Muswada wa Katiba:CHADEMA KUINGIA MTEGO WA CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muswada wa Katiba:CHADEMA KUINGIA MTEGO WA CCM?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Jatropha, Apr 6, 2011.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  kwa jinsi ambavyo Muswada wa Katiba uliosomwa kwa mara ya kwanza bungeni jana tara 05 Aprili 2011 ulivyokuwa na mapungufu makubwa ikiashiria kuwa upo mzaha katika maandalizi yake. Hali hii inashiria jambo moja tu, nalo ni kuwa CCM inataka kudivert attention ya watu makini katika vyama vya upinzania hususana CHADEMA ili wajishughulishe na mchakato wa Katiba na kusahau kabisa ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais 2010.

  Watu wasisahau kuw CCM ina uzoefu mkubwa wa kucheza na akili za binadamu, na inafahamu fika kuwa watanzania wengi ikiwemo idadi kubwa ya wanaojiita wasomi sasa hawajui tofauti kati ya Muswada wa kuandaa mchakato wa kupitia Katiba uliosomwa bungeni na mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya, ambao imekuwa ikidaiwa kwa muda mrefu sana.

  Hivyo wananchi walio wengi wanaona na kuridhika kuwa tayari Serikali inatekeleza matakwa na madai upinzani ya kutaka mabadiliko ya Katiba. Hivo jitihada zozote za kuweka shinikizo zaidi kwa njia ya mandamano n.k zinaweza kutafsiriwa kama fujo na machafuko. Tusisahau CCM walivyo wazuri kutumia misamiati hiyo hususan pale wananchi watakapoanza kushuhudia machungu ya hali hizo. Ikumbukwe kuwa watanzania hawajakomaa kiasi cha kuwa tayari kujitolea kama nchi tunazoona wakishiriki katika kudai haki kwa maandamano n.k

  CHADEMA inatakiwa kuhakikisha kuwa haizami moja kwa moja katika malumbano ya Katiba pekee na kusahau mambo mengine ya kitaifa kama vile kufuatilia na kufanya tathmni za kina kuhusu utekelezwaji wa ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni; kuwambusha wananchi mara ka mara kuhusu kiwango cha utekelezwaji wake na kujikita zaidi katika kukijenga chama kutoka ngazi ya taifa kilipo sasa kushuka chini hadi ngazi za mashina, kufungu matawi na kuiingiza idadi kubwa ya wananchama shughuli ambazo mpaka sasa hazionekani kuptiwa uzito wa kutosha.
   
 2. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180

  Jatropha, Mawazo yako yaweza kuwa kweli, haiwezekani wasomi, watu wazima walio na watoto na vijukuu, na akili zao timamu wakiwa na afya njema kimwili na kiakili walete mswaada mbovu kama ule mbele ya wawakilishi wa wanainchi kwa macho makavu tena mekundu kama wamama wa usukumani wanaodhaniwaga kuwa ni wachawi...hakika naamini hawa si wajinga kiasi hicho kama mswaada ulivyo bali kuna kitu ndani yake bado hatujakiona...tuendelee kutafakari kwa umakini ndipo tutakijua!
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu umesema kweli tupu na nadhani umeisoma vizuri dhamira ya CCM ktk kupunguza makali ya vyama vya Upinzani kwani wananchi wanapodai katiba mpya ni kwa sababu hakizao zimepotea kabisa ingawaje kikatiba zipp sheria zinazowalinda na hazifuatwi..

  Umuhimu kwa vyama kuwepo na katiba mpya upo palepale na ni lazima tuwe na katiba mpya inayoondoa madaraka makubwa ya rais na mamlaka makubwa ya chama CCM..

  Hivyo kwa kuangalia interest za pande zote mbili Chadema wasisahau kabisa kushinikiza mambo makubwa yanayowahusu wananchi wote na sii maslahi ya vyama vya Upinzani au muundo wa serikali ya Jamhuri kama wanavyofanya CUF..
  Hawa wamepania kujitenga zaidi ya kuwepo kwa muungano kwani hata ukisikia malalamiko yao mengi ni kwa maslahi ya Wazanzibar na sii Tanzania nzima.

  Chadema kama chama ombebi Wabunge wetu ndio wawe wawakilishi wa hoja za wananchi na ndio watakao wakilisha hoja hizo ktk tume itakayo chaguliwa iwe na rais au chombo chochote..
  Sasa mapendekezo hayo yasipokuwepo ndani ya katiba mpya ndio mnaweza kuanzisha vagi jipya lakini kwa sasa hivi swala la katiba lisichuke muda mwingi wa kuwawakilisha wananchi ktk matatizo sugu yaliyopo ikiwa ni pamoja na haki ya kumiliki ardhi zao, nyumba na mashamba wanayodhulumiwa, haki zao za madai ya kustaafu, mishahara kima cha chini na kadhalika..

  Kilimo kwanza pamoja na umuhimu wake pia umechangia mfumko wa bei za bidhaa kutokana na ongezeko la matumizi ya zana za kilimo kwa mkulima..Hilo pia serikali ilitakiwa kulitazama toka mwanzo kwani green revolution ya India walikabiriwa na matatizo makubwa sana na sisi tulitakiwa kuyatazama yote haya..ikiwa ni pamoja na athari zote za matumizi ya mbegu zakisasa na sii kutegemea kilichowezekana Ulaya basi bila shaka kitafanya kazi kwetu ktk mazingira tulokuwa nayo...
   
