Shalom!
Mithali 29:2
Waovu wakitawala, watu huugua; bali wenye haki wakitawala, watu hufurahi. Mpendwa Neno hili linatuonyesha wazi kuwa uongozi ni baraka au laana kwa watu, kutegemea tabia ya kiongozi.Kiongozi katili, dhalimu, au asiye na huruma huleta mateso, woga, na uchungu kwa watu wake. Watu hupoteza matumaini, amani na maono. Lakini kiongozi mwenye haki, anayesikiliza watu na kutenda kwa upendo na haki, huleta furaha, utulivu na maendeleo. Daima Mungu anachukizwa na viongozi wanaowatesa watu wake, kwani mamlaka yote yanatoka kwa MUNGU. Warumi13:1 inasema na kiongozi anatakiwa kuwa mtumishi wa watu, si bwana wao. Tumuombe sana MUNGU atupe hekima ya kumjua yeye na tuwe wanyenyekevu na wenye hofu ya Mungu.