Dr Orb
Member
- Aug 4, 2019
- 10
- 40
Uzi huu unaletwa kwenu na
Orb Tech LLC.
Ni muendelezo wa uzi huu Muongozo wa software developer anaeanza
Software development ni idara pana sana na ni ngumu mno. ugumu huwa mkubwa zaidi kwa wale ambao wataamua kutumia mfumo wa Learning kuliko studying. Kama moja ya wahanga wa mfumo huu wa Learning lakini wadau wakubwa wa mfumo huu napenda kubadilishana nanyi mnaopenda kuingia katika tasnia au mliopo machache ambayo yanaweza kuwasaidia safari yenu ikawa rahisi kidogo kuliko iliyokuwa kwangu.
Binafsi imenichukua takribani miaka 2 to Learn software development, safari ambayo imekuwa na changamoto za kila namna zilizopelekea kukata tamaa katika vipindi tofauti lakini nikaendelea kujipa moyo, na hatimaye sasa hivi mambo si kama iliyokuwa hapo awali.
Uwezo na uwelewa juu ya tasnia hii kwa sasa ni tofauti kabisa na miaka 2 iliyopita. hivyo nimejiridhisha ya kwamba natosha kutoa chochote ambacho kinaweza kuwasaidia wale wanaonza na waliopo.
Tuanze hivi, software development ni ujuzi wa kutengeneza programu za kompyuta ambazo zinaweza kutumika katika vifaa mbalimbali vilivyo na mifumo ya kompyuta ndani yake kama vile saa janja, simu janja na kompyuta mpakato. vifaa hivi hufanya kazi kwa namna tofauti na mifumo yao ya kompyuta huwa na tofauti kidogo kiutengaji.
Utofauti huu unapelekea tasnia hii kuwa ngumu zaidi na inayokulazimu kujifunza vitu vingi. lakini pia maendeleo ya tekinolojia ya kila siku ni moja vitu vinavyoongeza ugumu wa tasnia. na hali huwa ngumu zaidi kwa wale wanaoanza kuwekeza nguvu zao huku.
Turejee maana ya Software, ni mlolongo wa maelekezo unaotoa maelekezo kwa vifaa vilivyo ndani ya kompyuta kuhusu namna gani vishirikiane kufanikisha jambo fulani. Maelekezo haya hutolewa kwa lugha maalumu kwa mpangilio wa kipekee, lugha hizi huitwa Programming languages.
Kuna makundi makubwa mawili ya software, system software hizi ni maalumu kuunganisha vifaa vya kompyuta ili kufanikisha muingiliano wa majukumu mbalimbali ya kompyuta. na kundi la pili ni Application software hizi ni maalumu kwa ajili ya kufanikisha majukumu mbalimbali ya kibinadamu, mfano kuandika, kufanya mahesabu n.k.
Application software hufanya kazi juu ya system software, yaani system software husaidia kuleta maelewano kati ya application software na vifaa vya kompyuta na kufanikisha muingiliano.
System software dev. ni pana mno inahitaji uwanja mkubwa wa uelewa na ushirikiano na wanataaluma wengine mfano wataalamu wa vifaa vya kielectroniki. software hizi pia huihitaji rasilimali nyingi mno ambazo si rahisi kuzimudu mtu binafsi.
Application software hizi hazihitaji uwelewa mpana sana kama system software lakin kuna mengi ya kujifunza. ujuzi wa kutengeneza software hizi hauhitaji ujuzi wa ndani sana wa vifaa vya kompyuta lakini unahitaji ufahamu vitu vya msingi kuhusu computer.
Hivyo kama unataka kuanza safari hii unaweza kuchagua ni aina gani ya software unataka kujikita huko. Baada ya kuchagua aina ya software
Jambo la pili ni kuchagua kifaa ambacho ungpenda kuwekeza ujuzi wako kama vile;
Simu, Kompyuta mpakato, smartTV, vifaa vingine vya majumbani kama magari n.k.
Baada ya kuchagua kifaa yafuatayo ni mambo ya jumla ya kufuata, mapendekezo haya yamezingatia kwamba vifaa vyote vina mfumo wa koompyuta ambao utendaji kazi wake ni sawa.
Baada ya kuchagua kifaa na kujifunza ujuzi wa jumla wa kompyuta au kifaa chako nini kifuatacho.
Bonyeza hapa kuendelea sehemu ya pili
Stay tuned.

- Unapaswa kujifunza ujuzi wa jumla wa kompyuta (ujue kuwasha na kuzima kifaa husika, ujue namna gani mfumo wa kompyuta unafanya kazi katika kifaa husika, ujue aina ya system software ambayo kifaa kinatumia, ujue kutengeneza, kufuta, kuhamisha, na kufungua mafaili mbalimbali katika kifaa, ujue mgawanyo wa hifadhi ya kifaa (disk partition) na ujue ni wapi system software ilipo na wapi application software zilipo, ujue kusimika na kuondoa programu katika kifaa, ujue kuandika kupitia application mbalimbali za kifaa chako n.k)