Mvutio angani leo jioni - Zuhura (Venus), Mirihi (Mars) na Mwezi hilali (crescent Moon)

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
285
206
(See the English version below....)

Sayari za Zuhura na Mirihi (yaani Venus na Mars) zinakaribiwa na Mwezi hilali leo jioni karibu upeo wa magharibi mara baada ya Jua kuchwa. Angalia picha iliyoambatishawa.

Leo jioni ukiangalia mara baada ya Jua kuchwa karibu na upeo wa magharibi, kiasi cha nyuzi 20 juu ya upeo, utaona Mwezi hiliali nyembamba kushoto tu ya nyota inayong'aa sana ambayo ni sayari ya Zuhura. Mwezi na Zuhura zitakuwa jirani kiasi cha nyuzi 10 tu. Pamoja na hiyo Mirihi, ambayo ni sayari inayong'aa kama nyota nyekundu, itakuwa kiasi cha nyuzi 10 juu ya Zuhura. Mwezi hilali, Zuhura na Mirihi zitatatengeneza umbo la pembe tatu yenye pembemraba (right angled triangle) na kuleta mandhari ya kuvutia sana angani.

Kesho, Jumatano tarehe 1 Machi, Mwezi hilali utasogea juu jirani na Mirihi kiasi cha nyuzi 5 tu na pembe tatu na Zuhura itageuka kuwa nyembamba.

Wale walio na darubini ya kuweza kuangalia sayari ya Zuhura kwa jirani zaidi watashangaa kuona Zuhura nayo inaonekana ikiwa na umbo la hiliali, kama vile wa Mwezi.

Sayari ya Zuhura hubadilisha umbo lake katika mzunguko wake wa siku 584 wa kuizunguka Jua, kama vile Mwezi unavyobadilisha umbo lake kila mwezi katika mzunguko wake na Dunia.

Wale wanaohitaji kuangalia kwa undani zaidi, hii ni nafasi ya kutambua sayari ya Uranus kwa vile nayo ipo kati ya Mwezi hilali na Mrihi siku ya Jumatano tarehe 01 Machi. Utahitaji kuwa katika eneo ya giza sana na sehemu za bara mbali kabisa na miji ambazo huchafua hali ya mwanga angani. Uranus inabaki karibu na Mirihi kwa siku chache ikiwa inasogea mbali kila siku.

Zuhura, Mirihi na Mwezi hilali tarehe 28 Feb na 01 March.jpg


ENGLISH VERSION:
Venus, Mars and the crescent Moon will be seen close together today in the evening soon after sunset close to the west horizon. See diagram below.

This evening, Tuesday 28 February, if you go out soon after sunset and look about 20 degrees above the west horizon you will see a thin crescent Moon left of the shining evening star which is the planet Venus. They will be about 10 degrees apart. Also, 10 degrees above Venus you will see a red star which shines with a steady light. This is Mars. Venus, Crescent Moon and Mars will form a right angle triangle and will present a beautiful sight in the night sky.

Tomorrow, Wednesday 01 March, the crescent Moon will shift upwards close to Mars and will be separated by about 5 degrees. The Venus, crescent Moon, Mars triangle will change to a thinner triangle.

If you look at Venus through a telescope you will be surprised to see that Venus is also seen as a crescent similar to the Moon !! When Venus moves around the Sun every 584 days it changes phase similar to the Moon which changes phase when it moves around the Earth.

Those who would like to look in further detail can take this opportunity to identify Uranus which is in between Mars and crescent Moon on 01 March. You will need to be in a dark sky in a rural area away from city lights which cause light pollution due to reflections from the atmosphere. Uranus remains close to Mars for several days while they move apart day by day.

Venus, Mars, Crescent Moon and Uranus at sunset on 28 Feb and 01 March.jpg
 
niliona jumapili maghsrib kitu angavu kama ndege ipo karibu kumbe ni zuhura.
 
Juzi usiku niliona zuhura soon after sunset. Nilijua ni hiyo kwa kuhisi kwani ninapenda kufuatilia elimu ya anga
 
ila tangu mwezi huu wa pili uanze sayari ya venus imekuwa ikionekana angani mapema tuu baada ya jua kuzama
Ni kweli. Inaonekana kama nyota ya jioni upande wa magharibi jirani na upeo tangu mwezi Septemba. Ilipanda juu hadi nyuzi 45 na sasa ndiyo inateremka tena hadi itapotea katikati ya mwezi huu.

Baada ya mwezi mmoja itaonekana alfajiri upande wa mashariki na kuendelea na mzunguko tena.
 
Ni kweli. Inaonekana kama nyota ya jioni upande wa magharibi jirani na upeo tangu mwezi Septemba. Ilipanda juu hadi nyuzi 45 na sasa ndiyo inateremka tena hadi itapotea katikati ya mwezi huu.

Baada ya mwezi mmoja itaonekana alfajiri upande wa mashariki na kuendelea na mzunguko tena.
mkuu ukiacha venus na mars kuna planet nyingine ambayo huonekana kwa naked eyes?
 
Haya tu nashukuru mkuu tutajitahidi kuzitafuta hizi mihili na hilali na zuhura usiku kikwazo mawingu
 
Rekebisha kidogo zuhura siyo nyota ni sayari
Ni hilo tu mkuu
Asante kwa angalizo.

Ni kweli Zuhura ni sayari, lakini huwa angani huonekana kama nyota kwa hiyo anayeangalia hiyo anaiona kama nyota.

Inaweza kutofautishwa kama sayari iwapo tu mtu ataiangalia moja kwa moja kwa dakika chache na kuangalia kama inameremeta au la. Sayari hung'aa kwa utulivu moja kwa moja bila kumeremeta wakati nyota lazima itameremeta.
 
Back
Top Bottom