Mutungi: Vyama vya Siasa visisusie uchaguzi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,858
Hiyo ni kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Mtungi kama ilivyonukuliwa katika gazeti la Uhuru la siku ya leo.

Chanzo:Uhuru

Swali langu ni je,uchaguzi ulivyofutwa huko Zanzibar,msajili alitoa kauli gani juu ya uamuzi huo?

Msajili huyu aliwahi hata kushauriana na viongozi wa vyama hivi juu ya nini cha kufanya baada ya uchaguzi kufutwa?
 
Uchaguzi ulifutwa kwa makosa (kama yalikuwepo) yaliyokua kwenye tume ya ZEC, sio vyama. Leo hii tume ni ile ile iliyoharibu uchaguzi inaitisha uchaguzi mpya, huu ni zaidi ya ujuha.

Ujinga ni kuendelea kurudia uchaguzi kwa tume ile ile ukitegemea uchaguzi huo utakua tofauti
(Derived from Albert Einstein's speech)
 
Jaji hajawahi zungumza lolote tangu uchaguzi ulipofutwa. Je ameona nini mpaka anaamua kuwaambia wa vyama vya upinzani wasisusie uchaguzi ?
 
Huu ni uchaguzi wa aina yake unaofanyika bila kampeni na wagombea wanatakiwa kuwa walewale waiogombea Octoba 25, Je, endapo CUF wataendelea kushikilia msimamo wao wa kususia uchaguzi wa marudio ni nini kitatokea?
 
Uchaguzi wa zanzinbar upo chini ya ZEC, NEC haina mamlaka, msajili wa vyama vya siasa anasemea pande zote, Rais magufuli hana Mamlaka kusemea uchaguzi wa zanzibar, huu muungano una ukakasi sana. Lubuva kimya, kamaliza yake, Jecha anapata support ya mutungi, akhaaa.
 
Nilijua mngetumia ubavu kuhalalisha Shein aendelee kutawala kwa miaka mitano ijayo badala yake mnakuja na uchaguzi ambao ni upuuzi tu wa kupoteza hela na muda ,hata wakisusia sioni tatizo mlishasema serikali ya Zanzibar haibadilishwi kwa vijakaratasi vya kura
 
Mhhh ninawasiwasi na taaluma ya jaji mtungi kweli anasimamia haki huyu yeye ilikuwa wa kwanza kuwashawishi ccm kukubali matokeo Leo anaviomba vyama vya sasa kutokususia uchaguzi ccm B
 
Mhhh ninawasiwasi na taaluma ya jaji mtungi kweli anasimamia haki huyu yeye ilikuwa wa kwanza kuwashawishi ccm kukubali matokeo Leo anaviomba vyama vya sasa kutokususia uchaguzi ccm B
Ukishakua mwanasiasa Taaluma ni jambo la kipuuzi tu ,usishangae nae ni mwanachama wa ccm ,kama ilivyokua kwa jaji Augustino Ramadhani
 
Lililo tokea Zbr hakuna asiye jua ukweli wake, lime onyesha wazi vyama vya upinzani havina nafasi hivyo kama vyama vitaamua kuto shiriki uchaguzi sito shangaa wala kuwalaumu
 
sio usishangae...hio ndio hali halisi
Mkuu kama tuliweza kufaulisha watoto wasiojua kusoma na kuandika kwenda sekondari ,hili la Mtungi halinishangazi Mkuu kama liliwezekana kwa Tulia na Jaji Ramadhani basi ni dhahiri hakuna lisolowezekana kwa serikali ya Tanzania
 
Hiyo ni kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Mtungi kama ilivyonukuliwa katika gazeti la Uhuru la siku ya leo.

Chanzo:Uhuru

Swali langu ni je,uchaguzi ulivyofutwa huko Zanzibar,msajili alitoa kauli gani juu ya uamuzi huo?

Msajili huyu aliwahi hata kushauriana na viongozi wa vyama hivi juu ya nini cha kufanya baada ya uchaguzi kufutwa?
Huyo Msajili wa vyama vya siasa ni mpuuzi kupindukia na kutokana na kauli yake hiyo amedhibitisha waziwazii kuwa na yeye ni kada wa CCM.

Huyo Msajili anajua wazi kuwa Jecha hakuwa na mamlaka ya kuufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar, kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na sheria ya uchaguzi ya Zanzibar.

Hivi Hhuyo Msajili anawezaje kuhalalisha 'haramu' ya kurejewa uchaguzi wakati anajua wazi kuwa hakuna chama chochote kilichotumia utaratibu wa kisheria wa kuulalamikia uchaguzi huo?

Hivi huyo Msajili wa vyama anawezaje kubariki 'uharamia' wa kurejewa uchaguzi wote wakati anajua waangalizi wote wa ndani na nje ya nchi walioushuhudia uchaguzi huo walitoa taarifa zao na kusema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki?

Hivi huyo anayeitwa Jaji Mutungi anawezaje kuona ni halali uchaguzi huo wote kurejewa, wakati anajua hata washindi wa nafasi za uwakilishi walikabidhiwa vyeti vyao vya ushindi?

Kinachoonekana ni kuwa ukitaka kuwa mteule kwa nafasi za juu ndani ya serikali ya CCM ni lazima ukubaliane na 'condition' kubwa inayoambatana na uteuzi huo wa kuweka 'rehani' taaluma yako, kama alivyotekeleza Jaji huyo, kwa kuweka rehani taaluma yake ya sheria pale mtaa wa Lumumba!
 
Back
Top Bottom