HERI YA MWAKA MPYA 2017 WAPENDWA.
Leo nitazungumza na vijana wenzangu hasa wa CCM ambao Mara nyingi wamekuwa wakitushambulia tunapo mkosoa Dr Maghufuli
Sikilizeni vijana wa CCM niwaeleze, tunapomkosoa Maghufuli, hatufanyi hivyo kwa sababu ya Uenyekiti wake wa CCM. Sisi kama taifa uenyekiti wake wa CCM hautusaidii na nadhani kama mngekuwa makini zaidi hata hii nafasi ya uenyekiti msingempa, mgekuwa na uwezo wa kumsoa. Sasa ni hivi tunamkosoa kwa sababu Maghufuli kwa sababu ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, tunamkosoa kwa sababu ndie anakusanya kodi zetu kupitia TRA, tunamkosoa Maghufuli kwa sababu ndiye aliyepata nafasi ya kutekeleza ahadi zake, tunamkosoa Maghufuli kwa sababu ndiye anayeishi kwa hisani ya kodi zetu.
Sasa msivimbe mashavu mkadhani tunajali sana mnapokosoa viongozi wa upinzani kwa matusi na maneno ya kutunga, Hapana ! Tunawapuuza tu. Viongozi wa upinzani hawakusanyi kodi zenu, hawana nafasi ya kutekeleza ahadi zao, hawana dola, sasa mki-mnapowasakama eti Lowasa ooooh Mbowe huku Sumaye eti ahhh hata haka Kamwasanga nako NO ! mnakuwa kama watoto wa nguruwe walionyimwa maziwa na Mama yao, mjue wa kumlaumu ni rais Maghufuli na Serikali yake, wengi mnatoka mapovu mnakauka mate mdomoni acheni. Nawashauri tuungane serikali ihudumie wananchi, itoe mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, iwaonee huruma mama ntilie, wastaafu, itupie jicho kwa vijana wasio na ajira.
Vijana wenzangu naamini si kweli kwamba mnakipenda Chama Cha Mapinduzi hapana ni hulka tu za kujipendekeza kwa watu wenye madaraka ndio zinawaweka huko kwa maana nyingine kama CHADEMA ingeshika dola mngeweza kuhamia CHADEMA kwa sababu hamna fikra kinzani na ni kweli kwamba akina sisi tungehamia Chama Cha Mapinduzi ili tu kuikosoa, kuielekeza, na kuifunda serikali ya CHADEMA. Tunaikosoa serikali ya Maghufuli na Maghufuli mwenyewe kwa kuwa sisi ni Mbadala wake
Vijana wenzangu lazima mjue kazi ya kukosoa serikali za kiafrika ni kazi ya kijasiri, kama huna ujasiri huwezi kufanya hivyo, ndio maana hatuwezi kukaa meza moja. Tunachoamini sisi, na tunachojua ni kwamba kuna mengi ya kukosoa na tutakosoa bila kuogopa lazima binadamu tujue hakuna atakae ishi milele na kama huijui kesho lazima ujue kufa ukiwa na viungo vyote ni Bahati na ni mpango wa Mungu na kufa ukiwa umeondolewa kiungo chochote kwa kutetea watu wa Mungu ni mpango wa Mungu pia
Kwa hiyo vijana wenzangu tufunge mwaka tukijua tunakosoa kwa faida yetu kama watanzania tunaoishi leo na watakao ishi kipindi kijacho yaani watoto wetu na wajukuu wetu.
Najua wapo watao jitoa ufahamu na kuanzia kutukana upo huru kufanya hivyo kwa kuwa utakuwa ni utashi wako na ndio Malezi yako.
Namuomba Mungu atupe hekima, atuongoze na atulinde sote na atuwezeshe kuuona na kuuishi mwaka 2018 na miaka mingine ijayo