Ndugu wana JF heshima mbele,
Tangu gorofa lianguke jijini Dar na kuua watu, nimekuwa nikitafakari sana ni magorofa mangapi tena marefu zaidi ya lililoanguaka juzu na kuua makumi ya watu. Siku si nyingi zilizopita hata tume iliyoundwa (kiini macho) haijakamilisha vizuri kazi yake, GOROFA la secondari lilianguka na kuua 60% ya wanafunzi wote wahitimu wa kidato cha nne, 28% yao ni mahututi karibu ya kufa, wengi wao walikatika viungo na kubaki vilema hata hawana tumaini kwamba wakipona wanaweza kujifanyia lolote la maana. Gorofa liliangukia vichwa vyao na kuharibu ubongo kazi watakayoweza kuifanya ni kuomba omba au kufanya kazi za kutumia nguvu ambazo pia hawana na si akili.
Nasikia hata hao wanaosemekana walinusulika bila kuumia, kumbe nao waliumia vibaya lakini ilikuondoa aibu na lawama kwa mwenye gorofa walipelekwa hospitali wakaaruhusiwa kwenda nyumbani.
Hili gorofa la sekondari lilikuwa lefu sana, na limekuwa likianguka na kuua, tume zinaundwa lakini utafiti haufanyiwi kazi, mwaka 2010 lilianguka tume ya watu kumi ikaundwa, ikaja na mapendekezo 27 hata moja halikufanyiwa kazi. Leo limeanguka kwa kishindo tume imeundwa lakini haina jipya maana kinachoangusha magorofa hapa nchini kinajulikana. Kishindo cha gorofa la sekondari cha mwaka huu ni cha mtoto na tungoje cha mwaka ujao hapo tume zitaundwa mia, lakini hakuna kitakachofanyika mpaka tatizo la msingi lijulikane.
Gorofa jingine refu kuliko yote ambalo limekwishaanza kutitia na kishindo kikuu kinasubiriwa kwa huzuni ni gorofa letu la AMANI na MSHIKAMANO wetu kama watanzania msingi wa gorofa hili ulijengwa na wazee wetu kwa muda mrefu. Lakini kwa sababu ya uchu wa madaraka na siasa uchwala msingi wake umeanza kuchimbwa kwa kutumia makoleo ya udini, ukabila na ukanda. Wako watu wanaoona ni bora nchi ikaingia katika machafuko ya kidini na kikabila lakini hawako tayari kuona nafasi zao zinatishiwa. Hili gorofa nisinge penda kuliona linaanguka maana kishindo chake ni kikuu na inawezekana waasisi wa kuangushwa kwake hawajui kuwa huenda likawaangukia na wakawa wa kwanza kati ya watakao rejea kwa baba.
Magorofa ni mengi sana ambayo kila siku yanaanguka na kuua mamia kwa maelfu, kuna gorofa la afya, nishati na madini, bandari, miundombinu n.k. wao wanao yaangusha wamokwenye GOROFA LAO wanaloliona ni imara na kwamba litadumu milele wakichekelea. Wakiona wananchi wanatakakuja juu, wanawadanganya kwa kuunda tume kisha wakipoa hata matokeo ya tume hawayaoni na wala hayafanyiwi kazi. Vilio viko kwao wananchi walala hoi na si kwao. Wao wakiumwa hupelekwa kwenye magorofa ya afya ya wenzao huko India na Marikani hawana cha kupoteza!
Ndugu watanzania wenzangu mimi naona dawa ya kumaliza magorofa kuanguka ni kuliangusha gorofa ambalo huwahifadhi waangusha magorofa yetu. Na tuliangushe kwa kishindo kikuu lisagike tiki tiki.
Mwaka 2015 na tuliangushe GOROFA!