Mwakyembe atafuta "mchawi" JNIA

Mwakyembe atafuta "mchawi" JNIA

ACCOUNT FULL

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Posts
1,995
Reaction score
389
HATMA ya maofisa wanaoruhusu kupitishwa dawa za kulevya katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), imewadia kufuatia Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, kuwaweka kitimoto viongozi wa idara nne watoe taarifa ni kwa nini uwanja huo umekuwa uchochoro wa kupitisha dawa hizo.
Pia ametaka maofisa hao kutoka idara ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa kutaja majina ya watumishi wanaohusika kula njama na wasafirishaji wa dawa za kulevya kupitia uwanja huo ili aweze kuwachukulia hatua.
"Bado naendelea na vikao, kifupi nimetaka maofisa wa TAA, Anga, Polisi na Usalama wa Taifa wanipe taarifa haraka ni kwa nini uwanja wa JNIA umekuwa uchochoro wa kupitisha dawa za kulevya", alisema Dk Mwakyembe.

Aliongeza "nataka wataje wahusika wa biashara ya dawa za kulevya, nani aliacha mwanya hadi watu hao wakapita na dawa hizo, baada ya hapo ntachukua hatua",
Kabla ya kuwaweka kitimoto maofisa wa idara hizo, Dr Mwakyembe alifika katika uwanja wa JNIA kuzindua Kamati mpya ya Taifa ya Usalama wa Anga.
Source;NIPASHE
 
mtoto wa rais ndiye kinara hapo unafikiri rais au waziri atakuwa na maamuzi
 
Hili kombolera halitakaa lipate mzingaji, kama mpaka leo hii wanatafuta wakumfunga paka kengele.
 
watamtoa uwazili,ajui ni wa mwenye mbwa,

Hii hali ya kuwaona kuwa wao ni watu wakubwa ndo imetufikisha hapa,hata kama ni wakubwa sijui wazito kama tukiamua tunaweza kama si kimaliza tatizo kabisa basi hata kulipunguza. Maaana hii sasa ni aibu.
 
Back
Top Bottom