Museven Ashinda Urais Uganda

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
museven-884x1024.jpg
Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi.

Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu.

Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye alipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.

Awali, waangilizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola walikuwa wamekosoa uchaguzi huo wakisema kulikuwa na kasoro nyingi.

Aidha walishutumu kukamatwa kwa mgombea wa upinzani Dkt Besigye na kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.

http://globalpublishers.co.tz/museven-ashinda-urais-uganda/
 
Attachments

  • Museven Ashinda Urais Uganda.jpg
    Museven Ashinda Urais Uganda.jpg
    68.7 KB · Views: 41
museven-884x1024.jpg
Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi.

Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu.

Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye alipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.

Awali, waangilizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola walikuwa wamekosoa uchaguzi huo wakisema kulikuwa na kasoro nyingi.

Aidha walishutumu kukamatwa kwa mgombea wa upinzani Dkt Besigye na kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.

http://globalpublishers.co.tz/museven-ashinda-urais-uganda/
wazungu ni lazima warudi tena kutawala waafrika .
 
Nakumbuka clinton akiwa rais aliwasifia museveni, meles zenawi, paul kagame na yule wa Eritrea kama new breed of african leaders. Uliona mbali sana!
 
Hawa waangalizi wanakuja tu kuangalia Mali zao Kama zipo salama basi ila sio uangalizi wa uchaguzi Africa hamna demokrasia ya kweli
 
Kama hali ndio hii hakuna haja ya kuleta sanduku la kura mbele ya wananchi.
 
Back
Top Bottom