Mwakyembe bado mpo kwenye utafiti? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe bado mpo kwenye utafiti?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by makanga, Jun 14, 2011.

 1. m

  makanga Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mimi ni miongoni mwa wakazi wa kyela!!!! kwenye uchaguzi mkuu 2005 mgombea ubunge wetu(mwakyembe) alituahidi mambo mengi tu lakini yaliyokuwa yametugusa sisi wakazi wa kyela hadi tukaamua kumpa ushindi mkubwa ni 1.kutujengea kiwanda cha kusindika matunda, 2.kujenga stand kuu ya kisasa 3. kujenga barabara inayoanzia Kikusya- matema.Pamoja na kuwa hakuna hata moja alilotekeleza kati ya hayo matatu, mimi leo naomba mh mbunge wangu kama yupo humu jamvini anieleze alipofikia ktk ujenzi wa hiyo barabra.sababu ni kwamba barabara hiyo ni kiungo muhimu ktk uchumi wa wilaya yetu kwasababu mazao mengi kama mpunga, kokoa, korosho,mawese na matunda hutokea Matema na Ipinda. pia matema ni sehemu nzuri inayovutia watalii wengi wa ndani na nje ya nchi,hivyo kutokana na kero ya hiyo barabara wilaya inakosa mapato. na kero kubwa ni kipindi cha masika kwani barabara hiyo haipitiki na nauli hupanda kufikia hadi 5000.Hivyo kama mwakyembe umo jamvini naomba unijulishe maendeleo ya hiyo barabara kwani kwenye kampeni za uchaguzi ulisema kwamba tayari utafiti kuhusu hiyo barabara umeshafanyika na kama tayari je hiyo barabara imo kwenye bajeti ya 2011/2012? wakazi wa kyela hii kero wote inatuhusu kama ahadi haitekalezeki basi nguvu ya umma itumike!!!!!!!!!! NAWASILISHA!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 2. m

  makanga Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakazi wa kyela naomba sana mchango wenu kwni hiyo barabara inatutesa na ikumbukwe kuwa kyela hatuna barabara yoyote iliyojengwa kwa kiwango cha lami tangia tumepata uhuru (miaka 50), hivyo ni haki nawajibu wetu kudai hiyo bara bara!!!!!! tafakari, chukua hatua!!!!
   
 3. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu , kwa hili mnamuonea Mbunge wenu.
  Hivi unajua barabara za lami zinavyojengwa au mnasikia tu?
  Kwa kulinganisha ahadi za Mkapa kujenga lami toka Mtwara hadi Mwanza ndo inaendelea kutekelezwa karibu miaka 10 baada ya kutoa ahadi.

  Kwa kawaida upembuzi yakinifu huchukua mwaka mmoja.
  Utafutaji wa fedha za mradi mwaka mwingine.
  Tenda na kumpata mjenzi kuchukua mwaka vile vile.

  Kwa uchache unaongelea miaka mitatu kama mambo yamemyookea Mbunge wenu na yuko bennet na Mkuu wa Nchi.
  Ukitegemea sana unaishia kuchanganyikiwa.
  Samahani sana mi si mkazi wa Kyela lakini barabara hiyo naifahamu sana.
   
 4. m

  makanga Member

  #4
  Jun 15, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sio kwamba namhukumu ila yeye mwenyewe alisema kila kitu kimekamilika hivyo bado ujenzi tu.hivyo atueleze kama katika bajeti fedha zimetengwa au tuendelee kumuita ''mr promise''!!!!!!!
   
 5. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  They say"a good politician is the one who promise his/her people about the future,and when the future comes he promise again about the future,...and so it goes",...kwa hiyo nkamu gwangu ungasulumanyiaga-bubali habo mwalafyale,......otherwise tumpe muda kidogo halafu tutaona kama ni kweli ama porojo zao,..........
   
 6. A

  Anold JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Bado upembuzi yakinifu unafanyika, inatarajiwa kuwa upembuzi huo utakamilika mwaka 2014, kazi itaanza rasmi mwaka 2015 mara baada ya uchaguzi mkuu hivyo usifanye kosa kuchagua mwingine, chagua ccm chagua Mwakyembe.
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ni mpaema mno!tena nampongeza kwa ahadi chache ambazo ni rahisi kuzitekeleza.
  Labda kama alikuambia mwaka wa fedha 2011/12 kuwa atajenga ndo umlaumu ila kumbuka ubunge wake ni wa miaka 5.
  Kyela ni kwetu tena maeneo ya talatala ila bado haujafika wakati wa kumlaumu mda bado anao na nadhani atatusaidia katika hayo ni msikivu pia
  Budget ya wizara yake bado kusomwa you never know labda imo umo
   
 8. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Lakn anatakiwa aende akatoe taarifa ya kile kinachoendelea kuhusu hiyo ahadi aliyoisema,......still wanna be a player
   
 9. m

  makanga Member

  #9
  Jun 15, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hatudanganyiki tena!!mwambie huyo mbunge akamuulize mwakipesile kilichomtokea, naye alipendwa sana ila aliondoka kama mbwa! bado yeye!! mwaka 2015 jimbo linaenda chadema!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 10. m

  makanga Member

  #10
  Jun 15, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kamanda umenena,kwa sababu waajiri wake ni sisi (wananchi wa kyela) hivyo kauweka sisi kama vilaza!!! mwakyembe............ tafakari...........chukua hatua!
   
Loading...