Muundo mpya wa serikali una changamoto gani kwenye ajira na bajeti ya 2010/2011?

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2010
Messages
2,163
Points
1,195

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
Joined May 14, 2010
2,163 1,195
Jamani,

Napenda kujua tu kuhusu madhara au manufaa yatokanayo na muundo huu mpya wa serikali kwa wafanyakazi wa idara zilizohamishwa je watahama?

Na wanakohamia kama watahama watahama na vitendea kazi vyao kama vile computer?

Vipi kuhusu bajeti ambayo tayari ilishaidhinishwa na bunge ya 2010/2011, au ndio itabidi bunge liidhinishe marekebisho ya bajeti January/February.

Je hii inatuambia nini kuhusu mapendekezo ya CHADEMA kwamba wizara na muundo wa serikali unatakiwa uainishwe kwenye katiba?
 
Awo

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2010
Messages
794
Points
225

Awo

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2010
794 225
Kuweka muundo wa serikali katika Katiba kunazuia viongozi kupiga dana dana hizo idara bila tija. Kikwete miaka mitano iliyopita alivunja Wizara ya Ujenzi, akaiunganisa na Uchukuzi na Mawasilano, akatuletea Miundombinu. Miaka miwili baadaye akaondoa Mawasiliano, akahamishia kwenye wizara mpya ya Mawasiliano, Teknolojia na Sayansi aliyoimega toka Elimu ya Juu, ambayo aliivunja. Sasa tena amerudisha Ujenzi, ameunda Uchukuzi na blah blah kibao. Kama miaka mitano kumeshakuwepo na majaribio yoye haya ni lini watu watakaa chini wafanye kazi? Kwa mtizamo wangu watu wako busy wanahama na kutafuta ofisi, mark my words hii itaendelea katika miaka mitano ijayo.

Sina uhakika kama CHADEMA wamependekeza muundo was serikali uwekwe kwenye Katiba. Nakumbuka Dr Slaa alisema angekuwa na mawaziri kumi na tano na manaibu watano, nusu ya baraza tulilolisikia leo. Kenya wamelimit namba ya wizara, zisiwe chini ya kumi na mbili na zisizidi ishirini na mbili, kama sikosei. Marekani - ili kuongeza namba ya wizara Rais anahitaji kuungwa mkono na third ya Congress (kama sikosei).

Tanzania na nchi nyingine maskini, pamoja na Uganda yenye mawaziri 100 zinahitaji kudhibiti uundaji holela wa wizara, ambao kwa kweli ni matumizi mabaya ya madaraka. Mtu anakuwa na watu wake, anawaundia wizara na kuwapa wizara. Haya ni matumizi mabaya ya madaraka yanafuatiwa na matumizi mabaya ya fedha za umma.
 
Ukweli mtupu mkuu, nadhani kuna umhimu wa haraka muundo wa serikali ujulikane na ikihitajika kubadirika basi Bunge liidhinishe, siyo blah blah tunazoambiwa na watu wanaochezea akili zetu
 
Forum statistics

Threads 1,390,913
Members 528,291
Posts 34,066,460
Top