Mwaka huu mlimani imetoa graduates tegemezi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwaka huu mlimani imetoa graduates tegemezi.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by HAMY-D, Oct 26, 2011.

 1. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Nilikua nayatazama maafari ya chuo kikuu dsm,mara nikasikia wahitimu wanahojiwa na mtangazaji kuhusu hisia za muhitimu katika maafari hayo,cha kushangaza akakimbilia kusema nanukuu "yani nimefurahi sana maana nina cheti cha chuo kikongwe nitaweza kuombea kazi sehemu yeyote".

  Hivi ndio hawa wahitimu chuo cha udsm miaka hiyo ilikua ikiwatoa? Maana kama ndio basi bora lile eneo lote la mlimani walifanye kivutio cha histora na wasitishe kutoa elimu.Kama sio sasa wahitimu wa namna hii wanatokea wapi? Huwezi kukurupukia mambo ya kuajiriwa katika maafari kama yale au inaashilia wamepewa elimu ya kuajiriwa tu? YOU NEED TO BE A JOB CREATOR AND NOT A JOB SEEKER.
   
 2. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  ulimi ulimteleza.
   
 3. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Mbona unafanya generalization kizembe hivyo? Jipange mkuu.
   
 4. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  sio swala la kujipanga mambo ndio yalivyo,kama huamini subiri uone idadi kubwa ya vibahasha vya kaki maofisini vikiletwa na wahitimu.
   
 5. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  kwa hiyo wahitimu kupeleka bahasha za kaki maofisin kwako ni tatizo? Kujadili matokeo kamwe hakuwezi kutusaidia.
   
 6. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  ni mwaka gani haikutoa wahitimu tegemezi.
   
 7. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,999
  Likes Received: 2,654
  Trophy Points: 280
  Uko sawa 100% watu wengi wanasoma ili wapate vyeti na si elimu,ndio maana huku mitaani kumekuwa na msongamano wa majobless wengi,wanazunguka tu na vyeti mchana kutwa wakitafuta kazi,hawana fikra za kujinasua walipo kwa kuitumia elimu walioisotea miaka kadhaa,hawa watu ni janga la kitaifa.
   
 8. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Kuajiriwa ni utumwa, yeyote anayesoma ili akaajiriwe huyo ni limbukeni.
   
 9. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  mda tuliobaki nao watanzania ni mdogo mno na haututoshi kuendelea kulaumu serikali chini ya wizara ya kazi juu ya utendaji wake wa kivivu na usio na nia mathubuti katika kupunguza janga hili la uhaba wa ajira,Ni jukumu letu wasomi kuandaa mipango ya kujikomboa kwa kutumia elimu tuliyoipata hata kwa kuanzisha miradi midogo midogo mijini na hata vijijini,kwa namna hii hizi kelele za ajira zitapungua kwa kiasi fulani.Kuna baadhi yetu hatuamini katika ujasiliamali lakini inawezekana.
   
 10. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,369
  Trophy Points: 280
  Endeleeni kupoteza muda wenu katika kukiponda chuo cha udsm.
   
 11. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  acha kuwa mjinga wewe,kwani udsm ni mali ya wanafunzi au hao unaowaona hapo wanaowapa supplementary? Hicho ni chuo cha walipa kodi nikimaanisha cha jamii,wewe mwonyewe jifanye umelizika na hiyo mitaala ya kizamani mnayo fundishiwa hapo,mimi nna wadogo zangu waliofanya mistake ya kukiweka cha kwanza na wamepelekwa ila wanajuta sasa.

  Rai yangu ni kwamba watu binafsi waanzishe vyuo kwa wingi ili walikomboe taifa kwa kuzalisha wahitimu wabishi wasiojua hata taaluma zao zinawataka wafanye nini.WHEN COMES TO EDUCATION BE WILLING TO PAY ANY COST TO GET IT WELL.
   
 12. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,369
  Trophy Points: 280
  mjinga ni wewe ambaye unafikiri bado tunatumia mtaala wa zamani, mwaka huu umetolewa mtaala mpya katika kila sector, na upo tofauti kabisa na mitaala ya awali.... Tafadhali ukiwa unasema kitu,inabidi uwe na uhakika.

  Halafu nani amekuuliza kama ni chuo cha wananchi? Nadhani hukujua kwanini nilisema vile.
  hapa ndio nimeona umeongea la maana.
   
 13. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  ukweli huu ndio uliotuzunguka japo unauma!
   
 14. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Well said,UDSM ya kugawa PHD hata kwa vilaza,haitatufikisha popote,miaka 50 chuo hakina hata kakiwanda kadogo ka uzalishaji kama sehemu ya mafunzo,aibu ni matokeo ya Ma VC siasa wanatumia mda mwingi kujipendekeza kwa waliowaweka kuliko kuangalia mambo ya kitaaluma na kitaalamu

   
 15. Engager

  Engager JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hivi ni chuo cha udsm au ni udsm?

  Note: udsm- university of Dar es salan,
   
 16. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,369
  Trophy Points: 280
  whateva.. Najua ukishasema 'UDSM' unakuwa ume-include neno 'chuo'
   
Loading...