Mwakyembe awabeza wanaomkosoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe awabeza wanaomkosoa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Informer, Oct 5, 2012.

 1. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,224
  Likes Received: 2,438
  Trophy Points: 280
  Na Mariam Mziwanda | Majira | Oktoba 05, 2012

  WAZIRI wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, amewabeza watu wanaokosoa juhudi anazozichukua ili kuboresha miradi na taasisi za Wizara yake akidai watu hao wataendelea kuimba ngonjera kutokana na elimu yao duni ya darasa la saba.

  Alisema Wizara hiyo itaendelea kuongeza ufanisi wa kazi za maendeleo nchini na hakuna mradi usiotekelezeka kimkataba.

  Dkt. Mwakyembe aliyasema hayo Dar es Salaam jana baada ya kumalizika Mkutano wa Pili wa Nchi za Afrika, ambao unajadili mfumo na utaratibu wa vifaa vya uhakika vinavyosababisha uwepo wa bidhaa bora kwa mlaji.

  “Mimi kwa elimu niliyonayo siwezi kubishana na wasio na elimu ambao kila kukicha wanaangalia nimefanya kitu gani cha mandeleo ili wapotoshe ukweli, nitaendelea kufanya kazi na kuwaacha waendelee kutumia elimu zao za darasa la saba kutunga ngonjera.

  “Watu wanaobeza maendeleo waelewe chini ya Wizara yangu hakuna mradi usiotekelezeka kimkataba ili kuondoa utendaji ambao ulizoeleka, mikataba itambana kila mmoja kukamilisha mradi kwa wakati,” alisema Dkt. Mwakyembe.

  Kutokana na hali hiyo, alisema Wizara hiyo ililazimika kufanya ziara katika Mamlaka ya Bandari nchini ili kujua kilichokwamisha mradi wa boya la mafuta kwa wakati hali ambayo imezaa matunda ambapo mradi huo utaanza kazi Novemba mwaka huu.

  Alisema kukamilika kwa boya hilo, kutashusha bei ya mafuta na kudhibiti mfumuko wa bei nchini kutokana na ongezeko la kasi ya upakuaji na ushushaji mafuta bandari.

  Aliongeza kuwa, meli ya kwanza itashusha tani 150 na kufungua njia ya kushusha na kupakia meli nne kwa mwezi hivyo kuondoa msongamano unaojitokeza mara kwa mara.

  Akizungumzia mikakati ya Serikali kupitia mkutano huo, Dkt. Mwakyembe alisema Tanzania imejipanga kuboresha huduma za reli hivyo ndani ya miezi sita ijayo, nchi za Afrika na Watanzania watarajie huduma bora za uhakika ili kuboresha uzalishaji.

  “Mikakati hii ya Serikali inakwenda sambambana na njia zaidi za uboreshaji ugavi katika mazao ya chakula ili kukabiliana na tatizo la njaa na hatimaye kuwa na chakula cha kutosha,” alisema.

  Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji nchini Bw. Zacharia Mganilwa, alisema lengo la mkutano huo ambao Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji ni kupata uzoefu wa kiutafiti ili kukabiliana na maafa ya vifaa vya uzalishaji.

  Alisema kupitia mkutano huo ambao umeshirikisha wawakilishi kutoka nchi za Ujerumani, Japan, Ufaransa, Marekani na Uingireza nchi za Afrika, waatabaini namna ya kuwafikia wahanga katika huduma bora za bidhaa.

  *****
  My Take:

  Mkuu Mtanzania, tupo chini ya miguu yako; 2015 kamng'oe huyu jamaa huko Kyela. Amezidi dharau
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Wala hajakosea lolote!!!!
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Tuko pamoja. Bora Mwakyembe anaonyesha njia kwa vitendo. Wengine wanasema sema tu toka asubuhi mpaka wakati wa kulala.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Kama katika serikali ya thithimwewe wangekuwepo watu wa namna hii watatu, wala kambi ya upinzani Tz isingekuwepo!!!!
   
 5. m

  malaka JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Go mwaki.
   
 6. S

  SILVANUS NJENGA Senior Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 174
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  jamaa ameishaonesha matumaini ya kuwa anaweza kwa hiyo tuzidi kumuombea ili tuone kama taifa letu litapita hatua walau kwa miradi na sekta mbalimbali inayosimamiwa na wizara yake. BE BLESSED dk. MWAKYEMBE.
   
 7. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Anaweza nini huyu jamaaaa?
   
 8. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Aende wapk ndo ashafika huyo
   
 9. b

  bdo JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Nani hao "wenye elimu ya darasa la saba", au ni msamiati mpya kwa yeyote yule anayepinga?
  nimependa: hakifanyiki kitu bila mkataba....tusubiri
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Elimu Vs kukosolewa = kuna uhusiano gani? watanzania kwa majivuno ya Elimu?
   
 11. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Matamshi yake hayafahi kabisa kutamkwa na kiongozi wa umma! Kama ametamka hayo maneno ni jukumu la aliyemteua kumwajibisha. Usipende kusifia kauli za watawala wapenda sifa,jeuri na jazba!
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mwakyembe hajapona arudishwe India
   
 13. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Tuacheni siasa!
  Huyu jamaa ni kiongozi mzuri hata kama yupo kwenye Chama chenye watu wenye mikashfa ya kutisha!
   
 14. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Nasikia staff wengi wa TPA ni darasa la saba na kidato cha nne na ndio wanaongoza kwa majungu na magenge kwa vile walizoea kula kwa miguu na mikono.....sasa jamaa kawapiga na nyundo..............ni kauli mbaya lakini inawafaa sama wapiga majungu wa bandari
   
 15. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Mwakyembe ni mtu wa hovyo kuliko mnavyoweza kufikiria, kwanza anahusika na ufisadi wa umeme wa upepo Huko singida kijiji cha kisasida na walichukua fedha za mkorea kiasi cha dola millions 1.3 na wakamzunguka na Kwenda kusaini mikataba mingine na mwekezaji kutoka CHina kupitia NDC na sasa huenda akafikishwa mahakamani kwani mkorea amekaa mbogo. Na aliwaandikia kuwa kuanzia tarehe tano mwezi Huu atachukua hatua za kisheria.

  Pili kuna kitu cha kijinga sana anafanya kwa sasa kwenye wizara yake na anatengeneza kipindi maalum cha tv kuhusu mafanikio yake tangu awe waziri na anahojiwa yeye na naibu wake ila wameandaa maswali ya kuulizwa na kuyatuma kwa mwendesha kipindi eti awaulize na wao wayajibu. Wizarani kuna hasira sana kuhusiana na jambo Hilo kwani zitatumika zaidi ya millions 300 kwa ajili ya programme hiyo kwenye kununua air time tv Zote Huu ni ufisadi , subirini italipuka soon. Mengine nayaacha kwa sasa.
   
 16. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Informer Hapo mkuu Mhe Mwakyembe kasema ukweli, hao ndio mawaziri waliobaki CCM ni kama jahazi linalozama mabaharia waaminifu wanakazana kuchota maji na kuokoa wengine wanakazana kuzoa mali za kujiokoa nazo!!!! Maana yake CCM kuzama ni lazima wakina Mwakyembe pamoja na kupenda Chama chao cha CCM lakini hakuna jinsi kinazama atafute pa kutokea!!!

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Mkuu, mtazamo wako uko kwenye kumaintain "status Quo" wa kwangu ni "disturbing the equilibrium" unadhani kuna wakati tunaweza kuwa pamoja hata siku moja? Anapenda sifa Kivipi? Mnapenda kila wakati msifiwe tu na uozo wenu usisemwe?
   
 18. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  anapenda sana chokochoko kupitia media.. nilishangaa sana kuona wezi wamekamatwa bandarini halafu yeye mbio kwenda kuita wanahabari na kuelezea katukio as if yeye ndiye aliyewakamata wale wezi kwa mikono yake au PR wa bandari, ndio kwanzaa ana miezi 4 ofisini sasa majigambo yote ya nini? tusibiri umalize mwaka tuanze kujudge matokeo na si michakato
   
Loading...