Muonekano wa jengo la TAMISEMI litakavyokuwa

Muonekano wa jengo la TAMISEMI litakavyokuwa

mamayoyo1

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
1,011
Reaction score
1,019
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imekuja na maajabu mpya kwa kujenga Jengo la Kisasa litakalokuwa na mvuto wa kipekee katika mji mpya wa Serikali Jijini Dodoma.

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imekuja na maajabu mpya kwa kujenga Jengo la Kisasa litakalokuwa na mvuto wa kipekee katika mji mpya wa Serikali Jijini Dodoma.

Ujenzi huo unatekelezwa kwa kutumia utaratibu wa manunuzi ya moja kwa moja ‘Force Account’ na utagharimu Sh.Bilioni moja ambazo zimetolewa na Rais Dk.John Magufuli kwa kila Wizara.

Jengo hilo litachukua watumishi zaidi ya tisini pamoja na kumbi mbili za mikutano ikilinganishwa na majengo mengine yatakayochukua watumishi chini ya arobaini.

Kupitia utaratibu huo kuna kamati nne za ushindi zimeundwa ili kufanikisha ujenzi ambazo ni Kamati ya Manunuzi, Kamati ya Vifaa, Kamati ya Ujenzi, na Kamati ya Usimamizi na ufuatiliaji.

Katika kufanikisha ujenzi huo, TAMISEMI inatumia kitengo cha Ujenzi cha Chuo Kikuu Mbeya kama fundi wa ujenzi huo chini ya Wakala wa Majengo(TBA) kama mshauri.

Aidha, kamati ya ujenzi ya TAMISEMI iliyo sheheni wahandisi wake kutoka makao makuu wanasimamia kila kipande cha ujenzi huo ili kuendana sambamba na ushauri wote unaotolewa na TBA kwa lengo la kupata jengo bora zaidi.

Katika kufanikisha mapinduzi hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo alitoa maelekezo mahususi kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ambayo ni Taasisi iliyo chini ya usimamizi wa Ofisi ya TAMISEMI kuhakikisha unajenga jengo la aina hiyo pia kwa kutumia fedha za ujenzi walizonazo kwasasa.

Amesema hataki kuona Taasisi hiyo inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kupanga jengo na kwamba ifikapo Julai mwaka huu, agizo ambalo TARURA wameanza utekelezaji wake.

Kasi ya ujenzi wa jengo hilo inawapa changamoto Wakuu wa Mikoa, Wilaya, na Wakurugenzi wa Halmashauri hapa ambao wamepewa fedha za ujenzi wa ofisi lakini bado wanasuasua. Hili ni jambo la kutafakarisha kwa viongozi wote wa Mikoa, Wilaya, na Halmashauri zote nchini.
 
Kwenye hii picha Jafo yu wapi?

2.jpeg
 
Watumishi kufeni njaa tunajenga kwanza mji wa kiserikalI Dodoma.

Nimepita jana wanakojenga huu mji wa kiserikali maeneo ya Ihumwa/Mtumba hapa Dodoma kwa hakika ni lazima hela iende nyingi tu maana kila wizara ujenzi unaendelea.

Yaani kila wizara na kiwanja chake na jengo lake na eneo liliotumika ni kubwa sana na hapo miundombinu bado haijaanza kuwekwa zaidi ya barabara tu zilizochongwa kuwezesha ujenzi ufanyike
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Watumishi kufeni njaa tunajenga kwanza mji wa kiserikalI Dodoma.

Nimepita jana wanakojenga huu mji wa kiserikali maeneo ya Ihumwa/Mtumba hapa Dodoma kwa hakika ni lazima hela iende nyingi tu maana kila wizara ujenzi unaendelea.
huna mawazo ya msingi kwani hao watumishi hawalipwi mshahara??KWA KWELI WAPINZANI UCHWARA MMEISHIWA VYA KUSEMA TAFAKARI KWA MAKINI KABLA HUJA POST UJINGA WAKO
 
huna mawazo ya msingi kwani hao watumishi hawalipwi mshahara??KWA KWELI WAPINZANI UCHWARA MMEISHIWA VYA KUSEMA TAFAKARI KWA MAKINI KABLA HUJA POST UJINGA WAKO
Wewe hujui mateso na shida watu wanazopata hivyo kaa kimya.

Hivi sasa hata madeni watu hawalipwi acha promotion zilizosimama kwa mwaka wa nne sasa huu.

Mngefanya haya mambo kwa awamu wale isingekuwa tatizo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mbona hayo majengo yatakuwa madogo madogo sana kama hayatakuwa na wafanyakazi ziadi ya 50. Tofauti na baadhi ya majengo ya wizara kipindi zipo Dar.
Yaani hilo la TAMISEMI ndio linaonekana litakuwa jengo kubwa kuliko yote na hizo wizara nyingine ni kama gorofa moja moja tu.
 
Naomba picha ya itavyokuwa Mfugale fly over na ilivyokuja kuwa.
 
Force Account’ na utagharimu Sh.Bilioni moja ambazo zimetolewa na Rais Dk.John Magufuli kwa kila Wizara.

Yeye kazipata wapi hela zote hizi?

Haya ni maajabu zaidi ya jengo lenyewe. Yaani sasa akili zetu zimeelekezwa kila kitu kiwe ni kumsifu mtu?

Jengo ni la kawaida tu hilo. Mchoraji hawezi kujizolea sifa kwa ubunifu wowote katika muonekano wa jengo ulivyo..
 
Wewe hujui mateso na shida watu wanazopata hivyo kaa kimya.

Hivi sasa hata madeni watu hawalipwi acha promotion zilizosimama kwa mwaka wa nne sasa huu.

Mngefanya haya mambo kwa awamu wale isingekuwa tatizo
Wewe unayajua???? Umewasaidiaje??? Kulalamika jf??? Je chama chako kimewasaidiaje tofauti na kulialia??? Je ni kosa kwa vyama vya siasa hata kutoa elimu ya ujasiriamali au mikopo kwa wananchi?? Kama chama chenu tu kimeshindwa hata kuanzisha miradi au saccoss za kusaidia wasiojiweza hata wanachama tu sembuse watumishi????

Nonsense!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom