Muswada wa vyama vya siasa, 2018

Mtetezi_Paul_Kisabo

New Member
Jan 3, 2019
4
1
Hello ndugu mpenda haki za binadamu na mwanademokrasia nakusalimu sana.

Nakutaarifu kuwa leo Januari 3, 2019 nimefanya tafsiri isiyo rasmi ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama Vya Siasa uliotolewa Bungeni Jijini Dodoma Oktoba 15, 2018.

Muswada huu kwa maoni yangu kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mbovu haijawahi kutokea katika nchi yetu.

Binafsi ninaupinga kwasababu nyingi sana, naomba nitaje kadhaa

1. Muswada huu endapo utapitishwa kuwa sheria unampa msajili mamlaka ya kifalme. Nina imani kila mmoja anafaham mamlaka ya kifalme.

2. Muswada huu ni kanadamizi dhidi ya haki ya faragha ya vyama vya siasa kinyume na ibara ya 15 ya katiba ya JMT 1977.

3. Muswada huu ni kandamizi dhidi ya haki za kisiasa, kumbuka haki za kisiasa ni haki za binadamu. Mfano msajili ana mamlaka ya kufuta usajili wa chama cha siasa, kumfukuza uanachama mwanachama yoyote wa chama cha siasa na ana mamlaka ya kuomba na kupewa taarifa yoyote ile ya chama cha siasa.

4. Muswada huu ni adui namba moja wa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania.

Paul Kisabo
Mwanasheria
Januari 3, 2019View attachment Muswada wa Vyama vya Siasa 2018.pdf

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom