Mwakyembe: Mwanasheria anayebaka sheria kusudi

Tina

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2007
Posts
572
Reaction score
584
Itakumbwa kwamba mnamo tarehe 23 Agosti 2012, Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi alimteua Madeni Juma Kipande kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimiamizi wa Bandari Tanzania,(TPA).--Uteuzi huu ulifanyika baada ya Mwakyembe kutoa tuhuma zisizothibitishwa--kwamba aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA wakati huo, Ephraim Mgawe alishindwa kuiongoza TPA kwa uadilifu.- Hakuishia hapo, Mwakyembe alivunja Bodi ya Wakurugenzi na kuteua Kamati ya Uchunguzi ambayo -alisema -ingelifanya kazi kwa muda wa wiki mbili, na kuahidi kuwa muda huo ungelitosha kuthibitisha tuhuma zake -dhidi ya Mgawe na manaibu wake ili hatua za kisheria zichukuliwe.- Miongoni mwa tuhuma zilizoelekezwa kwa Mgawe lilikuwepo suala la kutoa ajira kwa upendeleo na kuajiri ndugu, jamaa, marafiki na kadhalika pasipo kufuata taratibu na kanuni za ajira kwenye mashirika ya umma.- Tuhuma nyingine zilihusu kushindwa kusimamia miradi na hivyo kulisababishia taifa hasara.
-
Uvunjaii wa Sheria:Kutokana na tuhuma hizi na nyinginezo dhidi ya Mgawe na wenzake, Mwakyembe aliiamrisha Bodi ya Wakurugenzi wa TPA kuwasimamisha kazi maafisa mbali mbali wa TPA ili kupisha uchunguzi.- Bodi hii ilikuwa chini ya unyekiti wa Raphael Mollel, na ilisheheni wajumbe wenye weledi na wazoefu katika nyanja zao mbali mbali. -Bodi ya wakurugenzi -chini ya Mzee Raphael Mollel ilimuomba Mwakyembe aweke kwa maandishi agizo lake hilo la kuwasimamisha viongozi hao wakuu wa TPA .---Waziri ilibidi kwa shingo upande akubaliane na Bodi na kuweka agizo lake--kwa maandishi kupitia barua iliyotiwa saini na Mwakyembe mwenyewe, huku akitambua -fika kwamba amri na barua kama hiyo, kama kungekuwepo na ulazima au sababu, basi ilibidi barua hiyo itiwe saini na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, lakini yeye aliamua kuvunja sheria na utaratibu halali wa kiutawala kwa ajili ya maslahi yake binafsi, kwa vile udharura wa yeye kuvunja sheria haukuwepo kabisa.- Hii imepelekea Mwakyembe kushitaliwa mahakamani yeye binafsi na mmoja wa maafisa hawa walioachishwa kazi.
-
Wiki mbili ziliisha na Mwakyembe bila aibu wala soni, alikuwa akiongeza muda wa Kamati ya Uchunguzi wiki baada ya nyingine. -Hatimaye -ripoti ya Kamati ya Uchunguzi ilikabidhiwa -mwezi wa Desemba 2012.- Baadaye, wananchi walitangaziwa hatua ya kuwaachisha kazi Mgawe na maafisa wengine, na kama kawaida yake, Mwakyembe aliahidi kuwa kazi zote zitatangazwa ili zishindaniwe na Watanzania wote ili kupata watu wenye uwezo kushika nafasi hizo na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.- Kumbe ahadi hii ilikuwa ni danganya toto tu, Mwakyembe aliendelea kuvunja sheria kwa kumlinda Kipande ili aendelee kukaimu nafasi hiyo, na ajira hizo hazikutangazwa hadi mwezi wa Mei 2013, bila shaka baada ya Mwakyembe kupata shinikizo la kufanya hivyo.
-
Juhudi za kumsimika Kipande kinyemela zilipofanikiwa, Mwakyembe ikawa sasa kachonga mzinga na hivyo akaendelea kulamba asali.- Kati ya Agosti 2012 na Januari 2014, Mwakyembe akiwa kama mwanasheria aliyebobea, amefanya uvunjaji wa sheria tena kwa makusudi, ili kulinda maslahi yake binafsi kwa kiasi kikubwa sana, hasa ikizingatiwa kuwa mambo mengi anayafanya kwa usiri mkubwa kwa kumtumia Kipande, Bodi ya TPA na baadhi ya viongozi wa wafanyakazi wa TPA.- Uvunjaji huu wa sheria, kanuni, taratibu na haki za binadamu umejikita katika maeneo na matukio mengi ikiwemo:
-
(i)------------ Amri ya kuwasimamisha kazi maafisa wa TPA kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa kutoa barua ambayo alitia saini yeye mwenyewe Mwakyembe mwezi Agosti 2012 badala ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, ambavyo ni kinyume cha sheria ya kazi za umma, utawala bora na kanuni na taratibu zilizowekwa na Serikali.
(ii)---------- Uteuzi wa kiini macho wa Madeni Kipande kwa wiki mbili, na kuishia kumkingia kifua hadi leo hii, kwa kuingilia kati, sio tu mchakato wa usaili, bali hata kuivunja bodi ya wakurugenzi, katika kipindi cha mwaka mmoja, aliyoichagua kwa mbwembwe na bashasha zote.- Baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo, baada ya kugundua janja ya Mwakyembe kuwatumia kwa faida yake, wakati wao wakijidhalilisha kwa kuvunja uadilifu wao, waliamua kumwadabisha Kipande kutokana na ukosefu wa nidhamu,n a pia uwezo wake mdogo kiutawala uliosabababisha Kipande kushindwa -kuiongoza taasisi kubwa kama TPA.
(iii)--------- Kuvunja sheria mama ya TPA (Port Act of 2004) kwa kumteua mfanyakazi wa ngazi ya chini bandari ya Mtwara kuwa mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa TPA. Sheria mama hii inatamka wazi kuwa mtu yeyote mwenye maslahi yanayokinzana katika Mamlaka ya TPA asiwe mjumbe wa bodi.- Uteuzi huu umefanyika kwa makusudi, ili mjumbe huyo alinde maslahi ya Mwakyembe kwa nguvu zote, ili na yeye ajihakikishie maslahi yake binafsi kutokana na marupurupu na posho nono za bodi hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa mteule huyo alikimbia umande na hajawahi kukanyaga darasani.
(iv)--------- Uteuzi wa wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi TPA kwa urafiki badala ya utaalamu, weledi na uzoefu katika nyanja mbalimbali, hususan sekta ya bandari ili kusimamia kwa umadhubuti taasisi hii muhimu ambayo kwayo nchi hii inaweza kuvuka kutoka kwenye dimbwi la umaskini.
(v)---------- Kushurutisha ajira za upendeleo kwa ndugu, jamaa, rafiki, familia na ukoo wa Mwakyembe na wenzi wao kadri atakavyo.- Mwakyembe kati ya Agosti 2012 na Januari 2014 ameshinikiza ajira za upendeleo bila kwa mtoto wa dada yake na ndugu zake wengine, ajira za watoto wa vigogo mbalimbali, ajira ya “Mkurugenzi wa Inteligensia” ambayo wala kwenye ikama ya TPA haipo kabisa, na baadae kushinikiza bodi kumwajiri mtu huyo kama Meneja Mipango, wakati hana taaluma yoyote katika maeneo haya.
(vi)--------- Kubuni miradi lukuki kwa maslahi yake binafsi kama ule wa nyumba ya wageni utakaogharimu zaidi ya shilingi 500.0 milioni jimboni kwake Kyela, Matema Beach. Miradi mingine ni kama ule wa kituo cha makasha cha SUKITA kwa kisinginzio cha kutunisha mfuko wa chama tawala, kumbe ni kwa faida yake binafsi na wapambe wake kama Kipande.
(vii)------- Kutoa amri ya kuvunja sheria ya manunuzi -kwa kuilazimisha bodi ya wakurugenzi TPA kutoa maamuzi ya kuiamuru menejimenti ya TPA aidha kuingia ubia na makampuni au watu binafsi bila kutangaza zabuni kama sheria ya manunuzi inavyoainisha, ili kuhakikisha kuwa maslahi yake binafsi yanazingatiwa na yanalindwa na kampuni hizo au na watu hao.- Mradi wa kujenga visima vya mafuta (storage tanks) ambao amedhamiria kuutoa pasipo tenda yoyote kwa kampuni moja ya kiitaliano. Miradi miwili kapania kuitoa kwa kampuni za kibelgiji bila tenda ambayo ni -mfumo wa ukusanyaji taarifa za mizigo (ECTN) ambao wadau waliukataa kwa vile ni wa kiutapeli na hauna faida kwa Taifa.- Kwa kuzingatia sababu hizi mahsusi, SUMATRA waliupiga chini mradi huu wa ECTN, lakini Mwakyembe mnamo mwezi wa Desemba mwaka jana, ameshurutisha Bodi na menejimenti kuutekeleza mradi huu, ambao utamwezesha Mwakyembe na washirika wake kutengeneza faida ya zaidi ya dola za kimarekani milioni mia moja kwa mwaka, kwa kazi hewa.- Mradi mwingine kwa kampuni ya kibelgiji ni wa ujenzi wa gati mbili za makasha hapo Gerezani creek, badala ya kutoa kipaumbele kwa ujenzi wa gati 13 & 14 na wachina.
(viii)------ Kushinikiza ununuzi wa ardhi ya kigogo mwenzake Kisarawe kwa ajili ya mradi wa bandari kavu. -Mwakyembe aliiagiza bodi kuwa TPA iingie kwenye mkataba na kigogo mmoja kutoka Zanzibar (jina tunalo) kwa lengo la kukodisha au kununua eneo/ardhi ya kigogo huyo Kisarawe kwa zaidi ya shilingi 16 bilioni au kuendeleza eneo hilo na kigogo huyo ili kumwezesha Mwakyembe na wenzake kupata mrahaba pasipo jasho. Mwakyembe alitoa agizo hili bila kuzingatia ukweli kuwa Wizara ya Ardhi tayari ilikuwa imeridhia TPA kupatiwa ardhi na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya mradi huu ulioko chini ya Big Result Now. -Wananchi wa Kisarawe wangelipwa fidia na TPA kama sheria inavyoelekeza.- Mwakyembe aliingilia mchakato huu mwezi wa Desemba mwaka jana huko Mtwara, na kuamrisha mazungumzo kati ya Mamlaka na kigogo huyo kuanza mara moja, chini ya usimamizi wa Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu na Idara ya Mipango TPA.
(ix)--------- Kutangaza jina baya la wizi kwa bandari ya DSM kuwa makontena yapapotea kama kiberiti bandarini bila kutilia maanani athari za tamko hili kwa mamlaka.
(x)---------- Kutangaza ongezeko hewa la mapato ya TPA kwa wananchi kwenye vyombo vya habari -kuwa mapato yamefikia wastani wa shilingi 50.0 bilioni kwa mwezi, kiasi ambacho hakijawahi kufikiwa na mamlaka hiyo.
(xi)--------- Kuwapakazia wajumbe wa bodi aliyoivunja kuwa aliwafukuza kwa ajili ya kuigeuza TPA shamba la bibi kwa kulazimisha safari za nje ya nchi kila mara na mikutano ya bodi nje ya ratiba, huku Mwakyembe akifahamu kuwa hii ilikuwa njama yake ya kupindisha ukweli. Inafahamika wazi kuwa safari hizi za ng’ambo na vikao vya bodi nje ya ratiba mara kwa mara, kama ilivyo ada hata leo, Mwakyembe huvitumia kuwarubuni wajumbe wa bodi ili wawe baridi”.- Kafanikiwa kwa bodi hii inayoendelea, -lakini alijaribu mbinu hizi kwa bodi iliyovunjwa bila mafanikio.
(xii)------- Kudanganya umma kuwa ugunduzi wa wizi wa mafuta kutoka bomba la mafuta kwa kutumia puto kubwa aliugundua yeye, kumbe si kweli.- Ukweli ni kwamba wizi huu uliripotiwa na wadau kwenye mahojiano na Kamati ya Uchunguzi aliyoiunda Mwakyembe, dhidi ya viongozi wa TPA mwaka juzi.- Lakini kwa mshangao mkubwa, mwezi wa Septemba mwaka jana, yaani baada ya mwaka mmoja, Mwakyembe aliibuka kama shujaa kwa kuitisha waandishi wa habari na kujigamba kuwa aliibua aina ya wizi huu mpya, kama vile kagundua lulu, kumbe ilikuwa ni uongo. -Ripoti ya Kamati ya Uchunguzi ni ushahidi tosha.
(xiii)------ Kupuuza dhana ya utawala bora, ukweli na uwazi katika uendeshaji wa taasisi hii kubwa, kwa kuwa yeye Mwakyembe amekuwa kama mtendaji mkuu wa TPA kwa kusimamia kazi za kila siku na kufanya kama atakavyo.
(xiv)------ Kutumia rasilimali za TPA vibaya na kwa matashi yake pasipo kufuata sheria na kanuni za fedha za Serikali.- Kwa mfano, Mwakyembe anaamrisha baadhi ya matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kugharamiwa na TPA ikiwemo posho za vikao na safari, takrima, n.k- Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu imetoa mifano hai kwenya ripoti yake ya ukaguzi kuhusu dhahama hii.
(xv)--- Kutumia viongozi wa chama cha wafanyakazi wa TPA kumlinda Kipande kwa kuwapatia viongozi hao marupurupu yasiyo na kifani ili kuwarubuni wakae kimya dhidi ya dhuluma ya wafanyakazi wa TPA aliyoianzisha yeye Mwakyembe kwa tuhuma za kubambikizwa. Hii imesababisha TPA kupata kesi nyingi za ukiukwaji wa haki za binadamu na madai ya compensation.
(xvi)- - Kushinikiza uteuzi wa wafanyakazi wa ngazi za chini kushika nyadhifa za juu za uongozi, pasipo sababu maalumu, ila tu ya kujuana (know who) na sio ya uwezo wa mtu (know how). -Hii imesababisha manung'uniko makubwa miongoni mwa wafanyakazi TPA, ambao waathirika wanajiona kama watoto ya tima, na wale walionufaika kwa kukaimu nafasi hizo za juu, wanawatambia mabosi wao, kwa kusema kuwa kutesa kwa zamu. Wakati mwingine, meneja wa kitengo anawajibika kwa ofisa mwandamizi au hata ofisa tu mdogo, ambaye labda kateuliwa kushika nafasi ya ukurugenzi kwa uswahiba tu.
Wito kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mheshimiwa Jaji Kiongozi : Chonde chonde Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mheshimiwa Jaji Kiongozi, kwa heshima na taadhima, mnaombwa kwa pamoja mfungue macho yenu muone, na masikio msikie ili mfahamu kinagaubaga, migongano na migogoro ya mwanasheria Mwakyembe, aliyebobea katika sheria na kuzivunja kwa hila, ili mchukue hatua za kinidhamu dhidi yake, kwa kuwa kadhalilisha taaluma ya sheria.- Haya sio makosa ya kisiasa, bali ni uvunjwaji wa sheria, uliukwaji wa haki za binadamu na udhalilishaji wa taaluma ya sheria ambayo nyie mnaisimia vizuri.
-
Kama alivyowahi kutamka kwa Waziri Mkuu Mstaafu mmojawapo, na yeye haina budi kupima huu uchafu wake na kujiondoa, au akikataa, basi aondolewe.- Huyu sio Waziri mzigo, bali ni Waziri hatari anaetumia mali ya umma kujitajirisha yeye na ukoo wake na hivyo kutudidimiza sisi walalahoi, tumemchoka.. Ikulu isiishie kumwambia tu uchunguzi huru ufanywe haraka. Kila taasisi zimechoka kuanzia TRA, polisi na wadau anavuruga bandari.
 
Wanafiki na wezi wakubwa nyie. Mwakyembe amewakalia kooni
 
Jibu hoja. . Unafiki ni upi? Jibu hoja kwa hoja sio general statement. ... munatia aibu kwa uvivu wa kifikra. JF ni eneo na fikra pevu na weledi sio porojo na mbwembwe.
 
Tina Aise we jamaa yangu inaonekana tangu akufukuze kibarua huyu waziri huna jema nae hata kidogo maana kila iitwapo leo wewe ni kumsakama tu majungu yasiyokuwa na kichwa wala miguu
Ushauri wangu tu ni kwamba kibarua ndo kimeshaota nyasi kwahiyo shika jembe tukalimee....... acha kuropoka ropoka
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mwakyembe ni mropokaji sana mtu wa kukurupuka, toka aliposhadadia treni ya Dar nilimuona hamnao,

Pia hayo madudu ya TPA na ATC.

Huwa najiuliza hivi amefaya kaazi gani ya kukumbukwa toka awe waziri
 
Aise we jamaa yangu inaonekana tangu akufukuze kibarua huyu waziri huna jema nae hata kidogo maana kila iitwapo leo wewe ni kumsakama tu majungu yasiyokuwa na kichwa wala miguu
Ushauri wangu tu ni kwamba kibarua ndo kimeshaota nyasi kwahiyo shika jembe tukalimee....... acha kuropoka ropoka

Wale wale! Jibu hoja. Bahati mbaya hujui ulisemalo. Sijawahi na siwezi kuajiriwa wala kulishwa maneno kama wanatetea wasiojijua. Kuna hoja chambua na kujibu hoja.
 
mwakyembe kawashika sana, wakati nyie mko ofisini mlikifanya nini cha maana? angalau siku hizi tunasikia kuwa pembe za ndovu zinakamatwa, sio kipindi chenu
 
Fuatilia uone. ... jibuni hoja. Musitetee musichojua Kauli ya Pengo na Dr.Slaa imetimia kwamba wapo wanapiga vita ufisadi ili na wao walipata nafasi wafanye. Mwakyembe huko nyuma amefanya mazuri na hata hapo Bandarini anayo mema but amewapumbaza watu kaaingia ama kaingizwa katika ufisadi.
 
Huwezi jua uchungu wa kufiwa hadi msiba ukufike, naona personal emotion hapa!
 
Fuatilia uone. ... jibuni hoja. Musitetee musichojua Kauli ya Pengo na Dr.Slaa imetimia kwamba wapo wanapiga vita ufisadi ili na wao walipata nafasi wafanye. Mwakyembe huko nyuma amefanya mazuri na hata hapo Bandarini anayo mema but amewapumbaza watu kaaingia ama kaingizwa katika ufisadi.
apa

Mwakyembe chapa kazi, achana na hoja za warasimu wanaopende kuona mambo yanajaa mezani yakisubiri maamuzi.
 
Itakumbwa kwamba mnamo tarehe 23 Agosti 2012, Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi alimteua Madeni Juma Kipande kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimiamizi wa Bandari Tanzania,(TPA).--Uteuzi huu ulifanyika baada ya Mwakyembe kutoa tuhuma zisizothibitishwa--kwamba aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA wakati huo, Ephraim Mgawe alishindwa kuiongoza TPA kwa uadilifu.- Hakuishia hapo, Mwakyembe alivunja Bodi ya Wakurugenzi na kuteua Kamati ya Uchunguzi ambayo -alisema -ingelifanya kazi kwa muda wa wiki mbili, na kuahidi kuwa muda huo ungelitosha kuthibitisha tuhuma zake -dhidi ya Mgawe na manaibu wake ili hatua za kisheria zichukuliwe.- Miongoni mwa tuhuma zilizoelekezwa kwa Mgawe lilikuwepo suala la kutoa ajira kwa upendeleo na kuajiri ndugu, jamaa, marafiki na kadhalika pasipo kufuata taratibu na kanuni za ajira kwenye mashirika ya umma.- Tuhuma nyingine zilihusu kushindwa kusimamia miradi na hivyo kulisababishia taifa hasara.
Tina,
Hii si mara yako ya kwanza kushusha tuhuma mzito mzito dhidi ya Mwakyembe na Mapande! Nakumbuka kwenye tuhuma zako za awali zili-include tabia mbaya ya Mapande kuwadhalilisha wanawake pale TPA, pamoja na mambo mengine ikiwa na kuwashika makalio bila ridhaa yao! Leo, umekuja na tuhuma zingine lakini kwa bahati mbaya zako zinakuwa juu juu wakati kati ya yale uliyotaja yangekuwa na uzito endapo yangekuwa yamewekewa nyama. Mathalani, ikiwa una uhakika kwamba Mwakyembe alishinikiza ajira kwa mtoto wa dadake basi bila shaka jina la huyo mtoto utakuwa unalifahamu unless kama na wewe umesikia tu kwa mtu kwamba yule ni mpwa wa Mwakyembe! Tuwekee hilo jina ili wasioona taabu kufuatilia wafanye hivo kwavile hili ni rahisi sana kulipatia ukweli!!!

Halikadhalika, hapa naona unajikanganya ama hueleweki. Unasema: "- Kuvunja sheria mama ya TPA (Port Act of 2004) kwa kumteua mfanyakazi wa ngazi ya chini bandari ya Mtwara kuwa mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa TPA. Sheria mama hii inatamka wazi kuwa mtu yeyote mwenye maslahi yanayokinzana katika Mamlaka ya TPA asiwe mjumbe wa bodi.- Uteuzi huu umefanyika kwa makusudi, ili mjumbe huyo alinde maslahi ya Mwakyembe kwa nguvu zote, ili na yeye ajihakikishie maslahi yake binafsi kutokana na marupurupu na posho nono za bodi hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa mteule huyo alikimbia umande na hajawahi kukanyaga darasani." Hebu tueleze hoja yako hapo ipo wapi hasa? NI kwamba aliyeteuliwa ni Junior Staff au aliyeteuliwa ana maslahi kinzani na TPA? Which is which?

Aidha unasema: "------ Uteuzi wa wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi TPA kwa urafiki badala ya utaalamu, weledi na uzoefu katika nyanja mbalimbali, hususan sekta ya bandari ili kusimamia kwa umadhubuti taasisi hii muhimu ambayo kwayo nchi hii inaweza kuvuka kutoka kwenye dimbwi la umaskini." Hii nayo ni easily provable subject ikiwa ungitoa ikiwa imejitosheleza! Ni akina nani hao? Kwanini usiweke majina na sifa/qualification zao hapa ili tujiridhishe kwamba kweli wamechomekwa kishikaji? Mathalani, ikiwa mmoja wapo ni NasDaz mwenye Certificate ya Agriculture kutoka Naliendele, hapo kweli watu itabidi wajiulize! Ikiwa umeamua, kwanini unakuja na habari nusu nusu? Kwa staili yako ya uletaji habari haitashangaza hata kidogo watu waki-conclude kwamba ni majungu.

Anyway, mifano ipo mingi lakini thread yako inatoa somo moja tu kubwa kwamba Harrison Mwakyembe yupo on top of the most corrupt people in the country. So, kwanini tuhuma mzito kama hizo usiwe unazipa nyama ya kutosha especially kwa yale maeneo ambayo ni rahisi watu ufuatilia? Unataja kwamba Mwakyembe amekula deal kununua ardhi kwa sh.16 billion ambayo ni ya kigogo mwenzake lakini hutaki kumtaja huyo kigogo na kuishia tu kusema (jina lako tunalo). Sasa wewe kweli lengo lako ni kufichua uovu au ku-deal na Mwakyembe? Sehemu kibao unaishia tu kusema kwa maslahi yake na ....na...na....; hao wengine hutaji; what does it mean? Angalia pia ulivyohitimisha hoja yako kwa kutoa wito kwa serikali: Wito kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali naMheshimiwa Jaji Kiongozi : Chonde chonde Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu waSerikali na Mheshimiwa Jaji Kiongozi, kwa heshima na taadhima, mnaombwa kwapamoja mfungue macho yenu muone, na masikio msikie ili mfahamu kinagaubaga,migongano na migogoro ya mwanasheria Mwakyembe, aliyebobea katika sheria nakuzivunja kwa hila, ili mchukue hatua za kinidhamu dhidi yake, kwa kuwakadhalilisha taaluma ya sheria.- Haya sio makosa ya kisiasa, bali ni uvunjwajiwa sheria, uliukwaji wa haki za binadamu na udhalilishaji wa taaluma ya sheriaambayo nyie mnaisimia vizuri." Tuhuma ulizotoa ni za ufisadi wa kutisha kiasi cha kuogofya lakini hitimisho lako ni kama unakerwa na Mwakyembe vile anavyobananga sheria na kanuni za uendeshaji; si tena ule ufisadi wa kutisha kwa maana mtu unaposema ardhi ya sh.16 billion kwa mahali kama Kisarawe; mwenye akili timamu anaweza kujiuliza ni ardhi ya namna gani hiyo; au wanataka kununua wilaya mzima? Lakini pamoja na hofu hiyo ya kutsha, unahitimisha kirahisi rahisi tu kwamba AG na Chief Judge wafahamu kinagaubaga, migongano na migogoro ya mwanasheria Mwakyembe, aliyebobea katika sheria na kuzivunja kwa hila, ili mchukue hatua za kinidhamu dhidi yake, kwa kuwa kadhalilisha taaluma ya sheria.- Haya sio makosa ya kisiasa, bali ni uvunjwaji wa sheria, uliukwaji wa haki za binadamu na udhalilishaji wa taaluma ya sheria ambayo nyie mnaisimia vizuri." where's your point really lay?

Last edited by a moderator:
Mwakyembe kaonja kifo haogopi mtu tena kwa watu wezi kama nyie awanyoosha tu.
 
Ningepata kujua kama polonium aliyonayo (Mwakyembe) haitamuua kabla ya 2020, ningeanza kampeni za kumfanya rais wa Tanganyika japo kwa miaka 5. Naamini ataitumia nchi kwa hofu ya Mungu hivyo hatapendelea marafiki zake wala kujipendelea yeye mwenyewe.
 
Fuatilia uone. ... jibuni hoja. Musitetee musichojua Kauli ya Pengo na Dr.Slaa imetimia kwamba wapo wanapiga vita ufisadi ili na wao walipata nafasi wafanye. Mwakyembe huko nyuma amefanya mazuri na hata hapo Bandarini anayo mema but amewapumbaza watu kaaingia ama kaingizwa katika ufisadi.
Kwani wewe unajua nii zaidi ya kutuletea mambo ya kuviziana na kutuhumu watu bila kuwa na ushahidi wa kutosha pengine nyie ndiyo miongoni mwa watu ambao mwakyembe kawabana mnapumulia mashine.
 
Dah kweli mkuu ukiangalia kwa umakini hoja zake hazina mashiko!:A S 103:
 
Kwani wewe unajua nii zaidi ya kutuletea mambo ya kuviziana na kutuhumu watu bila kuwa na ushahidi wa kutosha pengine nyie ndiyo miongoni mwa watu ambao mwakyembe kawabana mnapumulia mashine.

duh! Kweli Nyerere alisema Watanzania hodari kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu. Ametumwa.... si mwenzetu, wanapumulia mashine, wamebanwa, wamwache mpambanaji na kadhalika. Mtu mmoja mwenye hoja ndiye namtafutia majibu ya hoja na kwa heshima sio hizi porojo zenu.
 
Porojo urojo! Mwakyembe hammuwez enyi mhimili wa uovu na kishetani!
 
---

"" style="margin: 0px; padding: 0px; font-size: 12px; border: 0px; vertical-align: bottom;">

HomeNewsNational

NATIONAL

Why plan to have Dar port work around the clock has stalled

SHARE-BOOKMARKPRINTEMAILRATING

We doubt if clearing agents, truck owner and ICD operators can fully reap the benefits of the MOU and SOPs in their current state.”PHOTO|FILE-

By-Peter Nyanje The Citizen Reporter

Posted- Monday, January 27- 2014-at- 11:07

IN SUMMARY

The Ministry of Transport asked all port stakeholders to sign the agreement last Wednesday, but some, notably the Tanzania Shipping Agents Association (Tasaa), refused on the grounds that they were not ready to accept half-cooked strategies that would not work effectively.

SHARE THIS STORY

--

-1
inShare

"" style="margin: 0px; padding: 0px; font-size: 12px; border: 0px; vertical-align: bottom;">

Dar es Salaam. Plans to have Dar es Salaam port operate around the clock have suffered a setback after some stakeholders refused to endorse the suggestion, The Citizen has reliably learnt.

The Ministry of Transport asked all port stakeholders to sign the agreement last Wednesday, but some, notably the Tanzania Shipping Agents Association (Tasaa), refused on the grounds that they were not ready to accept half-cooked strategies that would not work effectively.

“We are not against the plan to have the port operate 24 hours. In fact, that is what we have been demanding for many years, but the plan is not good enough,” said Tasaa Executive Secretary Elitunu Mallamia.

Tasaa members argue that the plan drawn by the ministry does not adequately address requirements listed under the government’s Big Results Now (BRN) initiative, which is aimed at speeding up development in a number of key sectors.

“The 24/7 plan was a product of the BRN initiative of which I, on behalf of Tasaa, was a participant. The initiative involved KPIs (key performance indicators) for loading, discharge, clearance and delivery of cargo, among others. The KPIs are indicated in BRN documents.

We at Tasaa were hoping to see them in these documents, but we haven’t,” Mr Mallamia told The Citizen.

He said the two documents made available to them were lopsided and may not achieve the envisaged productivity because it was only private players that were given deadlines, and not government agencies such as the Tanzania Revenue Authority (TRA) and Tanzania Ports Authority (TPA).

“For instance, the standard operating procedures (SOPs) say that shipping agents should submit manifests within 48 hours, failure of which attracts a penalty. But the same document does not say within what time TRA has to approve manifests for us to issue delivery orders,” Mr Mallamia said.

The Citizen could not get a response from the ministry. However, Section 3.2 of the SOPs, which centres on documentation, billing and handling procedures, does not set a time limit for other stakeholders after manifests are submitted by shipping agents.

