Muuundo wa serikali tanzania katika katiba mpya

Muuundo wa serikali tanzania katika katiba mpya

tuwe na serikali kumi! serikali kuu na serikali nyingine tisa za majimbo. Majimbo manane ya bara na moja la zanzibar. Majimbo yawe na serikali zao na mamlaka kamili isipokuwa fedha, mambo ya nje, mambo ya ndani na ulinzi. Hii itasaidia sana kuondoa uwezekano wa kuvunjika muungano, itaharakisha maendeleo kwa kuleta ushindani miongoni mwa majimbo. Jimbo/nchi ya zanzibar itaendelea kuongozwa na rais ambaye atakuwa ni makamu wa rais na mwenyekiti wa baraza la Magavana. Majimbo mengine yataongozwa na magavana. Mpango huu utaondoa malalamiko kwa upande wa bara kuhusu zanzibar pia hofu ya wazanzibar kumezwa au kutumika kwenye mambo ya Tanganyika itaisha. majimbo yanaweza hata kuongezeka kama ilivyo Kenya wenye majimbo 47!
Hiyo ni serikali moja mkuu..
Au ndo unataka tuhesabu mpaka serkali za mitaa!
 
napendekeza kuwepo na jimbo la Tanganyika litakalokuwa na mikoa ya Tabora, kigoma, Rukwa na Katavi. Jimbo la Dar es salaam litakalokuwa na mkoa wa Dar es salaam na wilaya ya Bagamoyao na Kibaha, Jimbo Kilimanjaro litakalokuwa na mikoa ya Tanga, kilimanjaro, Arusha na Manyara. Jimbo la Zanzibar litakalokuwa na nchi ya Zanzibar. Jimbo la Victoria Nyaza litakalokuwa na mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara na shinyanga. Jimbo la kati litakuwa na mikoa ya Simiyu na Singida, na Dodoma. Jimbo Nyanda za juu litakuwa na mikoa ya Morogoro, Iringa,Njombe na Mbeya. Jimbo la kusini litakuwa na mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara
Majimbo mawili tu yanatosha yaani jimbo la Zanzibar na Jimbo la Tanzania a.k.a Tanganyika yaani ZNZ atawale Gavana au waziri Mkuu kisha Tz atawale Gavana au waziri Mkuu Rais awe mmoja ahamie Dodoma .kumbuka jina la Tanzania ni Mali ya huku Bara kwani jina Hilo lilitoka huku huku Bara hata Siku muungano ukivunjika Hakuna kubadilisha jina kuludi Tanganyika jina la Tanzania litabakia bara na kule wataitwa Zanzibar kumbuka Kule Newyork UN wanalitambua jina Tanzania sasa iweje kwenda kubadilisha jina wakati jina Tanzania ni Mali ya TZ bara
 
Baba Wa Muungano na Bara na ndiye alikuja na jina la Ubatizo yaani jina Tanzania hivyo jina Hilo ni jina lilitokea Bara ni Mali ya wabara Hakuna haja ya kuludia jina la Tanganyika wakati Tanzania Pia ni jina la Bara kule zenji wanaitwa Zanzibar japo huku kunaitwa Tz Bara lakini si Bara pekee Kama wanavyodhani kumbuka kuna visiwa vya mafia ukerewe ukara na utitiri wa visiwa vingi sana huku Tz hinyo huku panapaswa paitwe Tz Bara na visiwa vyake pia Chezea Tz wewe....
 
Rais + Rais + Rais + Rais = ?

Mtazamo wangu:

Mimi napendekeza serikali tatu, yenye muundo wa Rais mmoja tu wa Jamuhuri,

Serikali ya Tanganyika iongozwe na Waziri Mkuu wa Tanganyika,

Na serikali ya Zanzibar iongozwe na Waziri Kiongozi wa Zanzibar!

Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar.Uk 11-12 link Uongozi-Wetu-Na-Hatma-Ya-Tanzania-by-Nyerere

Serikali ngapi? Jibu : Mbili
Zipi? Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar.

Baada ya hapo, Muungano,Mkutano,ushirikiano, udugu, ujomba na ushangazi ni kupitia Shirikisho la Afrika Mashariki.

Tunaweza kuchagua kama alivyosema Mwl. Nyerere , Njia rahisi au njia ya tabu, ugumu na utata. Kwa kawaida Wadanganyika tunapenda utata na matatizo.
 
Majimbo mawili tu yanatosha yaani jimbo la Zanzibar na Jimbo la Tanzania a.k.a Tanganyika yaani ZNZ atawale Gavana au waziri Mkuu kisha Tz atawale Gavana au waziri Mkuu Rais awe mmoja ahamie Dodoma .kumbuka jina la Tanzania ni Mali ya huku Bara kwani jina Hilo lilitoka huku huku Bara hata Siku muungano ukivunjika Hakuna kubadilisha jina kuludi Tanganyika jina la Tanzania litabakia bara na kule wataitwa Zanzibar kumbuka Kule Newyork UN wanalitambua jina Tanzania sasa iweje kwenda kubadilisha jina wakati jina Tanzania ni Mali ya TZ bara

Pendelea kunywa chai asubuhi badala ya mnazi.
 
SERIKAL MOJA YA JAMHUR YA MUUNGANO WA TANZANIA ILI KUPUNGUZA GHARAMA.MIKOA IWE MAJIMBO NA ZANZIBAR IWE JIMBO MOJAWAPO KTK TZ.MUUNDO WA SERKAL MOJA MPANGO MZIMA,naipenda TANZANIA.
 
SERIKAL MOJA YA JAMHUR YA MUUNGANO WA TANZANIA ILI KUPUNGUZA GHARAMA.MIKOA IWE MAJIMBO NA ZANZIBAR IWE JIMBO MOJAWAPO KTK TZ.MUUNDO WA SERKAL MOJA MPANGO MZIMA,naipenda TANZANIA.

Weye ni mtanganyika mkataa kwao mtumwa,magamba yanaiba rasilimali zenu kwa vile hamna nchi.
 
zenji hawataki muungano hiv hamuelewi?....
Tanganyika kwanza,muungano baadae
 
Back
Top Bottom