muvi hii ya kibongo ina afadhali

chief72

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
623
500
mi ni mpenzi wa series kama 24, p/break, lost, fringe, heroes,revolution,walking dead, nk.....kuna siku bwana mdogo kaniletea muvi ya kibongo na akaniahidi sintoboreka nayo, kwa shingo upande nikaanza kuiangalia, infact wamejitahid nakushauri na we mwenzangu itafute inaitwa SHIKAMOO MZEE, kacheza mzee majuto,JB, shamsa ford na wengineo,kubwa nililo enjoy ni umahili wao wa kuongea na kujishahibisha na kuwa watoto wa mjini, kwa kweli ina afadhali ukilinganisha na zingine, kwa jinsi nivo iona sijui wadau kama mmeiona mwasemaje
 

Ponera

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
556
0
mi ni mpenzi wa series kama 24, p/break, lost, fringe, heroes,revolution,walking dead, nk.....kuna siku bwana mdogo kaniletea muvi ya kibongo na akaniahidi sintoboreka nayo, kwa shingo upande nikaanza kuiangalia, infact wamejitahid nakushauri na we mwenzangu itafute inaitwa shikamoo mzee, kacheza mzee majuto,jb, shamsa ford na wengineo,kubwa nililo enjoy ni umahili wao wa kuongea na kujishahibisha na kuwa watoto wa mjini, kwa kweli ina afadhali ukilinganisha na zingine, kwa jinsi nivo iona sijui wadau kama mmeiona mwasemaje

umetumwa kuja kutoa promo?
 

Mwana Ilala

JF-Expert Member
Jan 29, 2013
1,290
1,500
Itengenezee Link-tuweze kui-download Kamanda. Tukiiona iko Poa tutaenda kununua.
 

suleym

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,941
2,000
umetumwa kuja kutoa promo?

sidhani kama ni promo kitu kikiwa kizuri si mbaya kukisifu, hata mie nimeiona kwa "bahati mbaya" nikiwa safari kwenda tanga ni nzuri kwa kiwango chao hasa mzee majuto na jb wameigiza vyema kabisa.
 

suleym

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,941
2,000
mi ni mpenzi wa series kama 24, p/break, lost, fringe, heroes,revolution,walking dead, nk.....kuna siku bwana mdogo kaniletea muvi ya kibongo na akaniahidi sintoboreka nayo, kwa shingo upande nikaanza kuiangalia, infact wamejitahid nakushauri na we mwenzangu itafute inaitwa SHIKAMOO MZEE, kacheza mzee majuto,JB, shamsa ford na wengineo,kubwa nililo enjoy ni umahili wao wa kuongea na kujishahibisha na kuwa watoto wa mjini, kwa kweli ina afadhali ukilinganisha na zingine, kwa jinsi nivo iona sijui wadau kama mmeiona mwasemaje

umenena vyema mkuu nami nimeiona iko powa.
 

time theory

JF-Expert Member
Nov 22, 2013
767
1,000
Muvi za kibongo siku zote zimekuwa nzuri,ushahidi ni mafanikio ya waigizaji wake na hata jinsi wanavyopendwa mfano kanumba.ila ukilinganisha na standard za kimataifa ambazo wachangiaji wengi humu ndio wanazotumia,bado tuna safari ndefu.
 

Ringtone

JF-Expert Member
Nov 21, 2013
489
0
si mmezoea kuziponda tumesifia moja tu hiyo tatizo!!ila ningesema muv za kbongo tope tupu ungeona wachangiaji

Sio tu tope ni kinyesi kitupu,kwa sababu:
1.we sanaa itakuwaje wakati mtu mmoja ndio:mwigizaji,mtunzi,mpiga picha,mwalili,mpambaji n.k.
2.location na mavazi:"zile nguo za kulalia wao ndio wanashindia".hutaona tofauti ya mavazi mtu akiwa nyumbani,mtaani,ofisin
3.filamu ya dakika 70,wao wana weka part one na part two.hizi zaidi zitauzika huko uswahilini ktk mabanda ya video show
4.filamu zao hazina uhalisia wowote:kila filamu lazima utakuta muhusika ana nyumba kubwa la kifahari,gari la kifahari na ofice kuubwa yenye kipato kinene.mitakataka kama hii ndio inapelekea watu wa deal na "sembe"
5.kubwa zaidi ni hili la uzungu "yaani ulimbukeni wa wazungu kwao fasheni".kila kitu ni kuigaiga toka nje halafu wanasema watanzania hawana utamaduni wa kupenda vitu vya kwao!!

Sasa peleka hizo feedback,achana na promo
 

Tugutuke

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
500
250
hakuna muvi aliyoigza mzee majuto na jb uiangalie uboreke! Zote ziko safi tu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom