Mwakyembe atimua wengine 4 TPA

Mwakyembe atimua wengine 4 TPA

Sabato masalia

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2011
Posts
228
Reaction score
134
BAADA ya kuwasimamisha kwa miezi kadhaa kupisha uchunguzi waziri wa uchukuzi Dakta Mwakyembe tangu ijumaa tarehe 24/5/2013 amewatimua kazi wakurugenzi wengine 3 na meneja 1 wa mamlaka ya bandari waliotimuliwa ni Bi Florence Nkya mkurugenzi mipango, Bi Maimuna Mrisha mkurugenzi mawasiliano, Injinia Bakari Kilo mkurugenzi ufundi na Edmund Swai meneja wa ujenzi.

hapo namba imekamilika kwani tayari alishawatimu wakurugenzi Efraim Mgawe,Ahmad Koshuma,Juliasi Mfuko na Kamti. kwa wakurugenzi wa zamani kabaki mpika majungu mkubwa nae anatakiwa kusambaratishwa pia ni mkurugenzi wa masoko mama Fransiska Kajumulo Muhindi[mdogo wake waziri mama Anna Tibaijuka]. Fransiska nae pia ameomba nafasi ya DG majuzi zilipotangazwa ni kituko kweli kweli. yuko likizo marekani.
 
Safi sana Mwakyembe hii itaisaidia serikali kuto tegemea kodi kwenye sigara na pombe.
 
Safi sana Mwakyembe hii itaisaidia serikali kuto tegemea kodi kwenye sigara na pombe.

I hope anafanyia kazi ripoti sahihi na siyo kuwaonea watu wasio na hatia.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Bravoooo mwakyembe tunataka bandari iendeshe nchi si kila kukicha misaada! Tuko pamoja japo kuna wanafiki kwa njaa na uchu wa madaraka kwa mabwana zao wanajaribu kukupaka matope, kudadeki zao
 
Mwakyembe ni jembe la kwenye mawe. Kama mmeona impact yake kwa mizigo ya R1 pale K/koo baada ya kukwepa kodi kwa miaka 6 sasa kanasa kamba.

Tunahitaji watu wanofanya vitu kwa makini na utafiti. Naamini hajakurupuka.
 
Msaidie boss wako labda ataacha kuzurura kuomba omba wakati bandari pekee inaweza endesha nchi
 
Safi sana dokta kila fisadi timua tu,hamna nani wala nani
 
Jamaa kipofu anadhurura kuombaomba na bakuli akifika nyumbani anamimina ktk kapu lililotoboka wenye macho na wa nyumbani mwake wanaendelea kumla kisogo.tutafika tuu

TANZANIA BILA KUNG'OANA MENO TUTAFIKA??
 
Maoni yangu kwa Mwakyembe, pamoja na mauchunguzi yote yanayoendelea, fanya haya: TPA pamoja na TRL fanya recruitment upya! Kila mtu aombe ajira na utoe kwa masharti mapya ya kazi. Na hili liambatane na 'Performace agreement' kwamba kila mtu, kuanzia DG hadi secretary apewe target.

Kuna uozo mwingi sana TPA na TRL. Ukienda kwenye ofisi za TRL watu wako busy na mambo yao, hawataki kabisa kujishughulisha. Na ukiangalia kwa makini utagundua huyo mtu hana pressure - hana target anayotakiwa kufikia kwa hiyo apige domo au ale chapati yote sawa tu.

Ajiri upya- na weka masharti mapya.
 
Hii habari mpya au ya kale?
If yes mpya ALL THE BEST ILA UYO MUHINDI NAE SI TIMUA HUWEZI WEKA MVINYO MPYA KWENYE CHUPA YA ZAMANI
 
Mwakyembe, kila la kheri kurudisha uadilifu na uwajibikaji.
 
Njia Bora ni kuajiri waliofanya sekta binafsi na kuwapa power...kuwarudisha watu wa mfumo ni kupoteza muda...wataendela kufukuzwa kila leo
 
Maoni yangu kwa Mwakyembe, pamoja na mauchunguzi yote yanayoendelea, fanya haya: TPA pamoja na TRL fanya recruitment upya! Kila mtu aombe ajira na utoe kwa masharti mapya ya kazi. Na hili liambatane na 'Performace agreement' kwamba kila mtu, kuanzia DG hadi secretary apewe target.

Kuna uozo mwingi sana TPA na TRL. Ukienda kwenye ofisi za TRL watu wako busy na mambo yao, hawataki kabisa kujishughulisha. Na ukiangalia kwa makini utagundua huyo mtu hana pressure - hana target anayotakiwa kufikia kwa hiyo apige domo au ale chapati yote sawa tu.

Ajiri upya- na weka masharti mapya.
Naunga mkono hoja hii. management ya TRL haina uwezo wa kwenda na kasi tuitakayo, ikizingatiwa kwamba management hii ndiyo iliyofilisi TRC na kulazimika kuibinafsisha kwa wahindi feki.
 
kazi ipo,bt ukwel ni kwamba ubabaishaji ni mwingi,ufanis wa bandari hauwez kupatikana kama taasis shirikish km tra,tfda,tbs,tiss etc zikiwa zimelala.Tpa ni mtu wa mwisho baada ya mamlaka kumaliza majukumu yao,tatizo linakuja uozo wa mamlaka nyingine simply kwa kutokuelewa tu mtu analaumu tpa.

Na hli ni tatizo hta kwa mwakyembe maana anatoa maagizo tu kwa tpa kufanya yasio wahusu matokeo yake watu wanamshangaa tu na kumuona kama vile hana nia nzuri kama anavojipambua.

Kiukweli,bandari inamapungufu yake kma taasisi zingine za uma kwa kuwa watu wake ni watz wa kawaida wenye hulka kama sisi.sasa il tuitumie vizur bandar tusafishe mamlaka zingine kwanza hasa tra mdau mkuu.tpa inafanya vizur bt sio kwa kiwango wanachopanswa so hii expectation gap itajazwa pale ambapo wadau wote hasa serikal itamuunga mkono mwakyembe il taasis zingine zifanye angalau hta kwa 70%.

Mungu ibarik tz ibarik afrika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom