Musalia Mudavadi: Kenya haina Ugomvi na Majirani

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Waziri wa Mambo ya Nje, Musalia Mudavadi, amekanusha ripoti za kuwa Kenya ina uhusiano mbaya na majirani zake, licha ya mizozo kadhaa iliyotokea hivi karibuni ambapo alisisitiza inatatuliwa Kidiplomasia.

Kenya inakabiliwa na kesi ya usambazaji wa mafuta na Uganda, pia Januari 16, 2024 ilimaliza mzozo wa usafiri wa anga na Tanzania. Januari 5, 2024 Sudan ilimrejesha nyumbani Balozi wake baada ya Kenya kuwa mwenyeji wa Mohamed Dagalo (kiongozi wa vikosi vya wanamgambo wanaopigana na Serikali)

Aidha, Desemba 17, 2023, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pia ilimrejesha nyumbani Balozi wake wa Nchini Kenya baada ya muungano mpya wa waasi wa Kikongo wakiwemo M23 kuundwa Jijini Nairobi

..........


Kenya's Foreign Minister Musalia Mudavadi has denied reports of deteriorating relations between the country and its neighbours, despite a number of recent disputes which he insisted were being resolved diplomatically.

Kenya has a pending oil distribution case with Uganda and only last week settled an air travel dispute with Tanzania.

Earlier this month, Sudan recalled its envoy after Nairobi hosted the head of the paramilitary Rapid Support Forces Mohamed Dagalo, who is engaged in a civil war with the Sudanese army.

In December, the Democratic Republic of Congo also recalled its ambassador in Nairobi after a new coalition of Congolese rebels was formed in the Kenyan capital.

In a speech on Sunday though, Mr Mudavadi insisted that Kenya was on the frontline in championing peace in the region.

"My brothers in the media, Kenya is not at war with any of its neighbours," he added.
Article share tools

Source: BBC
 
Vyote hivyo wanavyomtuhumu navyo kenya ni kuwa viko nje ya uwezo wake. Kenya ina uwezo mdogo sana wa kujilinda yenyewe. Ndiyo maana inaitwa a hot bed for terror. Watu wote wabaya na wenye hila kwa Afrika, wakitaka kupanga njama wanakuja Nairobi. Kwa kenya mgeni anaweza kuja na kuingia na kukaa huku akifanya jambo lolote lile analota na kuondoka. Hawana udhibiti na nchi yao. Hakuna ulinzi madhubuti wa ndani. Ndiyo maana Mackenzie akawa anaua watu kwa mamia, kwa miaka, lakini hakuna aliyeweza kumuona. Hivyo kama uansi wa nchi za ukanda huu unatokea kenya msimlaumu. Bali ni wa kumsikitia. Ila pia kwa hili EAC inabidi wamkemee kwamba anapaswa kuwa makini ili machafuko ya nchi jirani yasiwe yanaratibiwa kenya. Kenya isitumike kama kituo/kiini cha mahangaiko ya nchi jirani.
 
Back
Top Bottom