Mvomero: Mifugo inakufa kutokana na Ukame

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,849
67,285
Mifugo hasa Ng'ombe katika Mkoa wa Morogoro, wilayani Mvomero maeneo ya Wami Sokoine inafariki kutokana na kukosa chakula.

Wafugaji hasa wa jamii ya Kimasai wanadai hali ya Ukame imechangia kwa kiasi kikubwa mifugo hiyo kupoteza maisha na kusababisha uwepo wa Mizoga mingi iliyosambaa maeneo hayo hali inayosababisha mlipuko wa Magonjwa maeneo hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kebwe S. Kebwe amekiri uwepo wa Ukame mkoani mwake na ameahidi kuwasaidia Wafugaji hao kutokana na Ukame uliowakabili.

Source:
BBC Swahili, Dira ya Dunia.
 
Subiri kwanza hawajamalizana na yanga.
Tukimaliza tutakuja...
 
Eneo jingine ni Ukanda wa mvuha huko mizoga mingi imeoza porini na kusababisha inzi wengi wanene wa kijani na njano kuonekana hata maeneo yalipo maembe, hii ni hatari kwa afya ya wakulima wanaopita maeneo hayo wanaweza kubeba vimelea vya magonjwa kwenye miguu, viatu au nguo na kurudi navyo kwenye makazi. Na kama mvua zikinyesha hapo tutarajie mito kufurika mabaki ya mizoga
 
Wauze tu mifugo yao,kwani ni lazima wafuge? kwanza wamasai hawana maana,unakuta mtu anamiliki ng`ombe 400 harafu wakifa 10 analalama
 
Hivi ukame mnaozungumzia ni upi? Wamrudie mungu kwa kutoa sadaka za kuteketeze
 
Back
Top Bottom