 4. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maana yake nini?
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,077
  Trophy Points: 280
  kwani mpaka leo ni mambo mangapi yamezushwa na CCM/serikali kuamisha fikra za CDM na bado wamegota ...hapa mwanzo mwisho,ni katiba, viwanja vya ndege,meli kubwa,reli,maji,hospitali za rufaa ..hata kama vitashindikana watakaoulizwa 2015 ni nani? CDM/CCM? kwa maana waliopewa ridhaa ya kuunda serikali ni CCM ...wakishindwa tunaomba wananchi waipe CDM ridhaa 2015
   
 6. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,146
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  " NILITÀRAJIA SUALA HILI KUFANYWA KWA UMAKINI"
  Lakini tayari nauona mushkeli wa kwanza kabisa,nao ni lugha inayolazimishwa kutumika "ENGLISH" kwa wananchi asilimia 80 hawana uwezo wa kuielewa wala kuiongea.
  AG anaposema tutafsiriwe na wakalimani.mbona kwenye kampeni hawatembei na wakalimani afu waongee english na wananchi tutafsiriwe na alafu waone matokeo ya KURA?
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  silly .......
   
 8. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  CDM siku zote wakijichanganya kukaa mezani na ccm lazima walegee wenyewe kwani CDM hawana dhamira ya dhati wapo kimaslahi na ccm wamesha wasoma, Ndio maana CDM wakiwa nje husukumizia kwa wananchi wenyewe ndio tupige makelele na sio wao tuliowaagiza kutupigia makelele kwa mafisadi. wewe unadhani kwa jinsi walivyokuwa wamesha anza kufulia na walikuwa na usongo wa fedha wangefanyaje? ivi pale walikuwa walikuwa wanawaza kusign
   
 9. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  pathetic!
   
 10. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #10
  Apr 6, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Chadema ni chama makini chenye watu makini si chama legelege chenye watu wenye fikra mbinuko kama wenge wanavyo fikiri. Naamini makamanda wamejipanga sawasawa hasa ukichukulia wizara ya katiba na sheria iko kwenye mikono salama ya Tingatinga Tundu Lissu.

  Kila kitu kitaeleweka tu na kitafanyika kwa muda muafaka. Nani alitegemea kuwa swala la kagoda lingerindima tena jana? Wengi naamini walitegemea sana vumbi kutimka kwenye muswada wa katiba. Kilichotokea wenyewe tumeona.
  Tusivuke daraja kabla ya kulifikia kazi ya utabiri tuwaachie wanajimu.
   
 11. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nge watamu hao?
  Ndo jinsi CCM itakavyodhani ina-swallow Chadema bila kujua kuwa inameza sumu inayoimaliza yenyewe.
  For every trap made by CCM, CDM is devising reverse trap. Ni mambo ya counterintelligence na CDM wamebobea kwa hayo.
   
 12. E

  EMMA KIWIA New Member

  #12
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri suala ni katiba mpya na sio mapitio ya katiba, ok kwa muswada uliopekwa bungeni jana tarehe 05 Aprili/11 vyama vya upinzani, pamoja na watanzania wapenda mabadiliko bado tupo gizani kujua ni nini hasa lengo la serikali? Muswada huo ambao kabla hata ya kupelekwa bungeni ulishakoselewa na wadau mbalimbali wakiwamo waliohudhuria Kongamano la Katiba Lililoandaliwa na UDASA. Baada ya majadiliano nafikiri muswada huu ukipekwa bungeni utapitishwa kwa kishindo na wabunge wa chama tawala ambao ndio wengi. Ni wakati wa wabungebila kujali itikadi kuonyesha uzalendo wa kweli kwa kuukataa muswaada huu. Kwa upande wa Chadema ni chama makini chenye watu makini si chama legelege chenye watu wenye fikra mbinuko kama wenge wanavyo fikiri. Naamini makamanda wamejipanga sawasawa.
   
 13. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nadhani ushauri huu umekuja mda muafaka sana,hasa ambapo chadema wana jiandaa na phase ya pili ya maandamano nchi nzima,najua watatumia hili la katiba kama filimbi ya kwanza,lakini kweli kabisa wasisahau kuwakumbusha wana kigoma kudai "dubai" yao kama walivo sahau kuwakumbusha wana kagera kudai "mv bukoba mpya" na kwingineko
   
 14. l

  lemberwa Member

  #14
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe kupeng'e acha upuuzi wako nani bongo lala kati ya ccm na Chadema?
  CCm inayoongozwa na akina Tambwe Hiza kwa kweli wewe ni Dada Poa
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kumbe bishosti bado upo... Naskia ushachafua hewa Uganda aisee
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Apr 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Tatizo moja kubwa ni wachache kuutumia ujinga walioutengeneza kwa faida yao binafsi

  CCM wamezaa taifa la maskini na wasioelimika na sasa wanatumia umaskini na elimu ndogo kuburuza mambo...
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280

  unatafuta kutukanwa tu hapa...we shauri zako
   
 18. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Usipoteze muda kujibu pumba yoyote ya Kipeng'e
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hawa wako kuharibu tu topiki za watu...
   
Loading...