Msimlaumu Musonye sana kwani yeye ni mchumia tumbo tu ila nashangaa TFF kujiingiza kwenye kadhia hii kwa kukubali kuteua timu nyingine wakati ikifahamu kuwa wachezaji wote waliochaguliwa na yanga ni wale waliosajiliwa na kupewa leseni na TFF. Musonye amekuwa kama fisi mwenye tamaa ya kuona mikono ikianguka ili apate ulaji.
Leo hii ukimuuliza musonye cecafa wamejitahidi namna gani kukuza soka katika kanda yetu hakuna jibu kwani wanashindwa hata kutafuta wadhamini wengine ili mashindano hayo yawe ya manufaa zaidi kwa klabu shiriki.