MANI
Platinum Member
- Feb 22, 2010
- 7,320
- 6,376
.
Polisi wa Tz kwa sisiem ni sawa na Kibwetere na waumini wake.
.
Au mbwa kwa chatu !
.
Polisi wa Tz kwa sisiem ni sawa na Kibwetere na waumini wake.
.
Na hao polisi wana matatizo! Sijui kama wanafahamu Polisi ni jeshi? Wanapewaje amri na mtu asiye tambulika jeshini na wao wanakubali tu?
Magamba wanazidi kulowa. Maji yanazidi unga.
Wakati Mahakama ya Rufaa Kanda ya Dar es Salaam ikitoa hukumu ya kumrudishia udiwani na kumthibitisha Kamanda Ulole Ulole kuwa Diwani halali wa Kata ya Kijitonyama dhidi ya Abdalla Bulembo wa CCM leo, jana huko kwenye manispaa ya Musoma, Mwenyekiti huyo wa Wazazi Bulembo alikutana na nguvu ya umma akalazimika kuomba Jeshinla Polisi kuinusuru CCM mbele ya wananchi wa mji huo.
Ilikuwaje! Alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Musoma siku moja baada ya mkutano wa CHADEMA chini ya Kamanda Vincent Nyerere na Godbless Lema.
Hoja akawa hana au zikamwishia au hakujiandaa kama ilivyo kawaida ya magamba. Akaanza kutukana mbunge Vincent na wananchi wa Musoma waliomchagua. Akisema CCM ndiyo wenye serikali, ndiyo wanaotoa fedha, na yeye anazungumza kama Mjumbe wa Kamati Kuu na M-NEC, hivyo kwa miaka miwili au mitatu iliyobaki kabla ya uchaguzi mkuu serikali ya chama hicho haitatoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa watu wa Musoma kwa sababu walichangua mbunge wa CHADEMA.
Wananchi wakavumilia. Wakaendelea kusikiliza. Unajua hata mjinga mpe muda uujue ujinga wake unapoanzia na unapoishia. Akaanza kujilinda na kujishtukia. Anasema yeyote atakayeharibu mkutano wake ataamurisha polisi wamkamate. Akatoa amri kwa polisi kuwa yeyote atakayekaidi agizo lake la kukamata raia, atafukuzwa kazi na yeye anazungumza kama Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na M-NEC. Na kwamba kuanzia sasa CCM wataagiza watumishi wote wa umma ambao wanakaidi maagizo ya viongozi wa CCM, wafukuzwe kazi mara moja.
Watu wakaendelea kuvumilia. Na ukisikia watu wa Musoma wanavumilia, basi ujue wamevumilia kweli kweli.
Akaendelea kufyatuka. Akasema, DC wa Musoma kama walivyo ma-DC wengine nchi nzima ni makada wa CCM na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM ya Wilaya, hivyo watawajibika kutoa taarifa zozote zile kwenye mikutano ya CCM wala hawataweza kufanya hivyo kwenye mikutano ya Mbunge (hata kama ni mkutano wa kiserikali), kwa sababu ni mbunge wa CHADEMA.
Sasa ukawadia wakati wa maswali na majibu. Shughuli ikaanzia hapo.
Swali la kwanza; mwananchi akauliza, sasa kama CCM inasema inaweza kutoa amri kwa vyombo vya dola kuwakamata na kuwashughulikia wananchi kwa kutoa amri tu, kwa nini wasitumie amri hiyo na uwezo huo huo kuagiza mafisadi wakamatwe na fedha za Uswisi zirejeshwe. Oooh! Kosa kubwa. Bulembo akatoa amri pale pale 'kamata huyo'. Yule muuliza swali akadakwa pale pale na mmoja wa maaskari waliokuwa pale. Kitu cha kushangaza sana askari aliyekuwa akikamata ni dereva wa gari la polisi anayepaswa kuwa kwenye usukani muda wooote.
Swali la pili; mwananchi akahoji kwamba wao wanavyofahamu ni kwamba DC ni kiongozi wa kiserikali, sasa kwa nini kwenye mikutano ya CHADEMA ambayo inakuwa na watu WENGI viongozi kama yeye hawaji au hawafiki kutoa taarifa kwa wananchi badala yake wanakuja kwenye mikutano ya CCM ambayo inakuwa na watu wachache. Oooooh, kosa! Bulembo, Mwenyekiti wa Wazazi wa Magamba, akatoa amri tena mwananchi yule akamatwe. Akakamatwa palepale.
Kitumbua kikaingia mchanga. Watu uvumilivu sasa ukawashinda. Uonevu una mwisho wake wa kuvumiliwa. Mawe yakaanza kurushwa. Ikawa mawe Vs risasi za moto kutoka kwa PolisiCCM. Taarifa zinasema askari mmoja amejeruhiwa.
Mpaka mwisho jumla ya watu watano walikuwa wamekamatwa. Labda wameongeza wengine baadae.
1. Emmanuel Charles, mwalimu wa Shule ya Sekondari Mwembeni
2. Wabunda Biseko
3. Said Ally
4. Mwinyi Ramadhan
5. Bakari Ramadhan
Sasa kazi kutwa ya leo alikuwa nayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ambaye aligeuzwa au alijigeuza kuwa PRO wa CCM, akiwakusanya waandishi wa habari, akiwatongoza sana wasitoe hiyo habari. Haijajulikana kafanikiwa kiasi gani. Tusubiri tuone kuanzia jioni hii kwenye vyombo vya habari;
Nawasilisha wana bodi...
Gazetini:
Hili swali linafaa aulizwe IGPPolisi anamkataje raia bila kujiridhisha kuwa huyo raia ametenda kosa? Kuambiwa na DC au mjumbe wa NEC kuwa amkate raia haiotoshi, lazima polisi aridhike na sababu zilizotolewa. Sasa kuuliz swali ni kosa?

Nawasilisha wana bodi
Gazetini:
Bulembo umejiaribia CV