Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,278
- 8,868
Hali ya afya ya Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi aliyelazwa katika Hospitali ya Millpark nchini Afrika Kusini inaelezwa kuwa ni mahututi.
Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia akizungumza jana bungeni mjini Dodoma wakati akichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Katiba alisema, kutokana na hali ya mjumbe huyo kuwa mbaya, aliwaomba Watanzania kuendelea na sala kwa ajili yake.
Mbatia alisema, Kwa kuwa tunazungumzia suala la katiba huku mmoja wa wajumbe wake Dk Mvungi ni mgonjwa, tunahitaji kufanya mchakato huu kwa kuweka mbele masilahi ya taifa.
Hali yake Dk Mvungi bado ni mbaya sana huko katika hospitali ya Millpark na anahitaji kuombewa, hivyo Watanzania wote tumwombee, alisema Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.