Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Mahakama ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, imemuhukumu Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Butiama. Lawrence Mbaso (62), kifungo cha miaka saba jela.
Mbaso ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Butunguli wilayani humo, alikutwa na hatia ya kujifanya wakili wa Serikali na kuomba rushwa ya shilingi 300,000 kwa Mwananchi mmoja ili amsaidie katika kesi yake ya jinai. Hakimu Mwandamizi wa mahakama hiyo, Richard Maganga alimhukumumu baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashtaka na wawili wa upande wa utetezi usiokuwa na shaka.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa Polisi Theophil Mazuge kuwa, Januari 27 mwaka huu, saa 3 asubuhi, katika eneo la viwanja vya mahakama hiyo, Mbaso alijitambulisha kwa Monica Hokokoro, kuwa Wakili wa Serikali.
Mazuge alidai siku hiyo mshtakiwa huyo alisema alifika mahakamani hapo kuendesha kesi ya jinai namba 14 ya mwaka 2015, akidai kuwa anamwakilisha Kisuri Mayuya.
Alisema kufuatia maelezo hayo, mwanamke huyo alimtilia shaka na kuwajulisha maafisa wa polisi waliomkamata siku hiyo ya tukio na kumpeleka Kituo kikuu cha Musoma.
Alisema wakati anakamatwa tayari alishapewa na Mayuya, sh.180,000 za awali kati ya sh. 300,000 alizoomba kama gharama ili amsaidie Mayuya katika kesi yake.
Alidai Desemba 13, 2015, alijipatia sh. 180,000 kutoka kwa Mayuya, ambaye alikuwa na kesi ya kuvunjiwa duka lake na kuibiwa vitu akijitambulisha kama Wakili wa Serikali ambaye angemsaidia katika kesi yake.