Muuza nyama ajinyoga buchani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muuza nyama ajinyoga buchani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 22, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MFANYABIASHARA wa nyama na mkazi wa Daraja Mbili jijini Arusha, Lucas Laiser anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35, amekutwa akining’inia katika bucha lake la nyama baada ya kujinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya katani.

  Mwili wa mfanyabiashara huyo ulikutwa na wateja wake saa 12 asubuhi baada ya kufika katika bucha hilo kwa lengo la kununua nyama na kukuta mwili huo ukiwa unaning’inia.

  Baada ya wateja hao kugundua kifo hicho, Polisi waliarifiwa na kufika hapo na kuufanyia upekuzi mwili huo na kubaini kuwa Laizer hakuwa na jeraha lolote mwilini mwake na haikufahamika sababu za kujinyonga.

  Hata hivyo, Polisi walifanikisha kukuta ujumbe ulioandikwa na kijana huyo ambao walishindwa kuelewa kilichoandikwa na kwamba mfukoni alikutwa na Sh 82,000 pamoja na simu ya mkononi.

  Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa ajili ya uchunguzi zaidi, na hakuna anayeshikiliwa juu ya tukio hilo.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi zaidi wa kipolisi unafanywa ili kujua kiini cha tatizo hilo la kifo.
   
Loading...