Mwakyembe: Msigeuze kodi za Watanzania 'shamba la bibi' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe: Msigeuze kodi za Watanzania 'shamba la bibi'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fangfangjt, Apr 28, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Awila Silla, Singida
  NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakiembe, amewataka wakandarasi wanaotengeneza barabara za lami, kuacha mara moja, tabia ya kugeuza kodi za Watanzania kuwa ni shamba la bibi na kwamba vinginevyo, dawa yao iko jikoni .

  Kauli hiyo ya Dk Mwakyembe, inakuja huku kukiwa na miradi mingi ya barabara, inayotekelezwa na wakandarasi hao, ikiwa ama haijakamilika au haijajengwa katika viwango vya ubora vinavyokubalika.

  Naibu waziri alitoa onyo hilo jana, baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Singida- Kateshi, yenye urefu kilometa 65.1, inayojengwa na Kampuni ya Sino Hyadro Cooperation.

  Dk Mwakyembe alielezea kushangazwa kwake juu ya visingizio vinavyotolewa kampuni hiyo, kuhusu kucheleswesha ujenzi wa barabara hiyo, wakati tayari serikali ikiwa imeshatoa Sh40 bilioni.

  Alisema kitendo hicho kinadhihirisha namna baadhi ya wakandarasi, wasivyokuwa na wito au moyo wa dhati, katika kutekeleza miradi wanayokabidhiwa.

  Kwa mujibu wa Naibu waziri, vitendo vya wakandarasi kuchelewesha miradi, ni vya ukiukwaji mkubwa wa masharti ya mikataba na kwamba katu serikali haitaendelea kuvifumbia macho.

  "Muda ukifika tatuwaacha, mbona hapa nchini tuna wasomi ambao kazi zao tumezifanyia tathimini ya kiutendaji katika maeneo mengi na kubaini kuwa kazi zao zinafanyika kwa ufanisi wa juu," alisema Dk Mwakyembe.

  Alisema sasa si wakati wa kuwapuuza tena wakandarasi wa ndani kwa sababu wameonyesha kuwa wanaweza kulisaidia taifa kuokoa gharama za mamilioni ya fedha, zinazopotelea katika mikono ya wakandarasi wasio na mapenzi mema na watanzania.

  Mapema, Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) katika Mkoa wa Singida, Yustaki Kangole, alisema kususuasua kwa mtadu huo kutokana na fungu dogo la fedha na deni sugu la zaidi ya Sh560 milioni.

  Kangole alisema deni hilo linatokana na wakandarasi kufanya kazi na kutolipwa. Mradi huo ulioanza mwaka 2008 unatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu na kwa mujibu wa Kangole, utaufanya Mkoa wa Singida, kuwa miongoni mwa mikoa saba yenye barabara za kiwango cha lami.

  Habari zilisema hadi sasa ni kilometa saba tu zilizokamilika kati ya kilometa 65.1 za barabara hiyo, ambayo muda wa kukamilika kwake umebaikia miezi minne tu.

  Barabara hiyo inayojengwa kwa kodi za wananchi na msaada wa Benki ya Maendeleo (ADB), inatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh51 bilioni itakapokamilika.


  SOURCE: http://www.mwananchi.co.tz/biashara/-/11419-msigeuzi-kodi-za-watanzani-shamba-la-bibi
   
 2. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  dawa iko jikoni inafanya nini?, wape wanywe! Tunataka vitendo tu!, wao wakifanyiwa isivyo wanaishtaki serikali lakini wakifanya ovyo ovyo hawashtakiwi kwa nini?
   
 3. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,748
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  isije ikawa kama kikombe cha babu........
   
Loading...