Nakumbuka kuna wakati miaka kadhaa nyuma nilichangia uzi mmoja, kama sijasahau kulitokea ajali ya Mtumbwi wakafa Wanafunzi/Watoto kadhaa.. nilijaribu kuhoji jinsi inavyokuwa ngumu kwa Mtu asiye na uchaguzi (choice) ya usafiri mwingine.
Mimi ni Miongoni mwa Watu wanaoogopa sana usafiri wa kwenye maji na angani hasa ikiwa ni kusafiri na zile Ndege ndogo.
Kuna wakati kwenda Zanzibar kutoka Arusha nilipata fununu kuwa kuna tiketi zinatumwa kuondoka na Ndege ndogo ya kampuni moja (wakiwa kama moja ya sponsor wa shughuli tunayoiendea)..nilitangulia Dar fasta kwa basi kabla tiketi haijanikuta ili baadae nipande 'Kilimanjaro' niende zangu Zenji kwa gharama zangu.
Sasa huwa najiuliza, hivi inakuwaje kwa Mtu asiye na uchaguzi/choice ya usafiri?