Muungano ni ufisadi na mafisadi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano ni ufisadi na mafisadi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Mar 25, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][/h]Written by ole // 25/03/2012 // Habari // 1 Comment


  Na.B.OLE,
  Ushirikiano ni kitu muhimu sana katika maisha ya jamii au Taifa husika katika kuleta usawa na maendeleo kwa wote bila kujali rangi kabila wala sehemu ambayo mtu anatoka.Mara nyingi muungano wowote lengo na madhumuni ni kuboresha uhusiano na kuleta maendeleo kwa wahusika wa chombo hicho.
  Leo hii tumeshuhudia nchi nyingi zikijiunga na kuwa na nguvu moja,sauti moja, lengo ni kuboresha Wananchi wao pamoja na Serikali zao kuleta maendeleo katika jamii zao. Tunayo mifano mingi sana kama vile Marekani na bara ya ulaya lakini hata ukiwacha Mataifa makubwa bado kuna nchi zinashirikiana katika Muungano wao katika nyanja tofauti kiuchumi kisiasa na hata suala zima la utamaduni wa jamii zao zile zenye kufanana.
  Muungano wowote ule hata uwe wa mume na mke nyumbani lazima ujengwe kwa misingi na sheria madhubuti zenye muhimili wa haki sawa kwa wote. Napindipo muhimili mmoja ukikosekana basi Muungano huo hulegalega na hatimae nyumba ile huanguka na kupoteza dira yake.
  Tukija katika Muungano wa Tanzania, ni dhahiri ya kwamba hata kipofu na kiziwi anajua ya kwamba misingi ya haki na usawa imekiukwa, mihimili hii imekosekana na ndio maana matatizo na kero za Muuungano kama vile wanavyoziita wenyewe zimekuwa nyingi bila kiasi. Hii ni kutokana na kwamba wahusika hawakuzingatia maadili ya Muungano tokea hapo awali.
  Mwenye macho haambiwi tazama na wala mwenye masikio basi halazimishwi kusikia, Muungano wa Tanzania ni ufisadi uliofanywa na Mafisadi kulinda maslahi yao binafsi na sio Taifa wala Wananchi wao. Na hio ndio maana unapolizungumzia suala la Muungano Tanzania inaonekana kama vile umemsulubu yesu kanisani au umevunja msikiti.
  Watanganyika walio wengi wanaliona suala la Muungano kama vile nimzaha na mchezo wa watoto ule wakujificha kwenye migomba wakati wa mbaramwezi wanasahau kwamba wanaonekana ni kweupe na hakuna kiza, kutumia mwevuli wa Muungano kiutawala zanzibar, sio haki na wala jambo la kujisifia na kusherehekea.
  Wazanzibar sio wajinga na wala punguani wanafahamu na kuelewa kila kitu kwamba huu ni mwevuli na kisingizio tu kuwepo kwa Muungano bali wanajua fika kwamba wametawaliwa na Tanganyika. Lengo liko wazi na linajulikana kwamba ni kuipoteza Zanzibar katika ramani ya Dunia.
  Kwa vile historia ya Zanzibar iko wazi na Wazanzibar bado wanaendelea kuishi basi haliwezekani haki lazima ishinde zidi ya batili. Muungano huu hauwatendei haki Wazanzibar na tunasema kwa kinywa kipana kwamba haufai na haupo kwa ya ajili ya maslah ya Wazanzibar bali ni kwa ajili ya Ufisadi na mafisadi.
  Tokea kuasisiwa Muungano huu mimi binafsi nasema uliasisiwa kwa bahati mbaya na hayakuwa malengo mahsusi ya mmojawapo kati ya Waasisi wa Muungano huo kwa pande wa Zanzibar. Lengo na madhumuni ya hayati Karume hayakuwa haya tunayoyaona leo hii. Karume alishindwa kujua dhamira na ajenda ya Muasisi mwenzake Mwalim Nyerere, kwamba yalikuwa kuikalia Zanzibar kimabavu bila ya Wazanzibar kushtukia hilo kwa maslah ya tanganyika na Mataifa makubwa ambayo waliona kwa Zanzibar ni tishio kwao..
  Watanganyika walipata ushauri kutoka kwa Mataifa makubwa jinsi na mbinu za kutumia kuivunja nguvu Zanzibar na ifikie wakati ishindwe kujiongozana isalimu amri na kuwa serikali moja au sehemu mojawapo ya Tanganyika. Kwanza walikusanya zile sehemu nyeti za dola na kuzifanya ni za Muungano kama vile, vyombo vya ulinzi,fedha,mambo ya nje,uhamiaji,ushuru wa forodha,katiba na mambo mengine muhimu ambayo wanajua kwamba vitu hivyo ndivyo vinavyotoa hadhi,nguvu na utaifa wa Nchi husika.
  Wazanzibar yote hayo tumepokonywa na ndio maana ukaona leo hii Zanzibar inayumba sana ,hii ni kutokana na kwamba Zanzibar imevunjwa nguvu kama mgonjwa wa safura anavyolazimishwa kupiga mafunda ya uji wa muhogo ili apate angalau nafuu ya afya yake.Mafsadi wametumaliza na bado wanaendelea kutukandamiza pamoja na rasilimali zetu.
  Tuangalie leo hii Zanzibar hakuna hata udhibiti wa” passport” baina ya nchi hizi mbili. Taifa la zanzibar limekumbwa na ujambazi mkubwa,uvamizi wa wageni wanaoishi kinyume na sheria,mabadiliko ya utamaduni wa kizanzibar,upungufu wa kazi katika sekta za uchumi, kuongezeka kwa idadi ya watu kushinda uwezo wake na mengi kama hayo.
  Lakini kubwa ambalo hadi hii leo mimi binafsi nashindwa kuelewa nataka tujiulize na pia naomba Wazanzibar wenzangu munisaidie hivi Zanzibar hakuna Wasomi ? Nitoe mfano mmoja tu, mambo ya nje na uhusiano wa Kimataifa, Zanzibar inashindwa hata kutoa Balozi sasa tujiulize jee Nchi zote ambazo zinauwakilishi Tanzania inashindwa kuwakilishwa na Wazanzibar lazima Tanganyika tu, au vijana wa Kizanzibar hawana elimu ya Internationa relationship ? Yote haya ni mipango maalum iliopangwa na Tanganyika kuidhooifisha Zanzibar ishindwe kujitangaza kama nchi na ndio maana hata misaada ya kimataifa ikitolewa basi inaletwa kwa jina la Tanzania huku Wazanzibar wakiwa hawaambulii kitu.
  Hii ni mifano midogo tu ya vitendo ambavyo Watanganyika kupitia mwavuli wa Muungano huwamaliza ndugu zao wa dumu, hivi tujiulize hali itaenda mpaka lini na itatufikisha wapi sisi Wazanzibar ? Jibu la suala hili wanalo Wazanzibar wenyewe, ama kuwafurahisha mafsadi wao au……………..
   
Loading...