Nikikumbuka Rais Kaguta Museveni ameishi hapa Tanzania kwa kipindi kirefu
Kwanza wakati akisoma hapa UDSM
Pili wakati akiwa katika harakati za kumng'oa Idd Amin Dada. Huyu alikuwa rafiki mkubwa sana wa Mwl Julius Kambarage Nyerere, bila shaka hata yeye alimpenda sana Mwalimu kwani aliunga mkono jitihada zake za kuikomboa Uganda. Museven amekuwa na ndoto za kuja siku moja kuwa Rais wa kwanza wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ili aje atawale Afrika Mashariki inabidi awepo madarakani hadi hapo akichaguliwa, hii imebidi ageuke kama dictor nchini kwake kwa kitendo chake cha kubadilisha vipengele vya katiba ili kumwezesha azidi kuwepo madarakani. Hilo sisi kama Watanzania halituhusu.
Kilichonisukuma kuandika "Museveni hata wewe?" ni ubaridi wa mahusiano tunaouona toka kwa Mh. Yoweri Kaguta Museveni dhidi yetu Watanzania, ameungana na vijana wadogo kumpiga mawe "Baba yake Mlezi". Tanzania ni Baba mlezi wa Rais Museveni kwani alizaliwa kiakili akiwa UDSM, ikawa asubuhi ikawa jioni Mwl Nyerere akaone ni vema akamwambia Museveni inuka mwanangu nenda hadi nchi nitakayo kuonyesha yaani Bukoba, nenda ukapige kambi hapo ukabiliane na hasimu wako Idd Amini, Museveni akaitikia ndiyo Baba, akafunga safari kuelekea Bukoba. Mwalimu Nyerere akaona ni vema ikawa jioni ikawa asubuhi Mwalimu akamwambia Museveni chukua vijana wako wa uzao wako walete hapa kambini Bukoka nao wawe pamoja nawe wakipata mafunzo pamoja nawe kumkabili hasimu wako Idd Amini.
Aliweza hatimaye kumkabili akisaidiwa na Mwalimu hadi kumng'a Idd Amini Dada, akaiongoza Uganda hadi leo. Sisi Watanzania hatuwezi kuamini kama naye ameungana na vijana kuihujumu Tanzania kwa kuitenga katika nyanja na harakati za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kama ndivyo basi hakika naungana na manabii wa kale waliosema "Shukrani ya punda ni mateke" Ni mateke kwanini kisiwe kichwa. Museveni umetugeuka kwa lipi sisi Watanzania??? Waache hao vijana wacheze makida makida kwa muda halafu wataelewa nini Tanzania ilivyo, wewe ungana na sisi rudi nyumbani mwa Baba yako Mlezi, Tanzania!!!
"Mwalimu Nyerere akaona ni vema ikawa jioni ikawa asubuhi Mwalimu akamwambia Museveni chukua vijana wako wa uzao wako walete hapa kambini Bukoka nao wawe pamoja nawe wakipata mafunzo pamoja nawe kumkabili hasimu wako Idd Amini."
Na katika vijana wake aliowachukua na kuwaleta walikuwamo akina Kagame. Sasa anakabiliwa na tatizo awakane vijana wake au baba yake!