Muwa uliozamisha meli

Muwa uliozamisha meli

Jayspeed

Senior Member
Joined
Feb 23, 2014
Posts
156
Reaction score
169
Kuna story fulani kipindi fulani niliisoma iliitwa Muwa uliozamisha meli.. yule nahodha wa meli ile alipokuwa akisafiri na miwa mitamu akaamua aonje kidogo baada ya kuonja akanogewa akaanza kula mwisho wa siku alisinzia na chombo kikazama na habari yake ikaisha..
Story ile ilinipa mawazo mengi sana na kwa fikra zangu za kitoto nikawa nawaza mua huo utakuaje hadi upelekee Meli kubwa vile kuzama? Na je nahodha haruhusiwi kula muwa ndani ya meli?

Akili iliwaza muwa tu.. waandishi wa zamani walikua wanafikiria sana na kuandika bana tofauti kabisa na hawa wa kipindi hichi yaani bila umbo namba nane na sjui Saa sita mara taa ikazimwa wanakosa cha kuandika kabisa nadhani maisha ya zamani ya waandishi yaliwafanya wafikiri mbali zaidi nadhani.

kila siku kwenye maisha yetu na zama zinavyozidi kupita idadi kubwa ya Manahodha wanaoangusha meli kwa kunogewa na Muwa inazidi kuongezeka. Shida ni kuwa ukianza kula Muwa ule ndani ya meli na huku wewe ni nahodha chombo kitaenda mrama tu sababu MUA ni mtamu zaidi Kuliko safari.

Wataalamu wa mambo ya bahari na Meli wanasema kuwa Manahodha wengi wa siku hizi wanapewa majukumu wakiwa wadogo bado, tofauti kabisa na manahodha wa kipindi kile cha uhuru Manahodha wa kipindi kile walikua na weledi wa kazi, heshima, nidhamu na utii lakini hawa wa siku hizi hawana uvumilivu kabisa, wana tamaa kila wakiaminika na wenye Meli wao hushindwa kutunza uaminifu mpaka mwisho wa safari, mbaya zaidi ukiwasifia tu wao ni hodari basi wanavimba kichwa wanaamua kabisa kuweka miguu kwenye usukani wanavuta Muwa wanaanza kula wakiamini kuwa uhodari wao hawaezi angusha Meli na wala hawaezi sinzia, hawajifunzi kwa mifano ya waliopita hata kidogo tena wao ndio huwakosoa zaidi wanadai wenye meli hawakujua kuteua manahodha bora kipindi hicho..

Nasikia kuna Nahodha amepatikana huko akiwa HAI baada ya kuzamisha meli, kaua abiria wengi katia hasara kubwa sana, nasikia wenye meli wanafanya uchunguzi. Je, nae Alikula Muwa akajisahau au yeye hakuwa na vyeti vya unahodha? Lakini kwenye vyeti hapana maana wenye Meli walishatokomeza swala la vyeti feki kitamboooo. Nasikia pia wanasema Nahodha yule alikuwa mjanja sana na hodari hakula Muwa peke yake alikata vipingili akagawanya kwa watu wake wakaribu alioongozana nao katika safari na wote walinogewa hata meli ilipokuwa ikianza kuzama meli zilizokuwa jirani zilipiga honi kumpa tahadhari lakini wale wapambe wake walimwambia achana nao hao Meli haizami bali wanakuonea wivu unavoendesha meli yako kwa makeke na manjojo huku unakula Muwa.

Kutokana na kuwaamini watu wake wa karibu Nahodha aliendelea kula Muwa miguu kwenye usukani watu wake nao wakazidi kumchagulia Ule Muwa mtamu zaidi nasikia pia wanasema eti.. eti... atakua Mfano kwa Manahodha wengine lakini pia nasikia kuzama kwake na kutoka HAI kunaondoka na wengi sana wengine ambao hata hawakujua hili wala lile nao wametajwa huko uchunguzini.. wanajuta sasa lakini majuto kashakua mjukuu tayari.. Ngoja sisi tuone maamuzi ya wenye Meli wataamua nini juu ya nahodha yule mwenye makeke na njonjo awapo baharini.

Saa hizi bado ni Mbaya

Sultan
Screenshot_20210616-072058.jpg
 
Write your reply...suala la wakuu wapya wa wilaya limewachanganya wengi
Swala la wakuu wapya lipo tu na list ipo kitambo na wanaotoka wanajulikana pia labda abadili mkeka kutokana na matokeo ya ugenini au nyumbani....
 
Back
Top Bottom