Muziki wa sasa mtihani

Muziki wa sasa mtihani

Fbn

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
14,138
Reaction score
33,532
Miziki ya sasa hivi ni kama aibu !

Kama una umri fulani itakubidi kuchagua aina za miziki .

Kwa wale mnaofahamu lugha kutokana na miziki mtakuwa mnaelewa.

Tuje kwenye miziki yetu ya ndani hapa tanzania tena kizazi hiki.
unajua tena ofisi binafsi kama unamiliki kuwa na tv ni jambo la kawaida.

Sasa chaneli iliyowekwa ikawa inapiga nyimbo hizi za vijana.

Kuna nyimbo moja ya kadada kamoja kana jiita vitu vilivyomo kwenye bustani ,mtajua kwenye bustani kunatakiwa kuwekwa nini ila sio za bustani ya vyakula.

Ile nyimbo kwa kweli ni aibu kama inavosema "mwagia ndani ,mwagia ndani chakula ya watoto"

Suala jingine kwenye miziki ya sasa kuna maneno ya ajabu ajabu na si kiburudisho.
 
Tunatengeza kizazi kibovu watoto wanaharibika mapema sana baada ya miaka ijayo tutakuwa na jamii iliyoharibika na kukosa maadili
Tulipowasema tukaambiwa tunaharibu brand zao ambazo ni ngumu kuzijenga tena zikishaharibika. Tukaambiwa tuwaache.
 
Maua sama sio, Ubunifu kwasasa ni zero.
yule tangu mwanzo wimbo wake wa IOKOTE aliimba matusi humo na basata wakapotezea nyakati zikapita, basata huwa wanapigwa chenga kidogo sana, wimbo unajazwa matusi ya kingono unaachiwa mitaani watu wanaserebuka nao
 
mbaya zaidi zinatwanga mitaani in public basi balaa tupu...watoto wadogo wanaziimba kila kukicha...

Juzi nilipita mahala nikakuta watoto wanaimba "mdangaji malaya" sijui nini nini huko dah ilibidi niwafokee wale watoto japo nilionekana kituko kwenye ule mtaa...
 
Wasanii wa siku hizi haijulikani wanatunga nyimbo wakiwa na hali gani kihisia. Kwa kuwa wana majina makubwa na umaarufu wanajua wakitunga nyimbo yeyote itapokolewa kwa shangwe. Mwingine akiwaza mapenzi na ngono hapo hapo anatunga mashairi, mwingine ni mlevi wa pombe akiamka na hang over ya pombe kichwani ni kutunga mashairi ya kuisifia pombe tu, mpaka sasa hivi watoto wadogo wanaimba wimbo wake mtaani bia tamu. Ukiuliza watoto hao ni kweli bia tamu wanakujibu chungu. Ina maana watoto waliposikia wimbo huo wa kusifia bia tamu wakaenda kuonja wajue utamu wake ukuje mpaka usifiwe na msanii huyo wakakukuta ni chungu
 
Mbaya zaidi zinapigwa kwenye school bus, Dah!
 
Ndio tasnia ya burudani ilivyo kwa sasa sijui audience ndio tunazipenda au wasanii wenyewe ndio wameamua kutuforce kuzipenda
 
Kuna wasanii wengine hutunga nyimbo zisizo na madhara kwa jamii, wimbo wa kuwa mtanashati unaoitwa tisheti na jinsi, kila mmoja anapendeza, wimbo hauna matusi wala ulevi. Bora wasanii wakatunga nyimbo za kuhamasisha vijana wafanye kazi kwa bidii, wasome kwa bidii kuliko kuimba nyimbo za aibu
 
Na wewe unayepata muda wa kuwasikiliza mpaka kulenta Uzi humu JF, sidhani kama kuna tofauti yoyote kati yako na wao!
 
Siku hizi wamejaa wababaishaji tu

Wanaimba ujingujing

Ukiimba msg hupewi promo

Ngoja nmsikilize mwanangu salu T hapa

Ova
 
tatizo linaanza kwetu sisi, wakiimba matusi mashabiki kibao, wanaojaribu kuimba nyimbo za kueleweka kijamii wanajikuta wanaishia kujiona wapo peke yao.
 
Back
Top Bottom