Mkuu hili fao kwenye social security industry hakunaga, sema tu liliwekwa kama kuvutia wateja ndo maana wanataka walete unemployment benefit, once ukiingia kwenye social security scheme huwezi kutoka unless ukathibitika una ulemavu wa kudumu ambao hutoweza kujipatia kipato tena kwenye maisha yako, hapo ndo benefit zingine zitachukua mkondo wake ila fao la kujitoa hiyo kitu hakunaFao la kujitoa
Section 4 & 6 inaanzisha mfuko mpya, unaitwa Public Service Social Security Fund. (PSSSF)
Section 77 Inafuta mifuko yote ilokuwepo ispokua NSSF.
S.81 Hata Voluntary Schemes za mifuko ilofutwa zinahamia kwenye mfuko mpya.
S. 80 & 87 Watumishi wote wa Umma mfuko wao utakua huu mpya, hivyo walokua wanachama wa NSSF nao watahamishiwa huko.
Licha kuhamishwa, pesa / michango hazita hamishwa, ispokua Authority itakuja na formula ya kukokotoa stahiki zao (portability of benefits)
Vifungu kuanzia 90 hadi 105 vinazungumzia mabadiliko ktk NSSF
S. 92 (b) & 93 (a) Members wote wa private waliokua kwenye hiyo mifuko wanarudi NSSF,
S. 96 Ina futa Employment Injury Benefit na SHIB na kuweka Unemployment benefit tu kama fao jipya,, waziri ataleta kanuni za unemployment benefits,
Hawa sijui kama ni watanzani!Ndio mwanzo wa kupotea michango ya wafanyakazi, sasa wanaweka mfuko mmoja ili iwe rahisi kuchota. Hawa viumbe tuliowaweka madarakani nahisi sio Watanzania.
Hawa watu sijui wakoje? LAPF na PSPF ilikuwa mifuko mizuri sana. Sasa serikali imeona tunafaidi imekuja na mpango wa kudhurumu watu wake? Siamini ninachokiona!Old members wa PSPF na LAPF daaaah mkiangukia kwenye harmonization formula watakuwa wamewakatili sana, ila you have to obey the rule
Umenena vema Mkuu, lakini pia ilikua ikishindana kutoa Bonus kwa watumishi mf. fao la Uzazi, Malipo ya kianzio cha maisha kwa ajira Mpya, Piga kitabu, Mikopo ya Viwanja nk nk. Hii yote ilikuwa ni kwa ajili ya Ushindani wa kibiashara. Lakini wakiiunganisha ndio kifo cha mende kama TTCL maana hawana mshindani. OOooooooh God!Hawa watu sijui wakoje? LAPF na PSPF ilikuwa mifuko mizuri sana. Sasa serikali imeona tunafaidi imekuja na mpango wa kudhurumu watu wake? Siamini ninachokiona!
hapa watakuwa hawajatenda haki! formula mpya zianze kwa wapya! wastuletee za kuletaOld members wa PSPF na LAPF daaaah mkiangukia kwenye harmonization formula watakuwa wamewakatili sana, ila you have to obey the rule
Kufa kwa shirika la hifadhi ya jamii ni ngumu sana, ila ndo hivyo watakuwa monopoly hata utoaji wa huduma utakuwa mbovu na kwakuwa kwa formal employed person ni compulsory kujiunga na social security scheme hawatakuwa na haja ya kubembeleza members yaani mfano mzuri tanesco huwez kuta wanabembeleza wateja kwa matangazo eti tunatoa umeme kwa bei nzuri, we utake usitake.Umenena vema Mkuu, lakini pia ilikua ikishindana kutoa Bonus kwa watumishi mf. fao la Uzazi, Malipo ya kianzio cha maisha kwa ajira Mpya, Piga kitabu, Mikopo ya Viwanja nk nk. Hii yote ilikuwa ni kwa ajili ya Ushindani wa kibiashara. Lakini wakiiunganisha ndio kifo cha mende kama TTCL maana hawana mshindani. OOooooooh God!