Mwaka Kikaka Hupanda Shamba na Taka

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
Naam,

viongozi wetu bado hawajaanza kazi. wanaona kwamba ndiyo kwanza wamechaguliwa, wanahisi wanahitaji kupumzika kidogo. Matatizo yetu hayawasubiri wapumzike, yanaendelea kukua na mapya yanajitokeza.

Hamadi! Uchaguzi Mkuu huu hapa. Kwa pupa wataanza kupanda shamba na taka! Wananchi watakubali tena?

La! Siku hizi wananchi wanajua kuwajibisha serikali papo kwa papo. Wananchi wakihisi hawasikilizwi wanalianzisha na kufunga barabara. Wangelalamika kwa kufuata taratibu za kawaida wasingesikilizwa, wangepuuzwa kwa sababu viongozi wako bize, na serikali haina fedha!

Wangeomba kibali cha polisi kuandamana kwa amani wangenyimwa kwa hofu ya uvunjivu wa amani. Lakini wakilianzisha bila kibali, polisi waja tele kuwalinda, wahusika hujitokeza ghafula kutoa maelezo na kero yao hufanyiwa kazi papo kwa papo!

Dalili ya mvua ni mawingu. Serikali haiwajibiki ngazi zote. Wananchi wamepigika kutokana na kuporomoka thamani ya shilingi. mishahara haitoshi kugaramia maisha kwa siku saba. kilimo ndo kwanza mwisho. Giza nchi nzima. Maji hadimu mijini na vijijini. ukiugua unaanza kuandika wosia kabla ya kukimbilia hospitali. wanetu wakimaliza vyuo vikuu hawawezi hata kuandika barua ya kuomba kazi.......endeleza.

Rushwa, rushwa. Polisi, mahakama, hospitali, ardhi, serikali za mitaa, ........

Sawa nchi yetu masikini, hilo halina mjadala. lakini vipi maskini kushindana kununua mashangingi modeli mpya? Nyumba za kifahari? Safari na starehe? Wizi na ufujaji wa pesa na mali za umma?

Katiba baba, katiba. Tume. Sheria ya Uhuru wa habari na upatikanaji wa taarifa. Mchakato uanze sasa hivi, mwaka kikaka hupanda shamba na taka!
 

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
Wananchi huko Tabata leo walifunga barabara kutokana na kutosikilizwa kero yao ya mkondo wa maji ambapo maji yalijaa majumbani mwao. Polisi walitoa ulinzi, na Tanroads waliwasili mara moja na kuahidi kulifanyia kazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom