Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,675
Akiongea ktk kipindi cha "Clouds 360" Dr JJ Mwaka wa Foreplanre Herbar Clinic amesema ugeni wa Dr Hamis Kigwangala ktk wizara ya Afya na kutokujua sheria za Tiba Asili ndio vilivyosababisha afungie kituo chake kimakosa.
Dr JJ Mwaka anasema sheria ya Tiba Mbadala inaruhusu yeye kujitangaza ktk vyombo vya habari na kunadi huduma yake,kitu ambacho Waziri Kigwangala kwa kutokujua sheria au kwa ugeni wake ktk wizara aliutangazia umma kupitia vyombo vya habari kuwa Dr Mwaka anavunja sheria kwa kujitangaza.
Kuhusu elimu yake,Dr JJ Mwaka anasema amesomea "course" ya Utabibu Asili nchini Australia na Uchina,na anasema yeye ni mmoja kati ya waganga wa tiba asili wachache walioamua kujiendeleza,hivyo anastahili kupongezwa,na sio kubezwa kama ambavyo Naibu Waziri alivyokuwa anambeza kuwa hana hata elimu ya "udaktari" na bado anajiita "Daktari".
Dr JJ Mwaka "Mimi sijasomea udaktari wa kisasa,na wala sina shida nao,mimi ni tabibu wa tiba asili,nimejiendeleza kwenye elimu ya uganga wa tiba asili nchini Australia kwa mwaka mmoja na baadae nchini China,na vyeti vyangu vipo na hata kwenye mitandano ya kijamii vilirushwa".
Dr JJ Mwaka anasema watendaji wa Wizara waliombatana na Naibu Waziri ndio waliompotosha sbb ya ugeni wake ktk wizara kiasi cha kufanya mambo ambayo yamemtia aibu.
Anasema Madaktari wa tiba ya kisasa wana-discourage madawa ya tiba asili kwa kasumba tu ya kuendeleza madawa ya kisasa na kuendeleza soko la biashara kwa viwanda vya nje.
Dr anasema kituo chake kipo kisheria na hakuna mahali alipovunja sheria inayosimamia tiba mbadala,kwamba kituo chake kipo wazi na kinaendelea kutoa huduma kama kawaida.