Mungu usituache,sikia kilio chetu!

AZUSA STREET

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
2,007
1,893
Eee Mungu, Muumba wa mbingu na nchi, wewe ndiwe Mungu wa kweli, wewaza kutuokoa hata sasa. wewe ni Mungu wa haki, haki hutawala mbele zako milele na uovu na dhuluma hazitakushida wewe. Tunakuomba iponye Tanzania, tunakuomba ikomboe Tanzania, tuokoe toka kwenye mikono ya watesaji, wauawaji, wale wanaoleta huzuni katika mioyo ya watu, wale wanaotesa raia wasio na hatia, wao wanategemea nguvu za mwili, wanategemea waganga wa kienyeji, wanategemea bunduki na silaha za mwili, sisi tunakutegemea wewe Mungu ambaye haujawahi kushindwa, na hautakuja kushinda milele, uweza wako ni wa milele, nguvu zako ni za milele, haki yako hutawala milele na hautamwacha mtu atuonee milele.

usifurahi eeh adui yangu, niangukapo nitasimama tena. Eeh Mungu tunayaleta haya kwalo leo, yale yanayotuumiza mioyo yetu:
  1. Angalia Tundu Lisu alipigwa risasi mchana na watu wasiojulikana
  2. Angalia binti wa watu jana anatoka shule amepigwa risasi Kinondoni
  3. Angalia watu wanavyookotwa kwenye fukwe za bahari
  4. Angalia watu wanavyoishi kwa hofu na mashaka, hawana amani
  5. Angalia uchumi ulivyodorora, hakuna pesa mtaani, shida zimezidi
  6. Angalia watoto wetu wanavyokosa mikopo vyuo vikuu, ni wengi mno
  7. Angalia mishahara ya watumishi haipandishwi wala vyeo vyao
  8. Angalia watu wanavyofukuzwa kazi kwa upendeleo
  9. Angalia watu wanavyokamatwa bila makosa ya msingi na ya haki
  10. Angalia wanaosemekana na vyeti feki wamefukuzwa lakini wapo wengine hawafukuzwi
  11. Angalia watu walivyokosa furaha na amani,
Tunayaleta haya na menginie meengi kwako, wewe mwenyewe uhukumu, haki yako itamalaki, wewe kama hakimu wa wote, yule mwenye haki ukampe haki yake na yule anayedhulumu akapewe pia anachostahili, ninakuomba haya yote kwa Jina lako Takatifu la Yesu Krsto aishiye milele, Amina!
 
Tatizo sis wabongo ni waoga sana, ndo maana hatuna maendeleo,, na tutakufa hivihiv mpaka mungu atakapo rud, tanzania nchi ya waoga sio nchi ya amani hata kidogo,,,, woga wetu ndo umasikin wetu...... So sad
 
Km hujui haki na wajibu wako ktk taifa lako wataka Mungu ajibu kuhusu nini?

Rubbish
dawa pekee ya mtu mwenye nguvu za kimwili, ni kuingia kwenye maombi unapigana naye kiroho halafu itadhihirika kimwili atakapodondoka kwa kishindo. sisi wengine huwa hatupigani kimwili, tunapigana kiroho. tukipigana kimwili hatuna bunduki, hatuna jeshi, hatuna polisi etc, ila kiroho tunavyo hivyo vyote. tuwashitaki tu kwa Mungu ili hakimu wa wote asimame katikati atoe haki kwa anayestahili. tumeshoka.
 
ukufungua mioyo ya watz leo hii mmojammoja uangalie walivyo na machungu, walivyoichukia serikali kuanzia rais hadi balozi wa nyumba kumi, walivyo na vinyongo moyoni....utakimbia nchi kabisa. hili ni jipu ambalo siku likija kupata mlango wa kutumbuka linaweza kuleta hatari kubwa sana. watu wana hasira sana halafu watawala hawalijui hilo au wanalijua lakini wanadharau. mnaweza kutumainia uchawi na waganga, wasoma nyota wenu na hao wanaowatabiria kuwa hakitatokea kitu lakini jueni hayo ni mashetani tu, shetani kama baba wa uongo kuna siku atawaingiza kwenye mtego mlioutega wenyewe na mtanasa. vilio vya wazazi wa akwilima Mungu avisikie na atoe haki kwetu nyote kuania juu mpaka chini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom