Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,828
- 26,236
Mheshimiwa raisi wetu wa Tanzania heshima kwako kiongozi wetu mkuu.
Kukiwa kumesalia masaa machache tuuage mwaka wa 2013 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014 ninaomba mambo muhimu yafuatayo uyafanye.
Nikiwa raia wa Tanzania mwenye haki zote za kikatiba ikiwemo haki ya uhuru wa kutoa maoni, ningependa kutumia nafasi hii kukupongeza kwa jitihada zote ambazo umezifanya katika mwaka huu mzima ulopita, kuhakikisha unafanya yale ambayo ulikusudia tangia ulipofanya kampeni zako mbili za kugombea uraisi kwa ajili ya mihula miwili.
Na katika pongezi hizo basi, ni budi kukupongeza kwa kumteua mheshimiwa Dr Harrison Mwakyembe kuwa waziri wako wa uchukuzi, zizara ambayo ameiongoza na matunda ya jitihada zake za kuboresha wizara hiyo pamoja na asasi zake kadhaa zikiwemo, bandari ya Dar-es-Salaam , uwanja wa JNIA, idara ya mizani, pamoja na hili jipya la yeye waziri kwenda mwenyewe bandari ya Zanzibar.
Pia nakupongeza kwa uteuzi wako wa mheshimiwa John Magufuli ambae wizara yake ya ujenzi mpaka sasa inajitahidi kujenga barabara kwa kasi nchini kote ingawa bado kuna matatizo katika baadhi ya barabara hasa ile ya morogoro ambayo inaonekana kwa sasa imeharibiwa na magari ambayo yamekuwa yakipita hata kabla lami haijakauka hivyo kusababisha kujitokeza kwa mabongemabonge ya lami ama katikati ya barabara hizo au pembenizoni mwake.
Hali kadhalika nakupongeza kwa uteuzi mpya uloufanya jana wa mkuu mpya wa jeshi la polisi afande Ernest Mangu na naibu wake afande Abdulrahman Kaniki na leo umewaapisha rasmi kuwaruhusu maafande hao kuanza rasmi kutekeleza majukumu yao mapya.
Mheshimiwa raisi, nafahamu una majukumu mengi mno na jukumu la kupewa mamlaka na wananchi kuwaongoza ni kubwa na linahitaji kutuliza kichwa na bila shaka hata afya yako inabidi uiangalie na ndio maana hata juzi ulikwenda USA kuangalia afya yako ingawa bado unaonekana upo "fit" lakini kufanya MOT (uchunguzi) ya afya ni muhimu sana hasa kwa watu wenye nafasi kama wewe.
Kama unavyofahamu juzijuzi kulizuka majambo Bungeni na baadhi ya mawaziri wako ikabidi waachie majukumu waliyopewa kwa kujiondoa ingawa utakuwa uliwapigia simu kuwaambia kabla kusudio lako kwamba huwahitaji tena kukusaidia kwenye baraza lako la mawaziri. Suala la kufanya uteuzi wa mawaziri ni gumu na linahitaji ushauri makini na wa kuaminika, naamini washauri wako ndio wanamaliziamalizia orodha ambayo unapenda imalize lala salama ya muda ulobakiza wa serikali yako ya sasa.
Mheshimiwa rais tulielekea ukingoni kwa mwaka huu wa 2013 ningependa kutoa dukuduku langu kuhusu mambo mawili ya kuzingatia pale unapopiatia tena orodha ambayo bila shaka tayari unayo ya baraza jipya ingawa unaweza kuangalia tena kama inawezekana kufanya marekebisho haya mawili.
Nafahamu kwamba serikali ni sirikali na si kila jambo ambalo serikali inapanga au kuandaa ni lazima liwe wazi kwa raia wake, lakini naamini kwenye hili suala ambalo linahusu maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla ni lazima ufike wakati wananchi nasi tusikilizwe.
Mheshimiwa raisi, ningependa kuona unatengua uteuzi wa waziri mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda na kumpa nafasi hiyo mheshimiwa Dr Harrison Mwakyembe. Sababu ni wazi ambazo ni uchapaji kazi, kujituma na ufuatiliaji wa karibu wa utendaji na hiyo kazi Mheshimiwa Dr Mwakyembe anaiweza, na atasimamia kikamilifu utendaji wa shughuli za serikali bungeni.
Katika ziara zake mikoani ambazo zimeigharimu mamilioni ya pesa za walipa kodi, mheshimiwa katibu mkuu Kinana alikwishasema kwamba CCM kwa sasa imechoka kuwabeba mawaziri mizigo, hivyo hiyo ni nafasi tosha kwa wewe mheshimiwa raisi kuliangalia hili na kuteua mawaziri wachapa kazi, ambao wataongozwa na mheshimiwa Dr Harrison Mwakyembe.
Mheshimiwa raisi wizara ingine ambayo ningependa iangaliwe upya ni wizara ya maliasili na utalii na haitakuwa jambo baya kama waziri Magufuli akapewa wizara hiyo ili angalau asafishe kwa makini.
Jambo la pili kubwa ni la kuhusu wizara ya mawasiliano ambayo ipo chini ya mheshimiwa January Makamba. Mheshimiwa Makamba tangu ateuliwe kuongoza wizara hii bado hajaweza kuboresha mambo mawili, jambo la kuwatoza ada ya sm card watumiaji wa simu ambao wanalipishwa ada hiyo ambayo iiliahidiwa hapo kabla kwamba ingezungumzwa bungeni na badala yake ikapitishwa na ni wananchi wa kipato cha chini ndio wanaoathirika na sio wale wenye uwezo.
Pia kama hufahamu mheshimiwa raisi, tangia majuzi wale wananchi tuishio nje ya nchi tumekuwa tukipata matatizo ya kuunganishiwa simu tuzipigazo kuelekea Tanzania hivyo kukosa mawasiliano muhimu hasa ya kama wakti huu ambapo tunataka kuwapa salamu za kheri ya mwaka mpya wale ndugu zetu wa karibu.
Tatizo sidhani kama litakuwa uwingi wa simu ziingiazo Tanzania bali ni ubora wa mitambo ya simu ambayo inatumika pale TTCL. Kuna tetesi kwamba hii mitambo ni ya kutoka Uchina taifa ambalo kwa sasa ndio rafiki wetu kipenzi katika biashara na mahusiano ya kidiplomasia. Lakini tangia waziri huyu uliemteua kushika wizara hiyo ambayo ni moja ya wizara muhimu kabisa nchini mwetu, bado hajaweza kuangalia suala hili la mitambo inayotumika katika kuwezesha mawasiliano ama iwe ndani ya Tanzania au zile simu za kutoka nje na inadhaniwa kuwa kuna kasoro kwenye hii mitambo.
Hivyo basi lingekuwa jambo la busara kumteua mtu ambae ana ujuzu katika masuala ya mawasiliano ili aweze kuangalia suala la mawasiliano ha hasa mitambo, ambayo ununuzi wake kutoka nje ya nchi hakuna anaefahamu utaratibu wake.
Mheshimiwa raisi wetu, mimi nimefikia kikomo katika kuandika barua hii ambayo itakuwa ni moja ya zile posts zangu kwenye Jamii Forums ambayo ni forum ninayoshiriki kwa miaka takriban saba sasa.
Nakutakia kila la kherikatika kuuaga mwaka huu wa 2013 wewe na familia yako na Mwenyei Mungu akijaalia basi In-shal-lah, tutauona mwaka ujao salama.