Mwafrika na Uongozi

Mwafrika na Uongozi

nkobagu

Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
26
Reaction score
11
Nikiwa mwafrika nimekuwa nikitazwa sana na namna waafrika tumekuwa tukifanya mambo yetu: kisiasa, kiuchumi, kisayansi n.k. Kwa wasomaji wa historia watakumbuka mojawapo ya "excuse" ya wazungu kutawala Afrika (Kwa njia ya ukoloni) ilikuwa ni kwamba sisi hatuwezi kujitawala wenyewe na kwamba wangerudisha uhuru wetu tutakapokuwa na uwezo wa kujitawala. Classic mfano ni Tanganyika, ikumbukwe nchi hii haikuwa koloni la Waingereza bali walikuwa ni "trustees" kwa niaba ya league of nations, hii ni baada kunyang'anywa kutoka kwa Wajerumani.

Jukumu la waingereza ilikuwa ni kuisimamia Tanganyika mpaka pale itakapoweza kujitawala yenyewe, kwa muktadha huo hoja ya kurejeshewa uhuru Tanganyika ilikuwa ni kui-convince league of nations ya kwamba tumefika wakati tunaweza kujitawala wenyewe, hoja ambayo Julius Nyerere aliijenga kwa mafanikio na Tanganyika kupata uhuru Desemba, 9, 1961.

Swali ni kwamba kwa takribani miaka 60 je nchi zetu za kiafrika zinaweza kutembea kifua mbele na kusema tumeweza kujitawala wenyewe: kiuchumi, kisiasa, kisayansi, kitamaduni na katika nyanja nyingine? Classic mifano Tanganyika, Afrika Kusini, Zimbabwe nk.

Nawasilisha
 
bado sana, ndio maana juzi kati trump katudharau na anajua fika hakuna nchi ambayo itanyoosha kidole, hii ni kwakua bado tunawategemea kwa kila kitu!
 
Back
Top Bottom