Mr Mallamia noted further that the SOPs require a notice of a vessel’s arrival to be given, but does not give the maximum number of days ships are required to stay at outer anchorage while TPA goes through shipping lists.

This puts vessel owners, importers and shipping agents at a disadvantage, he added.

“Why, for instance, does it not say within what time the Tanzania Bureau of Standards and Tanzania Food and Drugs Authority are required to issue permits so that clearance can proceed?

If ICDs (inland container depots) are required to remove containers from the port within 72 hours, why is it that other stakeholders are not compelled to complete the discharging of cargo and all necessary procedures within these 72 hours?” he asked.

Mr Mallamia also said the agreement does not address a situation where ICDs were ready to collect containers, but TRA systems were down or terminal equipment was not working.

“It is all stakeholders, including government agencies, that should work 24/7 according to clearly defined performance indicators,” he said.

According to Mr Mallamia, merely stating procedures in the document and requiring stakeholders to sign would not work if all players would not strive to ensure that what had been agreed was implemented.

“We doubt if clearing agents, truck owner and ICD operators can fully reap the benefits of the MOU and SOPs in their current state.”

Why plan to have Dar port work around the clock has stalled - National - thecitizen.co.tz
 
Wadau wa bandari ni wengi na ndio hao wanaoyaona hayo madudu ya mwakyembe na kikundi chake wanavyofanya ufisadi. Watu wengine wanamshabikia mwakyembe pengine hawakumbuki alichowafanyia watanzania kwenye ripoti ya richmond kuwalinda wakubwa. HAFAI KABISA HUYU. Tina endelea kuweka mambo hadharani iko siku wataujua ukweli wa huyu fisadi.
 
Itakumbwa kwamba mnamo tarehe 23 Agosti 2012, Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi alimteua Madeni Juma Kipande kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimiamizi wa Bandari Tanzania,(TPA).--Uteuzi huu ulifanyika baada ya Mwakyembe kutoa tuhuma zisizothibitishwa--kwamba aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA wakati huo, Ephraim Mgawe alishindwa kuiongoza TPA kwa uadilifu.- Hakuishia hapo, Mwakyembe alivunja Bodi ya Wakurugenzi na kuteua Kamati ya Uchunguzi ambayo -alisema -ingelifanya kazi kwa muda wa wiki mbili, na kuahidi kuwa muda huo ungelitosha kuthibitisha tuhuma zake -dhidi ya Mgawe na manaibu wake ili hatua za kisheria zichukuliwe.- Miongoni mwa tuhuma zilizoelekezwa kwa Mgawe lilikuwepo suala la kutoa ajira kwa upendeleo na kuajiri ndugu, jamaa, marafiki na kadhalika pasipo kufuata taratibu na kanuni za ajira kwenye mashirika ya umma.- Tuhuma nyingine zilihusu kushindwa kusimamia miradi na hivyo kulisababishia taifa hasara.
-
Uvunjaii wa Sheria:Kutokana na tuhuma hizi na nyinginezo dhidi ya Mgawe na wenzake, Mwakyembe aliiamrisha Bodi ya Wakurugenzi wa TPA kuwasimamisha kazi maafisa mbali mbali wa TPA ili kupisha uchunguzi.- Bodi hii ilikuwa chini ya unyekiti wa Raphael Mollel, na ilisheheni wajumbe wenye weledi na wazoefu katika nyanja zao mbali mbali. -Bodi ya wakurugenzi -chini ya Mzee Raphael Mollel ilimuomba Mwakyembe aweke kwa maandishi agizo lake hilo la kuwasimamisha viongozi hao wakuu wa TPA .---Waziri ilibidi kwa shingo upande akubaliane na Bodi na kuweka agizo lake--kwa maandishi kupitia barua iliyotiwa saini na Mwakyembe mwenyewe, huku akitambua -fika kwamba amri na barua kama hiyo, kama kungekuwepo na ulazima au sababu, basi ilibidi barua hiyo itiwe saini na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, lakini yeye aliamua kuvunja sheria na utaratibu halali wa kiutawala kwa ajili ya maslahi yake binafsi, kwa vile udharura wa yeye kuvunja sheria haukuwepo kabisa.- Hii imepelekea Mwakyembe kushitaliwa mahakamani yeye binafsi na mmoja wa maafisa hawa walioachishwa kazi.
-
Wiki mbili ziliisha na Mwakyembe bila aibu wala soni, alikuwa akiongeza muda wa Kamati ya Uchunguzi wiki baada ya nyingine. -Hatimaye -ripoti ya Kamati ya Uchunguzi ilikabidhiwa -mwezi wa Desemba 2012.- Baadaye, wananchi walitangaziwa hatua ya kuwaachisha kazi Mgawe na maafisa wengine, na kama kawaida yake, Mwakyembe aliahidi kuwa kazi zote zitatangazwa ili zishindaniwe na Watanzania wote ili kupata watu wenye uwezo kushika nafasi hizo na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.- Kumbe ahadi hii ilikuwa ni danganya toto tu, Mwakyembe aliendelea kuvunja sheria kwa kumlinda Kipande ili aendelee kukaimu nafasi hiyo, na ajira hizo hazikutangazwa hadi mwezi wa Mei 2013, bila shaka baada ya Mwakyembe kupata shinikizo la kufanya hivyo.
-
Juhudi za kumsimika Kipande kinyemela zilipofanikiwa, Mwakyembe ikawa sasa kachonga mzinga na hivyo akaendelea kulamba asali.- Kati ya Agosti 2012 na Januari 2014, Mwakyembe akiwa kama mwanasheria aliyebobea, amefanya uvunjaji wa sheria tena kwa makusudi, ili kulinda maslahi yake binafsi kwa kiasi kikubwa sana, hasa ikizingatiwa kuwa mambo mengi anayafanya kwa usiri mkubwa kwa kumtumia Kipande, Bodi ya TPA na baadhi ya viongozi wa wafanyakazi wa TPA.- Uvunjaji huu wa sheria, kanuni, taratibu na haki za binadamu umejikita katika maeneo na matukio mengi ikiwemo:
-
(i)------------ Amri ya kuwasimamisha kazi maafisa wa TPA kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa kutoa barua ambayo alitia saini yeye mwenyewe Mwakyembe mwezi Agosti 2012 badala ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, ambavyo ni kinyume cha sheria ya kazi za umma, utawala bora na kanuni na taratibu zilizowekwa na Serikali.
(ii)---------- Uteuzi wa kiini macho wa Madeni Kipande kwa wiki mbili, na kuishia kumkingia kifua hadi leo hii, kwa kuingilia kati, sio tu mchakato wa usaili, bali hata kuivunja bodi ya wakurugenzi, katika kipindi cha mwaka mmoja, aliyoichagua kwa mbwembwe na bashasha zote.- Baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo, baada ya kugundua janja ya Mwakyembe kuwatumia kwa faida yake, wakati wao wakijidhalilisha kwa kuvunja uadilifu wao, waliamua kumwadabisha Kipande kutokana na ukosefu wa nidhamu,n a pia uwezo wake mdogo kiutawala uliosabababisha Kipande kushindwa -kuiongoza taasisi kubwa kama TPA.
(iii)--------- Kuvunja sheria mama ya TPA (Port Act of 2004) kwa kumteua mfanyakazi wa ngazi ya chini bandari ya Mtwara kuwa mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa TPA. Sheria mama hii inatamka wazi kuwa mtu yeyote mwenye maslahi yanayokinzana katika Mamlaka ya TPA asiwe mjumbe wa bodi.- Uteuzi huu umefanyika kwa makusudi, ili mjumbe huyo alinde maslahi ya Mwakyembe kwa nguvu zote, ili na yeye ajihakikishie maslahi yake binafsi kutokana na marupurupu na posho nono za bodi hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa mteule huyo alikimbia umande na hajawahi kukanyaga darasani.
(iv)--------- Uteuzi wa wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi TPA kwa urafiki badala ya utaalamu, weledi na uzoefu katika nyanja mbalimbali, hususan sekta ya bandari ili kusimamia kwa umadhubuti taasisi hii muhimu ambayo kwayo nchi hii inaweza kuvuka kutoka kwenye dimbwi la umaskini.
(v)---------- Kushurutisha ajira za upendeleo kwa ndugu, jamaa, rafiki, familia na ukoo wa Mwakyembe na wenzi wao kadri atakavyo.- Mwakyembe kati ya Agosti 2012 na Januari 2014 ameshinikiza ajira za upendeleo bila kwa mtoto wa dada yake na ndugu zake wengine, ajira za watoto wa vigogo mbalimbali, ajira ya “Mkurugenzi wa Inteligensia” ambayo wala kwenye ikama ya TPA haipo kabisa, na baadae kushinikiza bodi kumwajiri mtu huyo kama Meneja Mipango, wakati hana taaluma yoyote katika maeneo haya.
(vi)--------- Kubuni miradi lukuki kwa maslahi yake binafsi kama ule wa nyumba ya wageni utakaogharimu zaidi ya shilingi 500.0 milioni jimboni kwake Kyela, Matema Beach. Miradi mingine ni kama ule wa kituo cha makasha cha SUKITA kwa kisinginzio cha kutunisha mfuko wa chama tawala, kumbe ni kwa faida yake binafsi na wapambe wake kama Kipande.
