Habari ya Leo wakubwa,bila shaka mnaendelea salama na majukumu yenu.
Nina mpango wa kuanzisha mradi wa kufuga nguruwe kibiashara na Nina eneo la hekari moja.
Ninaomba kujuzwa mambo yafuatayo;
1.Mbegu nzuri ya nguruwe hasa kwaajili ya kuzaa na nyama.
2.Bei ya kununulia nguruwe wadogo huanzia bei ipi Hadi ipi?
3.Kwa kuanza na nguruwe 15 natakiwa kuwa na kianzio Cha mtaji wa shilingi ngapi Hadi kuja kuanza kuwauza?
4.Changamoto ya ufugaji nguruwe.
5. Tahadhali ninazotakiwa kuwa nazo kabla na wakati wa kuanza ufugaji.
Asanteni