Muuaji wa padri afutiwa mashitaka

Muuaji wa padri afutiwa mashitaka

Bwana Mapesa

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
2,551
Reaction score
1,777
MUUAJI WA PADRI MUSHI AFUTIWA MASHITAKA


Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim, ametupilia mbali uchunguzi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na kusema mtuhumiwa hana kesi ya kujibu mahakamani.

Padri Mushi ambaye alikuwa Paroko wa Kanisa Katoliki Minara Miwili aliuawa kwa kupigwa risasi Febuari 17, mwaka huu katika eneo la Beitrasi mjini hapa akiwa ndani ya gari alipokuwa akielekea kuongoza misa ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Theresia, mjini Zanzibar.
Baada ya mauaji hayo, Rais Jakaya Kikwete alitoa kibali cha kukaribisha maafisa wa FBI kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa mauaji hayo na Machi 17, mwaka huu Jeshi la Polisi lilimkamata Omar Mussa Makame kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
Uchunguzi wa NIPASHE umebaini kuwa DPP baada ya kulipitia jalada la uchunguzi wa mauaji hayo, juzi alitoa mwongozo kwa Jeshi la Polisi kuendelea kumtafuta muuaji wa Padri Mushi.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, DPP aliliandikia barua Jeshi la Polisi na kukabidhiwa juzi ikieleza sababu za ofisi yake kutofungua hati ya mashtaka hadi sasa dhidi ya mtuhumiwa wa mauaji hayo.
Jeshi la Polisi limethibitisha kuipokea barua ya DPP ambayo inaeleza kuwa ushahidi uliokusanywa katika jalada la kesi hiyo hauna mashiko na kwamba mtuhumiwa hahusiki na mauaji hayo.
Chanzo cha habari kutoka Jeshi la Polisi kilieleza kuwa DPP hajaridhishwa na uchunguzi wote uliokusanywa dhidi ya mtuhumiwa pamoja na watuhumiwa watatu wanaotuhumiwa kwa mauaji ya askari polisi, Said Abdulrahman aliyeuawa kwa kupigwa mapanga na watu wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar Oktoba 17, mwaka jana.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alithibitisha hatua ya DPP kutupa uchunguzi wote wa jalada la mauaji ya Padri Mushi na kuwataka waandishi wa habari kumtafuta DPP azungumzie sababu za uamuzi wake wa kutokubaliana na uchunguzi wa Polisi.
Hata hivyo, alisema kwamba Jeshi la Polisi bado linaamini uchunguzi walioufanya kwa kushirikiana na FBI hauna shaka na kwamba mtuhumiwa huyo ana kesi ya kujibu mahakamani na wataendelea kumshikilia.
Alisema kwamba kwa mujibu wa sheria, Jeshi la Polisi jukumu lake ni kuchunguza kesi na ofisi ya DPP jukumu lake ni kufungua hati ya mashtaka na kutetea kesi mahakamani.
Hata hivyo, NIPASHE ilipofika katika ofisi ya DPP, Katibu muhtasi wake alisema amepokea maagizo kutoka kwa bosi wake kuwa waandishi wote wa habari wanaofuatilia suala hilo, wamuone Kamishna wa Polisi kwa vile kazi aliyopewa ya kupitia jalada la uchunguzi kabla ya kufungua kesi ameikamilisha.
“Kamishna ndiye aliyeitisha mkutano na waandishi wa habari kuelezea hatua iliyofikiwa pamoja na kukamatwa kwa mtuhumiwa, sasa awaite tena amalizie kazi yake ya kuwaeleza hatua iliyofikiwa baada ya Mkurugenzi kurejesha jalada la mauaji,” alisema Katibu muhtasi huyo.
Katika hatua nyingine, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Yusuph Ilembo, jana alifika katika Mahakama Kuu ya Zanzibar, kufuatia ombi lililofunguliwa mahakamani na wakili anayemtetea mtuhumiwa wa mauaji, Abdallah Juma Mohamed.
Abdallah Juma amefungua ombi katika Mahakama Kuu kwa kutumia kifungu cha sheria 390 cha sheria namba 7 ya mwenendo wa makosa ya jinai ya mwaka 2004, akitaka Jeshi la Polisi litoe maelezo kwa nini mteja wake hajafikishwa mahakamani ndani ya saa 24 tangu alipokamatwa Machi 17, mwaka huu.
Wakili Abdallah Juma akisaidiwa na mawakili Shaban Juma Bakari na Shaibu Ibrahim Shaibu waliitaka Mahakama Kuu itoe amri ya kuachiwa kwa mteja wao kutoka mikononi mwa Jeshi la Polisi. Hata hivyo, Ilembo alisema kuwa kutokana na uzito wa kesi hiyo, anaomba kupewa muda wa kutayarisha majibu ya hati ya kiapo kwa maandishi na kuuwasilisha kwa upande wa utetezi na mbele ya mahakama hiyo kabla ya ombi hilo kuanza kusikilizwa na kutolewa uamuzi.
“Tunaomba mtuhumiwa aendelee kushikiliwa na Polisi, wakati tukifanya matayarisho ya kujibu hati ya kiapo,” alisema Ilembo.
Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu, Mkusa Isaack Sepetu, alisema baada ya kusikiliza pande zote mbili, alimtaka Ilembo awe amejibu kwa maandishi hati ya kiapo ya maombi hayo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo Aprili 8, mwaka huu.
Aidha, Jaji alisema wakati wa kusikilizwa kwa shauri hilo, ametaka mtuhumiwa huyo afikishwe mahakamani, baada ya hoja za upande wa mawakili wanaomtetea kutaka dhamana kwa mteja wao, kwa vile bado hajafikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.
Kutupwa kwa uchunguzi wa jalada la mauaji hayo pamoja na jalada la uchunguzi wa mauaji ya Polisi kunadhihirisha kuwapo kwa mvutano mkubwa baina ya Jeshi la Polisi Zanzibar na ofisi ya DPP.

MPEKUZI at 8:09 PM
 
Sishangai DPP kuona hakuna ushahidi wa kutosha kumfungulia mashataka mtuhumiwa. Hii inatokana na udhaifu ktk idara ya upelezi polisi katika swala zima la kukusanya ushahidi wa kutosha. kesi yoyote inajengwa kwa ushahidi imara na unaojitosheleza hasa kwenge kesi za jinai ambapo kanuni ya " proof beyond reasonable doubt" hutumiwa.
 
Juzi tu mkuu wa kaya katoka kuwahadaa watu kuwa muuaji kapatikana kwa juhudi za polisi na FBI!!

Ila hili nalo ni upepo, litapita..!
 
Huwezi ku frame kesi kwa ku attach katuni ya mtuhumiwa bila ya kuwa na uthibitisho beyond reasonable doubt kuwa anahusika.DPP hongera kwa kukataa ku Politisize proffession!
 
Huyu hakufutiwa kesi. Kesi yenyewe haikuwahi kuwepo. Kulikuwa na malalamiko na tuhuma tu. DPP hakuwahi kupeleka kesi Mahakamani ambayo ingeweza kufutwa. Hivyobasi,si weledi kusema 'amefutiwa kesi/amefutiwa mashtaka'.
 
Huwezi ku frame kesi kwa ku attach katuni ya mtuhumiwa bila ya kuwa na uthibitisho beyond reasonable doubt kuwa anahusika.DPP hongera kwa kukataa ku Politisize proffession!

ushahidi wao ni mzuri ila siyo convicing ulikuwa unahitaj colaboration.so wanakaz ya kutafuta ushahid wa kueleweka..siyo katuni na politricks..
 
Sishangai DPP kuona hakuna ushahidi wa kutosha kumfungulia mashataka mtuhumiwa. Hii inatokana na udhaifu ktk idara ya upelezi polisi katika swala zima la kukusanya ushahidi wa kutosha. kesi yoyote inajengwa kwa ushahidi imara na unaojitosheleza hasa kwenge kesi za jinai ambapo kanuni ya " proof beyond reasonable doubt" hutumiwa.

Mkuu uko nchi gani??

TAnzania tunatumia proof based on political affiliation
 
Sishangai DPP kuona hakuna ushahidi wa kutosha kumfungulia mashataka mtuhumiwa. Hii inatokana na udhaifu ktk idara ya upelezi polisi katika swala zima la kukusanya ushahidi wa kutosha. kesi yoyote inajengwa kwa ushahidi imara na unaojitosheleza hasa kwenge kesi za jinai ambapo kanuni ya " proof beyond reasonable doubt" hutumiwa.

Mimi huwa siamini sana ushahidi wa picha ya kuchora. Mara nyingi wachoraji huchora kwa kuulizauliza wapo mwonekano wa mtu anayeshukiwa. Sasa tatizo laweza tokea kwenye mchoro maana unategemea sana maelezo ya shuhuda. Kwa mfano mchoraji akapewa maelezo kisha akachora picha inayofanana na DPP hapo itakuwaje????
 
Sishangai DPP kuona hakuna ushahidi wa kutosha kumfungulia mashataka mtuhumiwa. Hii inatokana na udhaifu ktk idara ya upelezi polisi katika swala zima la kukusanya ushahidi wa kutosha. kesi yoyote inajengwa kwa ushahidi imara na unaojitosheleza hasa kwenge kesi za jinai ambapo kanuni ya " proof beyond reasonable doubt" hutumiwa.

Usiwashtumu Polisi Tu ., na hao FB mbona huwatupi lawama kwa kusaspect mtu ambaye sio.?
 
Lakini vitu vingine tunavikuza sisi wenyewe.
Yule aliyekamtwa ni mtuhumiwa tuu mpaka mahakama itakapo mkuta na hatia.
Sasa mtu anapoleta heading 'Muuaji wa Padri afutiwa mashitaka' kwa kweli tunatumia keybords zetu vibaya.
 
MUUAJI WA PADRI MUSHI AFUTIWA MASHITAKA


Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim, ametupilia mbali uchunguzi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na kusema mtuhumiwa hana kesi ya kujibu mahakamani.

Padri Mushi ambaye alikuwa Paroko wa Kanisa Katoliki Minara Miwili aliuawa kwa kupigwa risasi Febuari 17, mwaka huu katika eneo la Beitrasi mjini hapa akiwa ndani ya gari alipokuwa akielekea kuongoza misa ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Theresia, mjini Zanzibar.
Baada ya mauaji hayo, Rais Jakaya Kikwete alitoa kibali cha kukaribisha maafisa wa FBI kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa mauaji hayo na Machi 17, mwaka huu Jeshi la Polisi lilimkamata Omar Mussa Makame kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
Uchunguzi wa NIPASHE umebaini kuwa DPP baada ya kulipitia jalada la uchunguzi wa mauaji hayo, juzi alitoa mwongozo kwa Jeshi la Polisi kuendelea kumtafuta muuaji wa Padri Mushi.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, DPP aliliandikia barua Jeshi la Polisi na kukabidhiwa juzi ikieleza sababu za ofisi yake kutofungua hati ya mashtaka hadi sasa dhidi ya mtuhumiwa wa mauaji hayo.
Jeshi la Polisi limethibitisha kuipokea barua ya DPP ambayo inaeleza kuwa ushahidi uliokusanywa katika jalada la kesi hiyo hauna mashiko na kwamba mtuhumiwa hahusiki na mauaji hayo.
Chanzo cha habari kutoka Jeshi la Polisi kilieleza kuwa DPP hajaridhishwa na uchunguzi wote uliokusanywa dhidi ya mtuhumiwa pamoja na watuhumiwa watatu wanaotuhumiwa kwa mauaji ya askari polisi, Said Abdulrahman aliyeuawa kwa kupigwa mapanga na watu wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar Oktoba 17, mwaka jana.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alithibitisha hatua ya DPP kutupa uchunguzi wote wa jalada la mauaji ya Padri Mushi na kuwataka waandishi wa habari kumtafuta DPP azungumzie sababu za uamuzi wake wa kutokubaliana na uchunguzi wa Polisi.
Hata hivyo, alisema kwamba Jeshi la Polisi bado linaamini uchunguzi walioufanya kwa kushirikiana na FBI hauna shaka na kwamba mtuhumiwa huyo ana kesi ya kujibu mahakamani na wataendelea kumshikilia.
Alisema kwamba kwa mujibu wa sheria, Jeshi la Polisi jukumu lake ni kuchunguza kesi na ofisi ya DPP jukumu lake ni kufungua hati ya mashtaka na kutetea kesi mahakamani.
Hata hivyo, NIPASHE ilipofika katika ofisi ya DPP, Katibu muhtasi wake alisema amepokea maagizo kutoka kwa bosi wake kuwa waandishi wote wa habari wanaofuatilia suala hilo, wamuone Kamishna wa Polisi kwa vile kazi aliyopewa ya kupitia jalada la uchunguzi kabla ya kufungua kesi ameikamilisha.
“Kamishna ndiye aliyeitisha mkutano na waandishi wa habari kuelezea hatua iliyofikiwa pamoja na kukamatwa kwa mtuhumiwa, sasa awaite tena amalizie kazi yake ya kuwaeleza hatua iliyofikiwa baada ya Mkurugenzi kurejesha jalada la mauaji,” alisema Katibu muhtasi huyo.
Katika hatua nyingine, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Yusuph Ilembo, jana alifika katika Mahakama Kuu ya Zanzibar, kufuatia ombi lililofunguliwa mahakamani na wakili anayemtetea mtuhumiwa wa mauaji, Abdallah Juma Mohamed.
Abdallah Juma amefungua ombi katika Mahakama Kuu kwa kutumia kifungu cha sheria 390 cha sheria namba 7 ya mwenendo wa makosa ya jinai ya mwaka 2004, akitaka Jeshi la Polisi litoe maelezo kwa nini mteja wake hajafikishwa mahakamani ndani ya saa 24 tangu alipokamatwa Machi 17, mwaka huu.
Wakili Abdallah Juma akisaidiwa na mawakili Shaban Juma Bakari na Shaibu Ibrahim Shaibu waliitaka Mahakama Kuu itoe amri ya kuachiwa kwa mteja wao kutoka mikononi mwa Jeshi la Polisi. Hata hivyo, Ilembo alisema kuwa kutokana na uzito wa kesi hiyo, anaomba kupewa muda wa kutayarisha majibu ya hati ya kiapo kwa maandishi na kuuwasilisha kwa upande wa utetezi na mbele ya mahakama hiyo kabla ya ombi hilo kuanza kusikilizwa na kutolewa uamuzi.
“Tunaomba mtuhumiwa aendelee kushikiliwa na Polisi, wakati tukifanya matayarisho ya kujibu hati ya kiapo,” alisema Ilembo.
Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu, Mkusa Isaack Sepetu, alisema baada ya kusikiliza pande zote mbili, alimtaka Ilembo awe amejibu kwa maandishi hati ya kiapo ya maombi hayo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo Aprili 8, mwaka huu.
Aidha, Jaji alisema wakati wa kusikilizwa kwa shauri hilo, ametaka mtuhumiwa huyo afikishwe mahakamani, baada ya hoja za upande wa mawakili wanaomtetea kutaka dhamana kwa mteja wao, kwa vile bado hajafikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.
Kutupwa kwa uchunguzi wa jalada la mauaji hayo pamoja na jalada la uchunguzi wa mauaji ya Polisi kunadhihirisha kuwapo kwa mvutano mkubwa baina ya Jeshi la Polisi Zanzibar na ofisi ya DPP.

MPEKUZI at 8:09 PM

Huyu muuaji si alitambuliwa katika gwaride mbili tofauti? Kama ataachiwa itakuwa ni kile Maaskofu wameita a 'Systematic Persecution of the Tanzanian Church'.
 
Shida ya zenj ni swala la muungano tu,mkitaka msiyasikie haya ni kupigania juu ya muungano hewa kuvunjika hati ya muungano wenyewe hakuna ila kuna picha tu ya vyungu na wanaume wawili wakibadilishana michanga yaani nguvu za giza (uchawi)ndio unao linda muungano.zanzibar ni nch inayo takiwa iongozwe kidini kwani 99% ni waislamu na 1%ni wa kristo wakishisikiana na wapagani,leo tanganyika yetu haipo wakati uhuru tulio upata mwaka 61 ni wa tanganyika!!wakija kununua mahindi maharage mchele nk hua hawaombwi kibali lakini wewe nenda kanunue tv jokofu gari nk tuone kama hakuna kibali utakacho toa.zanzibar ninch ya kiislamu na wakoloni wao ni waarabu.waachieni nch yao muone kama haya yanayo tokea kama yataendelea.mnashughulika na majani wakati chanzo kiko kwenye mizizi!! Mnaelewa ila mnajifanya hamfahamu.fungukeni.hapa kwetu bara mbona chenge amewahi kuua watu wawili lakini alitna faini ya laki 7 nale yuko huru na nimwenyekiti wa kamati bungeni kule kunako wakirisha wana nch woote wa tz.yukuwapi zombe?salimu alii alitoa m7 kwa kosa la kuuza watu huko uarabuni magereza ni yawanyonge tu.
 
Tatizo la idara ya upelelezi katika kukusanya ushaidi siyo kwenye issue hii tu. Ni tatizo la kimfumo na weledi. DPP anatathmini ushahidi ulioletwa kabla ya kufungua mashataka kam ni dhaifu ana haja gani ya kufungua mashtaka. hapa hakuna swala la siasa wala utanganyika.
 
Shida ya zenj ni swala la muungano tu,mkitaka msiyasikie haya ni kupigania juu ya muungano hewa kuvunjika hati ya muungano wenyewe hakuna ila kuna picha tu ya vyungu na wanaume wawili wakibadilishana michanga yaani nguvu za giza (uchawi)ndio unao linda muungano.zanzibar ni nch inayo takiwa iongozwe kidini kwani 99% ni waislamu na 1%ni wa kristo wakishisikiana na wapagani,leo tanganyika yetu haipo wakati uhuru tulio upata mwaka 61 ni wa tanganyika!!wakija kununua mahindi maharage mchele nk hua hawaombwi kibali lakini wewe nenda kanunue tv jokofu gari nk tuone kama hakuna kibali utakacho toa.zanzibar ninch ya kiislamu na wakoloni wao ni waarabu.waachieni nch yao muone kama haya yanayo tokea kama yataendelea.mnashughulika na majani wakati chanzo kiko kwenye mizizi!! Mnaelewa ila mnajifanya hamfahamu.fungukeni.hapa kwetu bara mbona chenge amewahi kuua watu wawili lakini alitna faini ya laki 7 nale yuko huru na nimwenyekiti wa kamati bungeni kule kunako wakirisha wana nch woote wa tz.yukuwapi zombe?salimu alii alitoa m7 kwa kosa la kuuza watu huko uarabuni magereza ni yawanyonge tu.

Hongera mkuu,nadhani umetumia darubini kali kwenye hii issue,watanganyika wengi hawajui ccm inavyo tawala hapa tanzania na pia hawafamu vizuri neno mapinduzi daima.
 
Juzi tu mkuu wa kaya katoka kuwahadaa watu kuwa muuaji kapatikana kwa juhudi za polisi na FBI!!

Ila hili nalo ni upepo, litapita..!

kaka nchi hii haina mkuu wa kaya ina kivuli tu kinachoonekana pale magogoni.cjui aliyesema amekamatwa na Fbi ni huyu au kuna mwingine.
 
Hii njemba ina bahati kubwa sana. Polisimagamba walitaka kumharibia maisha yake kwa kumbambikia kesi. Amshukuru sana Mola wake angeozea lupango.
 
Back
Top Bottom