(vii)------- Kutoa amri ya kuvunja sheria ya manunuzi -kwa kuilazimisha bodi ya wakurugenzi TPA kutoa maamuzi ya kuiamuru menejimenti ya TPA aidha kuingia ubia na makampuni au watu binafsi bila kutangaza zabuni kama sheria ya manunuzi inavyoainisha, ili kuhakikisha kuwa maslahi yake binafsi yanazingatiwa na yanalindwa na kampuni hizo au na watu hao.- Mradi wa kujenga visima vya mafuta (storage tanks) ambao amedhamiria kuutoa pasipo tenda yoyote kwa kampuni moja ya kiitaliano. Miradi miwili kapania kuitoa kwa kampuni za kibelgiji bila tenda ambayo ni -mfumo wa ukusanyaji taarifa za mizigo (ECTN) ambao wadau waliukataa kwa vile ni wa kiutapeli na hauna faida kwa Taifa.- Kwa kuzingatia sababu hizi mahsusi, SUMATRA waliupiga chini mradi huu wa ECTN, lakini Mwakyembe mnamo mwezi wa Desemba mwaka jana, ameshurutisha Bodi na menejimenti kuutekeleza mradi huu, ambao utamwezesha Mwakyembe na washirika wake kutengeneza faida ya zaidi ya dola za kimarekani milioni mia moja kwa mwaka, kwa kazi hewa.- Mradi mwingine kwa kampuni ya kibelgiji ni wa ujenzi wa gati mbili za makasha hapo Gerezani creek, badala ya kutoa kipaumbele kwa ujenzi wa gati 13 & 14 na wachina.
(viii)------ Kushinikiza ununuzi wa ardhi ya kigogo mwenzake Kisarawe kwa ajili ya mradi wa bandari kavu. -Mwakyembe aliiagiza bodi kuwa TPA iingie kwenye mkataba na kigogo mmoja kutoka Zanzibar (jina tunalo) kwa lengo la kukodisha au kununua eneo/ardhi ya kigogo huyo Kisarawe kwa zaidi ya shilingi 16 bilioni au kuendeleza eneo hilo na kigogo huyo ili kumwezesha Mwakyembe na wenzake kupata mrahaba pasipo jasho. Mwakyembe alitoa agizo hili bila kuzingatia ukweli kuwa Wizara ya Ardhi tayari ilikuwa imeridhia TPA kupatiwa ardhi na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya mradi huu ulioko chini ya Big Result Now. -Wananchi wa Kisarawe wangelipwa fidia na TPA kama sheria inavyoelekeza.- Mwakyembe aliingilia mchakato huu mwezi wa Desemba mwaka jana huko Mtwara, na kuamrisha mazungumzo kati ya Mamlaka na kigogo huyo kuanza mara moja, chini ya usimamizi wa Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu na Idara ya Mipango TPA.
(ix)--------- Kutangaza jina baya la wizi kwa bandari ya DSM kuwa makontena yapapotea kama kiberiti bandarini bila kutilia maanani athari za tamko hili kwa mamlaka.
(x)---------- Kutangaza ongezeko hewa la mapato ya TPA kwa wananchi kwenye vyombo vya habari -kuwa mapato yamefikia wastani wa shilingi 50.0 bilioni kwa mwezi, kiasi ambacho hakijawahi kufikiwa na mamlaka hiyo.
(xi)--------- Kuwapakazia wajumbe wa bodi aliyoivunja kuwa aliwafukuza kwa ajili ya kuigeuza TPA shamba la bibi kwa kulazimisha safari za nje ya nchi kila mara na mikutano ya bodi nje ya ratiba, huku Mwakyembe akifahamu kuwa hii ilikuwa njama yake ya kupindisha ukweli. Inafahamika wazi kuwa safari hizi za ng’ambo na vikao vya bodi nje ya ratiba mara kwa mara, kama ilivyo ada hata leo, Mwakyembe huvitumia kuwarubuni wajumbe wa bodi ili wawe baridi”.- Kafanikiwa kwa bodi hii inayoendelea, -lakini alijaribu mbinu hizi kwa bodi iliyovunjwa bila mafanikio.
(xii)------- Kudanganya umma kuwa ugunduzi wa wizi wa mafuta kutoka bomba la mafuta kwa kutumia puto kubwa aliugundua yeye, kumbe si kweli.- Ukweli ni kwamba wizi huu uliripotiwa na wadau kwenye mahojiano na Kamati ya Uchunguzi aliyoiunda Mwakyembe, dhidi ya viongozi wa TPA mwaka juzi.- Lakini kwa mshangao mkubwa, mwezi wa Septemba mwaka jana, yaani baada ya mwaka mmoja, Mwakyembe aliibuka kama shujaa kwa kuitisha waandishi wa habari na kujigamba kuwa aliibua aina ya wizi huu mpya, kama vile kagundua lulu, kumbe ilikuwa ni uongo. -Ripoti ya Kamati ya Uchunguzi ni ushahidi tosha.
(xiii)------ Kupuuza dhana ya utawala bora, ukweli na uwazi katika uendeshaji wa taasisi hii kubwa, kwa kuwa yeye Mwakyembe amekuwa kama mtendaji mkuu wa TPA kwa kusimamia kazi za kila siku na kufanya kama atakavyo.
(xiv)------ Kutumia rasilimali za TPA vibaya na kwa matashi yake pasipo kufuata sheria na kanuni za fedha za Serikali.- Kwa mfano, Mwakyembe anaamrisha baadhi ya matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kugharamiwa na TPA ikiwemo posho za vikao na safari, takrima, n.k- Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu imetoa mifano hai kwenya ripoti yake ya ukaguzi kuhusu dhahama hii.
(xv)--- Kutumia viongozi wa chama cha wafanyakazi wa TPA kumlinda Kipande kwa kuwapatia viongozi hao marupurupu yasiyo na kifani ili kuwarubuni wakae kimya dhidi ya dhuluma ya wafanyakazi wa TPA aliyoianzisha yeye Mwakyembe kwa tuhuma za kubambikizwa. Hii imesababisha TPA kupata kesi nyingi za ukiukwaji wa haki za binadamu na madai ya compensation.
(xvi)- - Kushinikiza uteuzi wa wafanyakazi wa ngazi za chini kushika nyadhifa za juu za uongozi, pasipo sababu maalumu, ila tu ya kujuana (know who) na sio ya uwezo wa mtu (know how). -Hii imesababisha manung'uniko makubwa miongoni mwa wafanyakazi TPA, ambao waathirika wanajiona kama watoto ya tima, na wale walionufaika kwa kukaimu nafasi hizo za juu, wanawatambia mabosi wao, kwa kusema kuwa kutesa kwa zamu. Wakati mwingine, meneja wa kitengo anawajibika kwa ofisa mwandamizi au hata ofisa tu mdogo, ambaye labda kateuliwa kushika nafasi ya ukurugenzi kwa uswahiba tu.
Wito kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mheshimiwa Jaji Kiongozi : Chonde chonde Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mheshimiwa Jaji Kiongozi, kwa heshima na taadhima, mnaombwa kwa pamoja mfungue macho yenu muone, na masikio msikie ili mfahamu kinagaubaga, migongano na migogoro ya mwanasheria Mwakyembe, aliyebobea katika sheria na kuzivunja kwa hila, ili mchukue hatua za kinidhamu dhidi yake, kwa kuwa kadhalilisha taaluma ya sheria.- Haya sio makosa ya kisiasa, bali ni uvunjwaji wa sheria, uliukwaji wa haki za binadamu na udhalilishaji wa taaluma ya sheria ambayo nyie mnaisimia vizuri.
-
Kama alivyowahi kutamka kwa Waziri Mkuu Mstaafu mmojawapo, na yeye haina budi kupima huu uchafu wake na kujiondoa, au akikataa, basi aondolewe.- Huyu sio Waziri mzigo, bali ni Waziri hatari anaetumia mali ya umma kujitajirisha yeye na ukoo wake na hivyo kutudidimiza sisi walalahoi, tumemchoka.. Ikulu isiishie kumwambia tu uchunguzi huru ufanywe haraka. Kila taasisi zimechoka kuanzia TRA, polisi na wadau anavuruga bandari.

Tina, wengi humu jf wana mtindio wa ubongo maskini hawaelewe hoja zako wamejaa ushabiki!!! Nakupongeza kwa uzalendo wako kutokumwonea haya fisadi yoyote hata kama amevaa ngozi ya mwanakondoo.
La kuongezea tu huyu jamaa atupe maelezo kuhusu jamaa yake aliyeshinikiza aajiriwe TPA kama mlinzi na sasa hivi analinda nyumbani kwake na analipwa overtime kibao hakuna wa kubisha!
 
Back
Top Bottom