anyway, mifano ipo mingi lakini thread yako inatoa somo moja tu kubwa kwamba Harrison Mwakyembe yupo on top of the most corrupt people in the country. So, kwanini tuhuma mzito kama hizo usiwe unazipa nyama ya kutosha especially kwa yale maeneo ambayo ni rahisi watu ufuatilia? Unataja kwamba Mwakyembe amekula deal kununua ardhi kwa sh.16 billion ambayo ni ya kigogo mwenzake lakini hutaki kumtaja huyo kigogo na kuishia tu kusema (jina lako tunalo). Sasa wewe kweli lengo lako ni kufichua uovu au ku-deal na Mwakyembe? Sehemu kibao unaishia tu kusema kwa maslahi yake na ....na...na....; hao wengine hutaji; what does it mean? Angalia pia ulivyohitimisha hoja yako kwa kutoa wito kwa serikali:
Wito kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali naMheshimiwa Jaji Kiongozi : Chonde chonde Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu waSerikali na Mheshimiwa Jaji Kiongozi, kwa heshima na taadhima, mnaombwa kwapamoja mfungue macho yenu muone, na masikio msikie ili mfahamu kinagaubaga,migongano na migogoro ya mwanasheria Mwakyembe, aliyebobea katika sheria nakuzivunja kwa hila, ili mchukue hatua za kinidhamu dhidi yake, kwa kuwakadhalilisha taaluma ya sheria.- Haya sio makosa ya kisiasa, bali ni uvunjwajiwa sheria, uliukwaji wa haki za binadamu na udhalilishaji wa taaluma ya sheriaambayo nyie mnaisimia vizuri." Tuhuma ulizotoa ni za ufisadi wa kutisha kiasi cha kuogofya lakini hitimisho lako ni kama unakerwa na Mwakyembe vile anavyobananga sheria na kanuni za uendeshaji; si tena ule ufisadi wa kutisha kwa maana mtu unaposema ardhi ya sh.16 billion kwa mahali kama Kisarawe; mwenye akili timamu anaweza kujiuliza ni ardhi ya namna gani hiyo; au wanataka kununua wilaya mzima? Lakini pamoja na hofu hiyo ya kutsha, unahitimisha kirahisi rahisi tu kwamba AG na Chief Judge wafahamu kinagaubaga, migongano na migogoro ya mwanasheria Mwakyembe, aliyebobea katika sheria na kuzivunja kwa hila, ili mchukue hatua za kinidhamu dhidi yake, kwa kuwa kadhalilisha taaluma ya sheria.- Haya sio makosa ya kisiasa, bali ni uvunjwaji wa sheria, uliukwaji wa haki za binadamu na udhalilishaji wa taaluma ya sheria ambayo nyie mnaisimia vizuri." where's your point really lay?