Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Mama mmoja amedai kupigwa na muuguzi wakati akijifungua katika hospitali ya Rufaa Meta ya jijini Mbeya na baada ya kujifungua muuguzi huyo akamchukua mwanae mchanga na kumtupia kifuani jambo ambalo amesema lilihatarisha uhai wa mwanae.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amefanya ziara ya kustukiza katika hospitali ya Rufaa ya wazazi Meta ya jijini Mbeya na kushuhudia msongamano mkubwa wa akina mama wajawazito hospitalini hapo, na alipofika katika chumba cha akina mama ambao wanasubiri watoto wao ambao wamewekwa katika chumba maalum cha joto, ndipo akakutanana na malalamiko ya mama Salome Waya ambaye amedai kupigwa na muuguzi wakati akijifungua.
Kufuatia madai hayo, mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akalazimika kupitia nyaraka za mama huyo ili kumtambua muuguzi aliyemfanyia ukatili huo na akafanikiwa kumbaini kuwa anaitwa Beatrice Sanga ndipo akatoa agizo kwa mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya kanda ya nyanda za juu kusini, Dk. Goodlove Mbwanji kufanya uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya muuguzi huyo ndani ya siku saba.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk. Goodlove Mbwaji amesema kuwa katika mazingira hayo hawezi kujitetea na badala yake atazingatia maelekezo ambayo amepewa na mkuu wa mkoa.