Mussa Azzan Zungu, pamoja na Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Mheshimiwa Lt. Jen. (Mst) Yacoub Hassan Mohamed, walikutana na Spika wa Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Saqr Bhogash, Abu Dhabi tarehe 25 Novemba 2025.
Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha uhusiano wa kibunge baina ya Tanzania na UAE, na yameazimia kuunda kamati ya kudumu ya ushirikiano. Kamati hiyo itaratibu masuala ya pamoja, ikiwemo ziara za Wabunge na viongozi wa Mabunge ya pande zote mbili, kubadilishana uzoefu na kuimarisha uwezo katika masuala ya kibunge.