Muongozo wa CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muongozo wa CCM!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by vukani, Jul 17, 2012.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Jana nimekutana na kijitabu kidogo cha kijani kwenye maktaba ya baba yangu. Kitabu hicho kimeandikwa "MUONGOZO WA CCM" ambacho kilichapwa mwaka 1981, na Printpak.

  Wakati nakipitishia macho nikavutiwa sana na vifungu vilivyoandikwa ukurasa wa 77 na wa 80. Naomba ninukuu maneno hayo hapa chini.

  Ukurasa wa 77.

  (6)WIZI WA MALI YA UMMA , HUJUMA ZA KIUCHUMI, MAGENDO NA UJAMBAZI.

  Kumekuwa na ongezeko kubwa la uhalifu wa aina mbalimbali nchini tangu tupate uhuru. Uhalifu wenye kutia wasiwasi maalum ni uhalifu wa kiuchumi. Wizi wa mali ya umma umeanza kuwa ni jambo la kawaida. Kumekuwa na matukio ya baadhi ya maafisa kuhusika na kuidhinisha mikataba na makampuni ya nchi za nje bila kujali maslahi ya Taifa. Wakati huo huo vipusa, dhahabu na mali mbali mbali a Taifa zinatoroshwa nje ya nchi kwa magendo na kusababisha hasara kubwa kwa Taifa.

  Ujambazi wa kutumia silaha nao umetumika ili kunyang'anya mali na kutisha wananchi.
  Chama kitahakikisha kuwa Serikali inachukuwa hatua kali za kupambana na vitendo hivi vinavyodhoofisha uchumi wa Taifa. Iko haja pia kwa sasa ya kubuni sheria maalum zitakazoelekezwa kwenye vita dhidi ya uhalifu wa kiuchumi unaozidi kuongezeka"

  Mwisho wa kunukuu kipengele hicho.

  Halafu ukurasa wa 80, nao ulikuwa na maneno haya:

  92.
  watu wameanza kuthamini zaidi vitu kuliko utu na tamaa ya kujipatia mali bila kuitolea jasho inaenea, matukio ya wizi wa mali ya umma yameongezeka. Lakini lililo baya zaidi ni kuwa mwizi wa aina hiyo anapogunduliwa, baadhi ya wananchi, badala ya kumfichua au kulaani kitendo chake, humsifu na kumhusudu. Wakati mwingine mvivu na mtegaji kazini hutetewa hata na vyombo vya chama vyenyewe. Wakati huo huo bado kuna mabaki ya tabia ya kupuuza elimu ya shule kwa watoto na badala yake kuna wazazi wanaopendelea watoto wao wachunge mifugo au hata kuolewa badala ya kuendelea na shule...........na blah blah blah blah blah nyingine zinaendelea..............................

  Mimi nimesoma tu nikaona ni vyema nikashirikisha wasomaji wa JF kutafakari huo muongozo wa CCM, ulioandikwa hapo mnamo mwaka 1981.
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Hivyo vilishachomwa moto Lumumba. Vinatukataza kufanya yale tunayoyafanya kwa nguvu zote
   
 4. W

  WEMBE WENGE Senior Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nAKUSHAURI TOA PHOTOCOPY KITABU CHOTE NA UBAKI NA PHOTOCOPY HALAFY HIYO URIGINO UITUME CCM MAKAO MAKUU KWA ADDRESS IFUATAYO:

  NAPE NAWIE,
  KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI.
  CCM MAKAO MAKUU
  P.O.BOX......
  DAR-ES-SALAAM/DODOMA.

  AKIONE MWENYEKITI NA KATIBU MKUU WA CCM

  Labda atakumbuka vilivyoandikwa na baba yake mzee NNawie. vikapitishwa ma Mlm Nyerere.
  inaweza kuwafanya wajutie ufisadi na kuipenda Tanzania yetu ambayo inaliwa kila kona mpaka CDM watakapoichukua itabaki mashimo na mbuga tuu, madini yoooote hakuna, misitu yooote hakuna.

  halafu tuwaulize yale Matrekata pale JKT Lugalo ndipo kilipo kilimo kwanza???????? kama si ufisadi ni nini?
  CCM hatuwawezi kila mtu ana dili lake, mtu kaanza ooo kilimo kwanza kumbe ana akili yake kandua kuna pesa za matrekta. kwa bidii akaagiza mengiiii akijua kuna mabilioni atavua humo. tukifuatilia kampuni iliyoleta, magumashi, bei yake magumashi, nimesikia bungeni wakisema haa clearing costs pia magumashi,,, eeee makubwa,
  Someni mipango ya wazee wenu muijenge nchi. hta hayo mabilioni yaliyopo uswiss yasingekuwepo badala yake yangenunua vitabu na madawati kwa ajili ya watoto wetu.
   
 5. MKL

  MKL Senior Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 126
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  NAPE si mtoto wa Mzee Nnauye hili likukae kichwani kama si rohoni, unakumbuka alipoanza chokochoko za UVCCm mjane wa baba Nnauye alimkana waziwazi? na baada ya hapo uliibuka ukweli? kuanzia leo elewa kuwa Nape si mtoto wa Nnauye na usimshangae kwa roho ya kifisadi aliyonayo ni kuwa hiyto sio Roho ya Mzee Nnauye ni ya Fisadi moja linaumwa kwa sasa.
   
 6. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 80
  Katika kitabu "TANU NA RAIA" kilichoandikwa na JULIUS K. NYERERE cha mwaka 1962 katika kipengele cha uongozi wa tanu aya ya tatu mwalimu anasema 'Asili ya uongozi wetu ni mbili: Ya kwanza ni WATU .Hatukutumwa kutoka katika mwezi kuja kuongoza watu wa nchi hii. Wala sisi si viongozi wa kikoloni kwamba tulitumwa na serikari ya kigeni kuja kuongoza watu wa nchi hii. Uongozi wetu hauna budi utokane na watu wa nchi hii, bila hila, bila rushwa, bila vitisho na ujanja wa aina yoyote, Tunapofika katika uongozi kwa kupitia mlango wa hila, au rushwa, au ujanja wa aina nyingine yoyote, basi hatukutokana na watu wenyewe.
  Asili ya pili ya uongozi wetu ni HAKI. Tuliunda tanu iondoe ukoloni pamoja na maonevu pamoja na dhuluma za aina yoyote zilizoambatana na ukoloni. Lakini HAKI NI HAKI kwa WATU, sio kwa majani au miti. Basi, tukifika katika hali yetu ya uongozi kwa njia yoyote ambayo si ya HAKI, ni wazi kwamba haiwezekani tuwe tumetokana na watu wenyewe. Japo kama uongozi wetu haukutokana na kura za watu, bali niwa kuajiriwa, ni wazi kuwa tumeufikia kwa njia za hila, rushwa, vitisho au ujanja wa aina yoyote, hauwezi ukawa uongozi wa HAKI na hauwezi ukawa uongozi wa WATU. WATU NA HAKI ni misingi ya uongozi ambayo haiachani.
  Nikisema hivyo siyo kwamba kiongozi asiyechaguliwa na WATU hawezi akatenda yaliyo ya HAKI. Anaweza. Maana yangu ni kwamba walinzi wa HAKI za WATU ni watu wenyewe. Kutegemea haki zao zilindwe na viongozi wasiotokana nao ni jambo la kubahatisha.
   
Loading...