Muswada wa Katiba waongezewa muda...

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
majadiliano ya mwaada wa katiba ulikuwa uishe leo, lakini umeongezewa mda tena. Kama tunavyojua Bunge hili linategemewa kuhitimishwa ijumaa hii. Bado haijajulikana mkataba wa katiba utahitimishwa lini.
chanzo ni startv inayorusha matangazo live kutoka Bungeni.
mia
 
Aiseee... wameongeza muda wa kupiga mipasho na matusi? jamani wabunge kumbukeni ni kodi zetu hizo mnazitumia kupashana na matusi yasiyokua na tija! inatia kinyaa sana yanayoendelea bungeni dodoma kwa sasa, bunge limekua kama uwanja wa fisi manzese, ccm huu ulafi wa madaraka na ubabe utawatokea puani siku si nyingi.. mmeleta mswada mnaoutaka nyinyi mmeachiwa bunge muujadili badala ya kuujadili mmebaki kutoa matusi na vijembe kwa Chadema na nccr tu, kwani lazima muujadili na cdm wakiwepo?
 
Wanataka wajaribu kuwashawishi CDm waingie ndani ya bunge kwani wamekosa point za kuingiza kwenye mswaada . Zito, kabwe , Mnyika hawamo kwa hiyo wanapata kigugumizi cha nini kifanyike. Maana magamba yote baada ya kuchangia mswaada yamejkita kuishambulia Chadema ili hali yanajua kuwa mipasho hiyo haiwezi kuingizwa kwenye mswaada.
 
Sasa hivi hawachangii katiba bali wanaizungumzia CHADEMA tu, wabunge wa CCM hamna kitu wote ni Vilaza tuu

Hawajawahi kua na chochote cha kuongea.. inaonekana wanawamiss sana chadema manake bila chadema kuwemo hamna kinachoongelewa tena
 
majadiliano ya mwaada wa katiba ulikuwa uishe leo, lakini umeongezewa mda tena. Kama tunavyojua Bunge hili linategemewa kuhitimishwa ijumaa hii. Bado haijajulikana mkataba wa katiba utahitimishwa lini.
chanzo ni startv inayorusha matangazo live kutoka Bungeni.
mia
Kama tunadai nchi yetu ni ya kidemokrasia na bunge letu ni la kidemokrasia huwezi kupitisha kitu muhimu kama katiba bila kuungwa mkono na chama kikuu cha upinzani hata mataifa yatatushangaa, majirani zetu Kenya mbali ya kutofautiana na kuuana lakini walirudisha akili na kukaa pamoja kwa suala muhimu la katiba, tuchezee sheria na kanuni zingine lakini si katiba. Hongera Chadema kwa kuwa na msimamo usioyumba.
 
Aiseee... wameongeza muda wa kupiga mipasho na matusi? jamani wabunge kumbukeni ni kodi zetu hizo mnazitumia kupashana na matusi yasiyokua na tija! inatia kinyaa sana yanayoendelea bungeni dodoma kwa sasa, bunge limekua kama uwanja wa fisi manzese, ccm huu ulafi wa madaraka na ubabe utawatokea puani siku si nyingi.. mmeleta mswada mnaoutaka nyinyi mmeachiwa bunge muujadili badala ya kuujadili mmebaki kutoa matusi na vijembe kwa Chadema na nccr tu, kwani lazima muujadili na cdm wakiwepo?
Sasa ndio wameanza kujua nguvu ya wabunge 23 waliokuwa wanawabeza, si wapitishe sasa kwa vile wao wako wengi?
 
Haya maghamba bwana Si yamalize tu utumbo wao huu! Mimi naudhika kweli!
 
majadiliano ya mwaada wa katiba ulikuwa uishe leo, lakini umeongezewa mda tena. Kama tunavyojua Bunge hili linategemewa kuhitimishwa ijumaa hii. Bado haijajulikana mkataba wa katiba utahitimishwa lini.
chanzo ni startv inayorusha matangazo live kutoka Bungeni.
mia

Mpaka Chadema watoe michango yao!
 
Historia imeisha watupa mkono CCM lakini kama kawaida tawala zote zinazokaribia mwisho/kifo huwa hazina uwezo wa kuona wala kusikia! Bado najiuliza kama kweli Kikwete alikua anataka tumkumbuke kwa Katiba Mpya kwanini ameruhusu watu bogus toka serikalini na ndani ya chama chake wavuruge huu mchakato?!!!
 
Suala la KATIBA MPYA KWA NJIA YA BARAZA LA TAIFA LILILOUNDWA NA SISI WANANCHI WENYEWE ni bomu hatari ambalo laweza kulipuka wakati wowote nchini endapo watu hawaisha utani na jambo hili.

KATIKA HILI LA KATIBA KWA NJIA LA KUSIMAMIWA NA WANANCHI WENYEWE KWA HATUA ZOTE na wala si kusimamiwa na mtu yeyote ambaye ni mtumishi wetu serikalini - sote tunasema kwa pamoja mjiandae kutuua SOTE kwa kuwa hatuna lingine tena kwa sikio lisilosikiliza hili!!!
 
Historia imeisha watupa mkono CCM lakini kama kawaida tawala zote zinazokaribia mwisho/kifo huwa hazina uwezo wa kuona wala kusikia! Bado najiuliza kama kweli Kikwete alikua anataka tumkumbuke kwa Katiba Mpya kwanini ameruhusu watu bogus toka serikalini na ndani ya chama chake wavuruge huu mchakato?!!!

Safi sana mkuu. KIFO CHA CCM KIPO JIRANI.
 
CCM inapambana na wananchi badala ya kupambana na wapinzani wao. CCM inatakiwa ishauriwe kwamba ni heri ife kifo chema kuliko kufa vibaya maana kifio chake sasa hakiepukiki.
 
Back
Top Bottom