Muuguzi ahukumiwa kwenda Jela Miaka Mitatu kwa kufoji cheti cha Sekondari

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
55,296
77,674
Umofia Kwenu wana JF,

Muuguzi kutoka Mara amehukumiwa kwenda Jela Miaka Mitatu au Faini ya laki 6 kwa kosa la kugushi Cheti cha elimu ya sekondari na kukitumia kupata ajira.

Mshtakiwa huyo alilipa faini ya Sh. 600,000 hivyo kukwepa kwenda jela kutumikia kifungo cha
miaka mitatu.

==========================
Musoma. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mara, imemhukumu muuguzi Irene Machagge, kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh600,000 baada ya kumtia hatiani kwa kughushi cheti cha elimu ya sekondari na kukitumia katika ajira.

Taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa vyombo vya habari ilisema hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Karim Mushi baada ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashtaka na mshtakiwa.

Akitoa adhabu, Hakimu Mushi alisema amezingatia utetezi wa mshtakiwa, hivyo kumuhukumu kulipa faini ya Sh500,000 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kwanza, na la pili kulipa faini ya Sh100,000 au kwenda jela miaka mitatu.

Alisema adhabu zote hizo zitatumikiwa kwa pamoja.

Hakimu Mushi alisema Mahakama imemtia hatiani mshtakiwa kama alivyoshtakiwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na Jamhuri bila kuacha shaka yoyote.

Awali, mwendesha mashtaka wa Takukuru, Eric Kiwia aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na watu wengine wenye tabia hiyo.

Kabla ya huku, mshtakiwa aliiomba Mahakama imwonee huruma kwa kuwa ni mjamzito na ana ugonjwa ambao haumruhusu kukaa kwenye eneo lenye joto kali.

Mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Novemba 15, 2015 akikabiliwa na mashtaka mawili ya kughushi cheti cha elimu ya sekondari na kukitumia kujipatia ajira ya uuguzi katika Hospitali ya Mkoa wa Mara.

Ilidaiwa mahakamani na upande wa mashtaka kuwa kati ya Mei na Septemba, 2009 alighushi cheti cha kuhitimu Shule ya Sekondari ya Forodhani mwaka 1995.

Alidaiwa Septemba 3, 2009 aliwasilisha cheti hicho kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, hivyo kuajiriwa kama muuguzi katika hospitali ya mkoa.

Mshtakiwa aliyekuwa akitetewa na wakili Ostac Mligo alilipa faini ya Sh600,000, hivyo kukwepa kwenda jela.



Source: Mwananchi
 
Kwa hili tukio la muuguzi tulitakiwa tuwe barabarani na mabango kushinikiza aidha muuguzi aachiwe huru au Daudi Bashite naye awe jela.

Tatizo la watanzania ni kusema ''hayanihusu'' ila kibao kikigeukia kwake anaanza kuomba sympathy ya umma.
Magufuli kutokumtumbua DAB sababu ya forgery inaleta picha mbaya sana.

Je amemwacha sababu yeye ni ngosha mwenzie?

Je mtu kuwa CCM inampa kinga ya kufanya uhalifu bila kuguswa na sheria?

Je wana private relationship ambayo umma haujui lakini matokeo yake tunayashuhudia?

Maswali ni mengi kuliko majibu.
 
Wamrudishie nesi hela yake,Bashite mbona hawa mgusi?
Ionekane kugushi vyeti si tatizo kisheria.Wabunge wafanye marekebisho sheria hiyo.Raia wote wafaidi sawia kugushi vyeti
 
Shame on u Tz hii sheria inakata upande mmoja tu. Vipi kwa Bashite haimuhusu? Aibu kubwa kwa watawala wetu
 
Kwa hili tukio la muuguzi tulitakiwa tuwe barabarani na mabango kushinikiza aidha muuguzi aachiwe huru au Daudi Bashite naye awe jela.

Tatizo la watanzania ni kusema ''hayanihusu'' ila kibao kikigeukia kwake anaanza kuomba sympathy ya umma.
Magufuli kutokumtumbua DAB sababu ya forgery inaleta picha mbaya sana.

Je amemwacha sababu yeye ni ngosha mwenzie?

Je mtu kuwa CCM inampa kinga ya kufanya uhalifu bila kuguswa na sheria?

Je wana private relationship ambayo umma haujui lakini matokeo yake tunayashuhudia?

Maswali ni mengi kuliko majibu.
All the above
 
Bashite jeeeeeeeeeeeeeeeee?
Jaman ngojeni leo niweke wazi kipindi Daud yupo sekondari alibatizwa alipobatizwa baba yake nae akabatizwa pia babu yake nae akabatizwa ikawa DAUD ALBERT BASHITE lote limefutika,
sasa ni PCM badala ya DAB. sasa msitokwe povi nimewasilisha. PCM piga kazi mkulu hapangiwi!
 
Hapa ni mwendo wa kupakatana tu hakuna kipya tz.
Dadeki natamani ningekua mdunguaji.
 
Back
Top Bottom