Mwakosya atajwa kesi nyingine ya EPA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakosya atajwa kesi nyingine ya EPA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Oct 9, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  Friday, 09 October 2009
  Na Grace Michael


  SHAHIDI wa tano wa upande wa Mashitaka ambaye ni Mkurugenzi wa Benki Kuu Bw. Emmanuel Boaz ameieleza mahakama kuwa dokezo la kuomba idhini ya malipo ya Kampuni ya Changanyikeni Residential Complex kwa Gavana liliandikwa na Mkurugenzi wa Idara ya madeni Bw. Imani Mwakosya ambaye naye kwa sasa anakabiliwa na kesi nyingine za wizi.

  Hayo aliyasemwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati Boaz akitoa ushahidi kuhusiana na wizi katika akaunti ya madeni ya nje (EPA) uliofanywa na washitakiwa hao mbele ya jopo la Mahakimu, Bi. Sekela Moshi, Sam Rumanyika na Bw. Lameck Mlacha.

  Bw. Boaz alisema kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Changanyikeni aliandika barua BoT akiomba kununua deni kwa Kampuni ya Marubeni Corporation la dola za kimarekani 1,069,125 na dola zingine 501,210.02.

  Baada ya kuandikwa kwa barua hiyo, Bw. Mwakosya aliandika dokezo kwenda kwa Gavana wa BoT akiomba kibali cha kununuliwa deni hilo na Kampuni hiyo na Gavana, Daud Balali akaridhia malipo ya sh. 1,186,534,759.

  Baada ya kupata idhini hiyo, mchakato wa kulipwa fedha hizo uliendelea kufanywa na BoT hatimaye fedha hizo kuingizwa katika akaunti namba 01j013377401 katika Benki ya CRDB Tawi la Kijitonyama, Dar es Salaam na wahusika kujulishwa kwa hatua hiyo.

  Washitakiwa katika kesi hiyo ni Bw.Bahati Mahenge, Bw. Manase Mwakale, Bi. Eda Mwakale, Bw. Davis Kamungu na Bw. Godfry Mosha ambao wanakabiliwa na makosa ya wizi wa fedha hizo.
   
Loading...